Hii chelewa chelewa ya mshahara inanipa wasiwasi

Hii chelewa chelewa ya mshahara inanipa wasiwasi

Hello,

Ni miaka 7 sasa mishahara tunapokea tarehe 21, 22 au 23. Kama tarehe 21 ikiangukia katikati au mwisho wa wiki mshahara tunaupata tarehe hiyo.

Kama tarehe 21 ikiwa Jumapili au Jumatatu basi Jumanne tarehe 22 tunapata mshahara. Sasa jana tarehe 22 Jumanne kwa kawaida ilibidi watumishi wote tupate mshahara lakini kimya. Mwezi uliopita tulipata tarehe 26 sijui 25.

Kuna nini hapa kati? Je, hii iwe kama alarm kwa watumishi kwamba lolote linaweza kutokea mbele yao? Pay Master ni mpya anajitahidi amudu mazingira au kapu liko na changamoto? Hii mada haihusiani na majibu ya tafuta kazi nyingine nje ya kazi.

Nina shughuli zangu hivyo pesa ya kula si shida kivile. Maana watakuja watu eeeh leo tu unaanza kulalamika
Juzi kati hapa alienda kuhemea Arabia.

Kwani hakuna kilichoingia?
 
Wapi nimesema mama hana pesa ya kulipa Watumishi? Ni hivi, mimi ni Mzabuni najua nisemalo. Kama kuna muhasibu au mtu anayesimamia mfumo wa Malipo ya serikali (MUSE) aseme kama wameweza kufanya malipo ya miradi ya maendeleo hadi OC kama zimelipwa toka mwezi wa 10. Nakwambia nchi haina pesa miradi yote imesimama.
Duh!....zimekwenda wapi hizo pesa ?
 
Jipe miaka 3 au 4 jijenge vyema. Baada ya hapo jijenge zaidi kwa kufanya uwekezaji.

Yaani shughuli za kwako mwenyewe binafsi ambazo zitakuingizia kipato na kuweza kumudu gharama za maisha mbali na kunyanyuka kiuchumi.
 
Kimsingi hamuna malipo yoyote si kwa wakandarasi wala wazabuni wala mradi wowote wa Maendeleo toka mwanzo wa mwezi huu. Hali ni ngumu kibubu kimekauka kabisa.
Upo sahihi!

Ila kwa ambao hawajui watakubishia.
 
DALILI ZINAONYESHA HAZINA HELA NI CHANGAMOTO KWANI NASIKIA HATA ELIMU BURE HAIJAWEKWA YA OCTOBER .
Sio elimu bure, niradi yote ya maendeleo imesimama. Hakuna fedha iliyolipwa toka October ndio maana hata wale wa SGR hawafanyi kazi na wanapunguza watu. Hakuna OC Maofisini wala malipo ya fedha za maendeleo. Kama kuna mtu yupo kwenye mfuml ule wa MUSE aseme hapa kama nadanganya.
 
Mtu kaanza kazi mwanzo wa mwezi, tarehe 1, kwanini alipwe mshahara tarehe 22? Au 12 kama ulivyotoa mfano?
Kwahyo kwakuwa watumishi wanatofautiana siku ya kuanza kazi kwahyo...unapropose kila siku iwe ni Siku ya Mshahara kwa kila mtu?

Kwa mfano kuna wanaoanza tarehe 1 kazi 2 mpaka 10 na kuna wengine wanaanza 12 na kuendelea..

Kwahyo kila mtu alipwe kwa Tarehe iliyoanza kazi?
Huoni kama itakuw Vurugu?
Maana leo unaweza ukasikia Fulani leo kapata mshahara,kesho kapata ,mwingine n.k

Na ndio maana kuna standard ya Payroll Iwe siku zinazofanan haijalishi umeanza kazi lini ila tu uwe umeanza kabla ya tarehe 15 ya ujazwaji ya Taarifa za kiutumishi za mishahara HCMIS...

Na kumbuka Tarehe hiyo huwa ni starting point ya Circle ambayo itaendelea Kila mwezi ambayo hukamilisha siku thelethni inaweza ikaanza kwa circle ndogo ila kadiri inavyoendelea huwa sawa..

Kwa mfano unaweza ukaanza kazi tarehe 1 na tarehe 22 ukapata mshahara wa mwezi wa Tatu (lets say)

Ili ifike tarehe 30 tangu upokee mshahara wa kwnza itakuwa Tarehe 22 ya mwezi wa 4 (Unaofuata)..
So iko sawa kulingana na miezi inayofuata sio mwezu uliopo.....

Huwezi kuhesabu kabla hujaanza na Moja hapo moja yenyewe haihesabiki!
 
Back
Top Bottom