Hii hapa mikoa 12 inayoendesha uchumi wa nchi, inamiliki na kushikilia asilimia 70% ya uchumi wa Tanzania

Tanga haiwezi kuishusha Mbeya, tuache ubishi wa mwanza na mbeya, ile ni zone kubwa Kwa Tanzania lile ni lango, utake kutoka mbeya, south, zimland, zambia, tswanaland, malawi, halafu kilimo, mpunga, mahindi, uchimbaji wa dhahabu japo chunya yote imejaa wasukuma ndio wanaofaidi dhahabu ile, kitu pekee cha ajabu ni serikali kutowekeza miundombinu bora, mfano uyole na mafiati panakosaje bypass au hata vivuko vya juu Kwa watembea Kwa miguu, haya cocoa ujue kyela ndio ina bei nzuri kuliko Tanga na Moro japo nao wana kokoa, Kwa kesi ya moro ngoja waanze kuexport karafuu tutawasikilizia mbali sana
 
Mikoa isiyo na rasilimali kwa wingi itakuwaje ?
Hakuna Mkoa usio na Rasilimali Kwa Wingi hapa ila mfumo wa Utawala hautoa nafasi ya ufanisi mzuri na ushindani na pia Serikali ndio inaamua kipaombele.

Unadhani kungekuwa Kuna kujisimamia ,Hali ya Maendeleo ingekuwa duni kama ilivyo?

Mwisho nitajie Mkoa ambao unadhani hauna Rasilimali lakini pia Kuna kanuni za mgawanyo ambazo Huwa Zina consider factors zote ikiwemo hiyo unayoisemea wewe.
 
Tabora itaimarika zaidi, kigoma nakubali miradi yao ya barabara ikiisha, watatisha sana , nilifika kasulu miaka mitatu nyuma wale waha biashara wanafanya sana, ni wilaya ambayo niliona wacongo, warundi wanafunga mzigo wa duka pale na magorofa yanajengwa Kwa kasi kubwa hadi unapata hamasa watu wanavopambana
 
Pamoja na kwamba wewe unasema Mbeya ni rangi ila Mbeya inapakana na Malawi tuu,Rango la Sadc ni Mkoa wa Songwe,Tunduma huko ambao ulimegwa Kwa Mbeya.

Mbeya Ina watu aggressive sema nini ,hata kama Walimega Songwe Ile distance ya Tunduma Hadi Mbeya ni fupi so Bado Mbeya ndio Ina influence kote huko na kufaidika na Ile establishment yake Toka Mwanzo.
 
Tanga sio ya kuona, Tanga iliwahi kua na viwanda vingi nyuma huko kuliko hata Dar, ona bandari ikiboreshwa, bomba la mafuta ya uganda likamilike, ile ni strategic zone toka enzi ya mkoloni
Kuna kitu kikiuliwa pale Tanga basi ikuwa na maendeleo sana
 
Kila nikipita Nyakanazi ninakutana na malori yenye plate number zinazoanzia na RA, naambiwa ni malori ya Rwanda yanayopeleka Rwanda makaa ya mawe kutoka huko ulikotaja.
 
Tujenge kituo Cha uwekezaji Kigoma au Tabora kutarget soko la DRC, RWANDA, BURUNDI na Zambia, badala ya nchi hizo kufuata mizigo China ziichukulie Tabora au Kigoma.
Ushauri utazingatiwa.Tungekuwa na kanuni za Utawala zinazoruhusu ushindani hili lingefanyika ila Sasa inategemea Huduma za Wanasiasa wa Chama Tawala 🤣🤣

Ndio maana napinga mfumo wa Utawala huu wa centralization sio mzuri
 
Kila nikipita Nyakanazi ninakutana na malori yenye plate number zinazoanzia na RA, naambiwa ni malori ya Rwanda yanayopeleka Rwanda makaa ya mawe kutoka huko ulikotaja.
Ni hatari. Hayo umeona ya Rwanda ukienda Namanga mpakani au Bandari ya Mtwara ndiyo utazimia kwa wingi wa hayo malori. Lakini ukienda Songea au Mbinga yanakotoka hayo makaa yenyewe wamechoka hadi wanatia huruma.
 
Songwe ukitoa mlowo, tunduma na kiasi isongole, mkwajuni, uende hadi mbalanga huko, mbeya bado ni baba yake sawa na mwanza ilivozaa geita, geita haitokuja kuipita mwanza
 
Hiyo mikoa yote iliyotajwa Kuna key factor moja ambayo mikoa ya Njombe haina.
Idadi ya Watu.
Kuna wenye watu wengi ila wako hovyo eg Kagera,Simiyu,Rukwa nk.

