TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

Walikuwa wapenzi, hidaya Alikaa pia Congo enzi za pepe Kalle. Walizaa watoto watatu. Mmoja alikuwa na mwili mkubwa kama babake.
Watoto wake wawili walilowea Congo maana baada ya kifo cha baba yao aliwaachia utajiri mkubwa.
Hidaya yeye alirudi bongo kuja kumuuguza mamake baada ya hapo hakurudi tena Congo.
Hidaya kafariki akiwa tajiri haswa
Lazima atakuwa njema tu wewe si unaona hata huyo binti yake na safari za ughaibuni?
 
Watu wanaanzia mbali aisee! Awilo na hao jamaa wengine umewataja. Awilo hakuwa akisikia tofauti na hawa wengine. Nakumbuka mzee wangu alikuwa akinunua kila kaseti ya alubamu ya huyu mzee Pepe Kalle
Congo DR nzima ukitafuta wapiga Drums ( Wakaanga Chips ) bora waliowahi kutokea na waliopo lazima uanze na hawa....

Mac Macaire alipiga mno na TP Ok Jazz ya Marehemu Franco, kidogo Pepe Kalle na anamalizia kwa Aurlus Mabele.

Awilo Longomba aliyepiga mno na Pepe Kalle.

Titina Alcapone ( a.k.a Le Grand Prete ) aliyepiga mno na Bendi yangu pendwa ya Wenge Musica BCBG yake Kipenzi changu JB Mpiana kabla ya kwenda Kustaafia kwa Bendi ya Quarter Latin yake Koffi Olomide.

Seguen Mignon Maniata huyu anapiga na Bendi ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana na ndiyo Roho ya Bendi nzima na Kipenzi chake JB Mpiana na Mtu anayeaminika nae zaidi kwani hata Maji ya Kunywa ya JB Mpiana hushikwa nae huyu Seguen mpaka Chakula au Mvinyo wa JB Mpiana awapo katika Tamasha Ukumbini hukaguliwa nae Kwanza huyu Mpiga Drums wake Seguen Mignon Maniata na huyu Seguen akikuchukia ndani ya Bendi hiyo hukai na unafukuzwa.

Papy Kakol anayepiga na Wenge Musica Maison Mere yake Ngiama Makanda ( wengj mnamjua kama Werrason )

Ramatoulaye Diabate anayepiga na Bendi ya Extra Musica Zangul Zangul yake Ibambi Ikombi ( wengi mnamjua kama Roga Roga Missile )

Wapiga Drums wote wa leo ( sasa ) wanawaiga hawa Wakubwa zao niliowataja hapa kwani wanajua kweli Kuzikaanga hizo Chips ( Ngoma ) zao.
 
innalillah wainna ilayh rajiuun,poleni sana.....kumbe arusha walikuwepo wazuri wa kimataifa kama huyo mama!
sikuwahi kujua hii aisee.
 
Walikuwa wapenzi, hidaya Alikaa pia Congo enzi za pepe Kalle. Walizaa watoto watatu. Mmoja alikuwa na mwili mkubwa kama babake.
Watoto wake wawili walilowea Congo maana baada ya kifo cha baba yao aliwaachia utajiri mkubwa.

Hidaya yeye alirudi bongo kuja kumuuguza mamake baada ya hapo hakurudi tena Congo.

Hidaya kafariki akiwa tajiri haswa
Hidaya yeye ni kabila gani?
 
Ilikuaje Hadi akaimbwa na Pepe!!!???
 
Huyu hidaya alikuwa mpenzi wa Pepe kale pia wakazaa watoto watatu wawili wamelowea Congo sababu waliachiwa Mali nyingi.

Pia huyo huyo hidaya alirud Tanzania kuja kumuuguza mama yake.

Huyo huyo hidaya kafa akiwa Tajiri sana.

Pepe kale kathibitisha alimuona hidaya Mara moja tuu na nafsi ilimkubali sana na kuweka Nia ya kurudi Tanzania japo hajui atamkuta Morogoro au Arusha.

Sasa wewe unamzungumzia hidaya yupi?

Ntapita nije niwaone kina Pepe kale hapo na kuwapa pole
Hivi Allan Kabasele aliyekuwa Akudo naye ni damu ya Pepe Kalle?
 
Nimepoteza kipenzi changu hapa Tanzaniaa[emoji445]
Nimepoteza kipenzi changu hapa Tanzaniaa[emoji445]
Kama kule arushaaa sijuiii[emoji445] au morogoroo sijuiii[emoji445]
Nitarudiii[emoji445] nitarudii kwa ajili ya hidayaaa[emoji445]
Nitarudii[emoji445] nitarudiii kwa ajili ya hidayaaa[emoji445]
Nimepoteza[emoji445] mkanda wa kiuno[emoji445] nitarudiii nitafutieni ichoo[emoji445][emoji445]

Daah Hidaya alikua n mrembo sana vjana wa zaman walitesekea sana hyo chombo lakn zama zinakuja na kondoka na mwsho wetu wote n umauti
 
Hivi Allan Kabasele aliyekuwa Akudo naye ni damu ya Pepe Kalle?
Mkuu utafute wimbo wa "safari sio kifo" kuwahusu hao Akudo, kisha, kabla Allan Kabasele hajaanza kughani kimadoido, Christian Bella atakuwa ameshakupa jibu kwa mwitikio wa sauti zake za nyuma. Akhsante!
 
Back
Top Bottom