Hii inamaanisha nini, BUNDI kukaa nje ya Nyumba zaidi ya Mwezi kila Usiku na haondoki?

Hii inamaanisha nini, BUNDI kukaa nje ya Nyumba zaidi ya Mwezi kila Usiku na haondoki?

Wakuu wa Jukwaa, leo na mimi nina swali ambalo linakua linanitatiza sana kichwani kwangu kwa muda kidogo sasa.

Nimekua napitia hali ya kujiuliza maswali mengi sana juu ya kiumbe hiki kinachoitwa BUNDI. Bundi ni ndege mwenye sifa kede wa kede. Sitaki kuzungumzia sifa za ndege huyu, leo nimeona niwaulize km mimi ninavyojiuliza imewezekanaje ndege huyu kuishi tunapoishi kwa zaidi ya Mwezi?

Yaan anakuja kila usiku unapoingia kuanzia majira ya saa 4 - 6 mpaka 7 usiku BUNDI anakua kashafika tayari kwenye mazingira yake na anakaa palepale anapokaa siku zote kwenye mti ule ule anaosimamaga siku zote na anatazama uelekeo ule ule anaotazama siku zote (anatazama mlangoni watu wanapotokea na kuingia) yaan ukifungua mlango kwa ajili ya kutoka nje unakutana na BUNDI yupo juu ya mti anakutazama na anakukazia macho haswa, na haondoki hapo mpaka kunaenda kupambazuka saa 11 kuelekea 12 asubuhi ndio BUNDI anaondoka ni km amekuja kulinda nyumba au sielewi, ukimpita anageuza shingo, hapo kabla sikua najua nilikua nasikia tu na kujionea kwenye video za kule Utube km BUNDI anao uwezo wa kugeuza shingo yake kwa jinsi anavyotaka, hii nimejionea mubashara yaani nimejionea bure kabisa bila kwenda kwenye Mbuga au Hifadhi fulani na kulipa kiingilio ili nione.

Sasa basi leo naomba tujiulize kwa pamoja au km yupo mwenye kufahamu atufahamishe inawezekanaje BUNDI kukaa sehemu moja kila unapoingia usiku kwa zaidi ya Mwezi? Na anapofika BUNDI watu waliopo ndani ya nyumba hata waliopo nyumba za jirani usiku wanaweweseka sana, utasikia mtu anaweweseka huko unajua tu tayari BUNDI yupo nje hapo kashaweka kambi, na ukisikia mtu kaweweseka ukitoka tu nje ile kufungua geti tu unamuona bundi yule pale kwenye mti anakutazama, hii ina maana gani wakuu? BUNDI kuweka kambi kila usiku anatutazama nje wakati sisi tumelala ndani, hii inamaanisha nini?

Atakuwa anafukuzia demu hapo kwenu
 
Km unamaanisha kweli na una uhakika kwamba BUNDI anakula Popo nahisi sasa nimeshajua kwanini hawa BUNDI wamekuja kuweka kambi hapa.. ila km ni vinginevyo BUNDI anakula panya, anakula mende, anakula nini kingine?
Hivyo Vyote N.k Pia Yeye Anabonyeza Kiulaini Tu...
 
Mgonjwa wa nini? Ungefafanua vizuri mkuu kumbuka ni zaidi ya Mwezi yupo tena haji mmoja sasa wamekua wanakuja na wenzake watatu km sio wawili, sema huyo mmoja ndio anakua front line yeye ndio anasimama kwenye huo mti anatazama mlango kwa sana na anapenda sana kukaa kwenye huo mti na haogopi hata ukimsogelea (nimethubutu kufanya hivi) labda uonyeshe ishara za kutaka kumrushia kitu ndio anaruka (nilifanya hivyo pia) kisha anazunguka na kurudi tena kwenye ule ule mti
Nimeuliza hilo swali kwa sababu kuna thread inayohusiana na bundi ipo humu,kati ya ninachombuka mmoja wa wadau alisema bundi ana uwezo wa kunusa seli za mtu mgonjwa anae elekea kufariki.
 
Nimeuliza hilo swali kwa sababu kuna thread inayohusiana na bundi ipo humu,kati ya ninachombuka mmoja wa wadau alisema bundi ana uwezo wa kunusa seli za mtu mgonjwa anae elekea kufariki.
Na mimi hilo nalijua ila ni mwezi sasa umepita hakuna aliekufa na hapa hakuna mgonjwa anaekaribia kufa wote ni watu wazima km kuugua ni magonjwa ya kawaida tu maralia, kifua, kikohozi, nk hakuna mgonjwa mahututi kabisa asieweza hata kutembea.. hio ni simulizi ya Kale sana ipo hivi na hata mimi nimewahi kusimuliwa.. km kuna mgonjwa ndani ya nyumba ambae amelala tu hatoki nje, yupo ndani tu haongei hata km anaongea basi ni kwa tabu sana, kutembea hawezi anasaidiwa tu kufanya kila kitu, akitokea bundi akatua juu ya paa la nyumba (elewa ni paa la nyumba) sio mti ulio karibu na nyumba, basi huyo mtu mgonjwa haitochukua siku nyingi atakufa..
 
Uchuro, nuksi, gundu, ushirikina.
Hatima take ni Msiba au Kifo.
Akili za kizamani sana hizi. Tupo karne ya 21 mkuu. Huyo bundi anakuja kujitafutia chakula hao popo, na wengine walioongezeka kawaita wenzake nao waje wajipatie chakula. Hamna cha uchuro wala nini, mamtoni kuna watu wanawapa hadi wenzao bundi kama zawadi, bundi ni ndege kama ndege wengineo, mawazo ya kijima zamani tuliaminishwaa huo upuuzi eti bundi analeta nuksi kumbe ni uongo tu wa ngozi nyeusi kuamini ushirikina.
 
Back
Top Bottom