TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

Hidaya alitoa gari kwaajili ya kumbeba Pepe Kalle kutoka KIA mpaka Arusha alipoenda kufanya show.

Hidaya alijaaliwa uzuri wa kila eneo, basi ukichangia na ule uchangamfu na ucheshi wake, Kabasele Yampanya "Pepe Kalle" akamtungia wimbo maridadi sana uitwao "Shikamoo Seye" akiuimba kwa lugha adhimu ya Kiswahili...
Hivi ulikuwa ni urafiki wa kawaida tu uliopelekea Pepe Kalle kumtungia wimbo au Pepe alikuwa akimla kabisa huyo Hidaya?
 
anakumbukwa baadanyankufariki.mimi sikujua kama huyu Hidaya alikuwa ni mtu wa kweli nilidhani pepekale aliimba tuuu
Sema uliyekuwa hujui ni Wewe tu peke yako usiyependa Kufuatilia mambo mbalimbali.

Kwa taarifa yako tu huyu Hidaya wa Pepe Kalle alijulikana na wengi tokea miaka ya 2000.

Na ungekuwa unafuatilia sana 'interviews' za Wanamuziki katika Redio na Tv za Tanzania ungejua.

Miaka ya 2000 walikuja akina Papy Text, Dilu Dilumona na Rapa ( Atalaku ) Bileku Mpasi ( Djouna Mombafu ) Waandamizi wa Bendi ya Empire Bakuba yake Marehemu Kabasele Yampanya ( Pepe Kalle ) wakasema.

RIP Hidaya wa Pepe Kalle kwani ulimkuna zaidi Marehemu Pepe Kalle kwa Urembo wako uliotukuka.

Na hata Wimbo wenyewe pia ulitendewa haki hasa upande wa Vyombo ambako katika Gitaa la Solo alisimama mwenyewe Dally Kimoko ( Gitare Enzanga Likwanza ) akisaidiwa na Dilu Dilumona kisha upande wa Rythm Gitaa alikuwepo Lokasa ya Mbongo na upande wa Bass alisimama 'Mwamba' Lofombo ( Baguna Bass ) huku katika 'Drums' akiwepo Awilo Longomba ( ambaye leo hii ) kawa Muimbaji.
 
Kwanini Pepe Kalle alimuimba Hidaya, any detailed story?
Walikuwa wapenzi, hidaya Alikaa pia Congo enzi za pepe Kalle. Walizaa watoto watatu. Mmoja alikuwa na mwili mkubwa kama babake.
Watoto wake wawili walilowea Congo maana baada ya kifo cha baba yao aliwaachia utajiri mkubwa.

Hidaya yeye alirudi bongo kuja kumuuguza mamake baada ya hapo hakurudi tena Congo.

Hidaya kafariki akiwa tajiri haswa
 
Walikuwa wapenzi, hidaya Alikaa pia Congo enzi za pepe Kalle. Walizaa watoto watatu. Mmoja alikuwa na mwili mkubwa kama babake.
Watoto wake wawili walilowea Congo maana baada ya kifo cha baba yao aliwaachia utajiri mkubwa...
Asante sana Mkuu
 
Hidaya aliyeimbwa na Pepe kalle,Mola akulaze pema, mama Hidaya alikuwa akiishi Arusha Mtaa wa Kaloleni
 
Walikuwa wapenzi, hidaya Alikaa pia Congo enzi za pepe Kalle. Walizaa watoto watatu. Mmoja alikuwa na mwili mkubwa kama babake.
Watoto wake wawili walilowea Congo maana baada ya kifo cha baba yao aliwaachia utajiri mkubwa..
Huyu hidaya alikuwa mpenzi wa Pepe kale pia wakazaa watoto watatu wawili wamelowea Congo sababu waliachiwa Mali nyingi.

Pia huyo huyo hidaya alirud Tanzania kuja kumuuguza mama yake.

Huyo huyo hidaya kafa akiwa Tajiri sana.

Pepe kale kathibitisha alimuona hidaya Mara moja tuu na nafsi ilimkubali sana na kuweka Nia ya kurudi Tanzania japo hajui atamkuta Morogoro au Arusha.

Sasa wewe unamzungumzia hidaya yupi?

Ntapita nije niwaone kina Pepe kale hapo na kuwapa pole
 
Sema uliyekuwa hujui ni Wewe tu peke yako usiyependa Kufuatilia mambo mbalimbali.

Kwa taarifa yako tu huyu Hidaya wa Pepe Kalle alijulikana na wengi tokea miaka ya 2000..
Watu wanaanzia mbali aisee! Awilo na hao jamaa wengine umewataja. Awilo hakuwa akisikia tofauti na hawa wengine. Nakumbuka mzee wangu alikuwa akinunua kila kaseti ya alubamu ya huyu mzee Pepe Kalle
 
Back
Top Bottom