Sema hivi miundombinu ya uchumi ilichelewa na huo ni Mkoa Mpya huwezi linganisha na Mikoa mikubwa but with time itafunguka na itarealise their potential
 
Umejipinda kweli kweli ila inakuaje Mkoa wenye wasomi udai kwamba unatengwa? Si Kila Idara ya serikali mumejaa? Why msijipakulie minyama?

Visingizio fc 🤪🤪🤪🤪
Nadhani wewe ni wale wanaosoma bila kuelewa kilichoandikwa na ni miongoni mwa niliowaongelea kwenye aya ya kwanza. Sasa unasema tumejaa kila idara na unasema tujipakulie ni wapi nimekwambia natokea huko?
Hata hivyo fikiria nje ya box.

Nilipata kusoma sehemu kuna yule mzee wa miaka hiyo aliyesema wajitenge kama serikali inavyowatenga wawe na nchi yao hakukosea kwa nilichokiona na kukipitia. Ndiyo maana nimesema kinachoendelea huko hakiwezi kueleweka kwa wale wasio wafuatiliaji na wapambanuzi wa mambo.J

Juzi juzi hapa tulimsikia Mbowe akisimama na kuongelea masuala ya biashara na uwekezaji. Kuna wakati alitamka neno "wachaga tulitengwa", wengi walimshambulia nikiwemi mimi kwa kuwa alitumia hilo neno la wachaga na ikaonekana ni mkabila lakini baada ya tafakari ya kina na kuzungumza na walioko katika hayo maeneo nilielewa ni kwanini alisema hivyo. Sasa ndiyo sawa na wewe unayesema "mmejaa kwenye kila idara"
 
Sasa usitete watu wavivu
 
Hakuna laana yoyote. Ungejua miradi inayotekelezwa Kagera. Ungekaa kimya tu...
Zaidi ya Km 150 za lami zinajengwa kagera, km 5 za njia nne Bukoba mjini, upanuzi wa bandari za Bukoba na kemondo, kuna meli mpya ya Mv mwanza inaanza safari za Mwanza Bukoba soon...uwanja wa Bukoba unawekewa taa za kuongoza ndege ( kigoma ule uwanja acha tu)...
Kuna miradi ya maji kibao tu ya kusambaza maji vijijini huko kama mradi wa maji kutoa ziwa victoria ( vijiji kibao Bukoba vijijini karibu na kwa kina bashiru ally kemondo vinawekewa maji ya bomba) kuna mradi wa maji wa kyaka... vijiji kibao vina maji ya bomba

Kuna campus mpya ya chuo cha UDSM inajengwa km chache kutoka Bukoba mjini...kwenye mashule na hospital huko usiongee kabisa

Hizo takwimu za makaratasi zisikupumbaze. Kigoma bado sana kulinganisha na kagera. Huo ndo uhalisia...sio kigoma tu mikoa mingi bado sana kulinganisha na kagera...

Siku hiz hadi barabara za vijijini mfano ile ya muhutwe, kamachumu nshamba...na ile ya muleba Rubya zina lami!
 
Nasikia kuna Mzungu alishawahi kufunga safari hadi Geita kwa lengo la kwenda kushuhudia hali ya huo "mji"unaosifika kwa kutoa dhahabu! Alipofika alistaajabu! Badala ya kukuta jiji lililojengwa na kujengeka, alikutana na mkoa uliogubikwa na harufu ya umaskini kuanzia mwonekano wake mpaka watu wake.
 
Hilo swala vyuo sijawahi elewa kwa nini havifunguliwi aisee....wawekezaji walijitahidi wakajenga majengo na wanafunzi walikuwa wanasoma vzr. Serikali ikavifunga mpaka leo. Wamiliki wameomba sana TCU lakini wapi. Huenda leo vingekuwa vyuo kamili vinavyojitegemea...wanasahau watu waliokuwa wamejenga hostels, clubs nk karibu na vyuo hivyo biashara zilivyoharibika...

Hata hiki chuo kipya cha UDSM kinachojengwa hapo Bukoba ni baada ya maprofessor wa kihaya wakina Rutinwa UDSM kuomba sana serikali hadi kushawishi wanakijiji watoe ardhi bure ili chuo kijengwe ( mikoa mingine serikali inanunua viwanja yenyew na kujengwa vyuo)
Chuo kinajengwa sasa....lakin viwanja vyote karibu na chuo vishanunuliwa...na mji wa Bukoba unapanuka kuelekea huko..

Kagera watu wanapambana wenyew
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…