Hakuna nchi duniani ambayo kila mtu anaishi maisha yake tu bila kuhojiwa na bila kutimiza wajibu fulani kwanza. Hata akina P Diddy hawaishi maisha yao tyuuu bila checks and balance. Msiwahadae vijana kuwa wanaishi kuishi watakavyo bila kutimiza wajibu.
Mtu kama mm ndiyo maana nahangaika kuandika humu kila leo kujaribu kupambana na wapotoshaji wa vijana wasiojua hili wala lile.
Mtu kama Lissu, kwake yeye kila mtu hajui ila yeye tu. Mimi ni nilikuwa mwanachadema nina kadi ya karatasi na ya mtandao. Hata hoja ya no reforms no election ni wazo lake yeye wakati wa mkiti Mbowe. Lissu is uncontrolable iwe bungeni, iwe kwenye chama, iwe TLS, iwe kwenye mikutano ya kitaaluma and everywhere. Safari hii amekiingiza chama na wanachama kwenye mtaro wa kina kirefu pale alipowakataza wenzake woooote wasusie uchaguzi wasigombee nafasi yoyote huku akijua yeye alikuwa mbunge kwa miaka 10 mfululizo kwakutumia tume hiihii. Kwa ujuaji wake aliwakasirikia hata akina Halima mdee wakawaita majina ya hovyo kabisa kisa wamekuwa wabunge wa viti maalum.
Sasa chama kimekosa bara na pwani, pangani na bweni, kipo tu kama kundi lenye hasira.