Asante sana kwa muongozo wako. Na nimekupata vzr..
JE kuna hii nyingine unauelewa nayo kama ndio naomba msaada wako kwa uwekezaji wa 20 million kwa mwaka mmoja kwenye LIQUID FUND. Nitapata kiasi gani cha gawio
LIQUID FUND ninayoijua mimi ni miongoni mwa mifuko iliyopo UTT-AMIS. Nadhani unajua UTT-AMIS ni nini hakuna haja ya kuelezea hilo, ila kama hujui basi nijuze nitakuelezea.
Moja ya sifa ya mifuko ya UTT-AMIS interest yake hubadilika mwaka hadi mwaka kulingana na hali ya soko, inaweza ikapanda pia inaweza kushuka: Kwa mfano
2021/22 interest ilikuwa ni 14.7%
2020/21 interest ilikuwa 15.30%
2019/20 interest sikupata kujua ni kiasi gani
2018/19 interest ilikuwa 11.49%
2017/18 interest ilikuwa ni 13.79%
2016/17 interest ilikuwa ni 15.38%
2015/16 interest ilikuwa ni 13.4%
Kwa interest hizo basi, Kama ungewekeza 20M mwaka 2015 gawio lako lingekuwa kama ifuatavyo
2015/16 ungepata 2,680,000
2016/17 ungepata 3,488,184
2017/18 ungepata 3,236,671
2018/19 ungepata 2,669,893
2020/21 ungepata 3,468,493
2021/22 ungepata 3,449,868
Umeona gawio linavyopanda na kushuka? Sababu zipo nyingi ila magawio yao ni mazuri pia. Faida nyengine ya kuwekeza UTT-AMIS, wanatoa compound interest sijui kwa Kiswahili inaitwa vipi hii. Lakini ni nzuri alafu pia huwezi ipata kwenye T-BONDS
Nitakuelezea kwa mfano kuhusu hii Compound Interest.
Mfano
Umewekeza 20M alafu wakatangaza interest ni 13.4% ina maana utapata gawio la 2,680,000. Pesa ya uwekezaji na gawio lako ukaviacha hukuchukua, ina maana utakuwa jumla ya TSH 22,680,000 katika uwekezaji wako. Mwaka unaofuata wakitangaza interest nyengine watapigia hesabu ya pesa iliyopo katika uwekezaji wako kwa wakati huo, yaani 22,680,000 na sio tena 20M. Kwahiyo kama watatangaza faida ni 13.4% basi gawio lako litakuwa 3,039,120 na sio 2,680,000 kama mwaka uliopita.
Umeona gawio lilivyozidi kushindamwaka uliopita?
Hiyo ndo compound interest sasa ila kama ulichukua pesa yako wao wana'calculate pesa iliyomo katika muda husika.
Faida zipo nyingi nyingi,
Faida nyengine ya kuwekeza kwenye huu mfuko unaweza kuuza sehemu ya uwekezaji wako au wote na kupata pesa zako ndani ya siku 3 za kazi.
Wanatoa faida shindani kulinganisha na taasisi zengine za uwekezaji. Ofisi zao zipo mikoa yote nadhani. Ila kwa hapa Dar wapo mtaa wa Ohio jengo la Sukari floor namba mbili.
Fika pale watakupa utaratibu wote, na taarifa zote.
KARIBU SANA