Hii Elimu ya Mbunge Erick Shigongo sijaielewa, naombeni kueleweshwa

Vipaji vyake ni vipi?? Kutafsiri story kutoka kiingereza kwenda kiswahili au kuna zaidi ya hapo? Ukiniambia ana uthubutu nitakuelewa.
 
Hawezi kutoboa
 
Si ndo huko tena mlimpa Ubunge??? Mimi nahisi hizi habari zako hazina mashiko!
 
WATANZANIA tuna roho mbaya na husda juu ya mafanikio ya wengine....sijui kasumba hii itaisha lini......ili uweze kupiga hatua unatakiwa uishi na waTanzania katika mlengo wa kiuadui na kimumiani....usidanyanyike na tabasamu lake usoni.......

Sijui tunajisikiaje raha kuona watu wakiteseka.....

Hata huko maofisini badala ya kazi ni majungu na kurogana tu.......
 
Sifa za kuwa mbunge kielimu ni zipi?,
 
Mkuu mwaka 2016 au 2017 I'm not sure ila TCU walisema kuwa mtu mwenye kipaji akasome degrees so ndo alienda huyo Mpiga zumari wa ccm kwa kutumia kipaji Cha kuandika that all.
Mkuu acha utani basi.
 
Bado hujajibu hoja mkuu. Tz inawezekana mtu kutoka la saba kwenda degree?
 
Tatizo hapoo ni kuwa watu wanapopwea digrii za heshima ama kwa vipaji vya au kwa sababu yoyote, wao huziita ni sehemu ya elimu yao badala ya kuziweka kwa kipengele cha "Awards and honors"
 
Tanzania hakuna kuchekana unakuta Chuo Cha Maji harafu maji yanakatika au hakuna kabisa..hakuna ugunduzi wowote tunsofanya zaidi ya kujisifia A za chuo zisizo na msaada wowote...Nchi ina ardhi ya kutosha madini na mbuga ila hatujui tufanye nini na tuanzie wapi tunalia kama vile Nchi ipo Jangwani...
 
Unauliza kwa kugundua wewe au baada ya yeye mwenyewe kusema?
 
kwani palipojengwa chuo cha maji ni lazima maji yawepo muda wote?
Kitu kidogo kama hiki kinakusumbua utaweza kupata majibu kwa vitu Tata kweli...Maji yanapotea mto Ruvu daslm hakuna ukiulizwa unaona sawa tuu wakati wenzetu wameweza kusafirisha Maji kutoka mbeya mpaka Arusha kwa umbali wake nikizungumzia KM hutaelewa...
 
Watu wengi humu mna hiyo degree lakini hata kuandika hamjui.

Kikubwa ni ujinga uliowajaa.Kwani elimu ya degree ina nini cha ziada ambacho mtu hawezi kusoma?Mbona huyu mnayemwita darasa la saba alikuwa na GPA ya 5?

Tatizo kubwa la nchi hii watu wanasoma kupata cheti na si kupata elimu.
Cheti kinatumika kama njia ya kutengeneza madaraja ya wasomi na wasiosoma.
Ukweli wapo wengi sana mtaani wamekosa fursa tu ya kusoma kwa sababu ya umaskini lakini wana akili kuliko ninyi mnajidai hamkuunga.
Inawezekana hata uliopo huwezi kuwa hata mwenyekiti wa kikundi kwa sababu huna uwezo
 
Katibu wa Mbunge unapambana kweri kweri.
Au nasema uongo ndugu zangu?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Naona kampeni za kulitwaa jimbo zimeanza mapema sana
 
Ni kweli, kwa jinsi unavyoandika, sitaelewa!
 
Umemtwanga na kitu kizito hapa
 
Sasa huyu aliyepata utajiri kwa dhuluma ya mali za mjomba wake ana kipaji gani?

Hata biashara zake nyingi ni za dili za kihuni tu. Hukumbuki alikuwa anatoa machozi enzi za jiwe alipokataliwa kulipwa malipo hewa ya t-shirt za ccm??
Na enzi za Magufuri huyo huyo akaukwaa ubunge
 
Shida ya wasomi wana mambo mengi ya kumeza kutoka vitabuni na inapofika kwenye real life wanakuwa kama vilaza kabisa.

Wasomi wengi ukiwasimamisha na kibajaji ili wajenge ushawishi kwa wananchi, nakuhakikishia hutaona tofauti kati yao. Vichwa vingi vya wasomi hasa wa Bongo vimejaa Mfekane war, Kinjenkitile, Kirchofs, Benulier, Bohre theory, Dalton na takataka nyingine. Hakuna applied knowledge. Tunahitaji kizazi kipya cha kuikwamua hii nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…