Hii inamaanisha nini, BUNDI kukaa nje ya Nyumba zaidi ya Mwezi kila Usiku na haondoki?

Kuna panya hapo kwenu anawinda.
Anawasubiria wajitokeze awakamate.
Hiyo kawaida. Kuna sehemu hapa wapo kila siku kwa miaka 3 Sasa.
Wanaingia hadi ndani Mara kadhaa. Hakuna ceiling board.
 

Atakuwa anafukuzia demu hapo kwenu
 
Km unamaanisha kweli na una uhakika kwamba BUNDI anakula Popo nahisi sasa nimeshajua kwanini hawa BUNDI wamekuja kuweka kambi hapa.. ila km ni vinginevyo BUNDI anakula panya, anakula mende, anakula nini kingine?
Hivyo Vyote N.k Pia Yeye Anabonyeza Kiulaini Tu...
 
Nimeuliza hilo swali kwa sababu kuna thread inayohusiana na bundi ipo humu,kati ya ninachombuka mmoja wa wadau alisema bundi ana uwezo wa kunusa seli za mtu mgonjwa anae elekea kufariki.
 
Nimeuliza hilo swali kwa sababu kuna thread inayohusiana na bundi ipo humu,kati ya ninachombuka mmoja wa wadau alisema bundi ana uwezo wa kunusa seli za mtu mgonjwa anae elekea kufariki.
Na mimi hilo nalijua ila ni mwezi sasa umepita hakuna aliekufa na hapa hakuna mgonjwa anaekaribia kufa wote ni watu wazima km kuugua ni magonjwa ya kawaida tu maralia, kifua, kikohozi, nk hakuna mgonjwa mahututi kabisa asieweza hata kutembea.. hio ni simulizi ya Kale sana ipo hivi na hata mimi nimewahi kusimuliwa.. km kuna mgonjwa ndani ya nyumba ambae amelala tu hatoki nje, yupo ndani tu haongei hata km anaongea basi ni kwa tabu sana, kutembea hawezi anasaidiwa tu kufanya kila kitu, akitokea bundi akatua juu ya paa la nyumba (elewa ni paa la nyumba) sio mti ulio karibu na nyumba, basi huyo mtu mgonjwa haitochukua siku nyingi atakufa..
 
Uchuro, nuksi, gundu, ushirikina.
Hatima take ni Msiba au Kifo.
Akili za kizamani sana hizi. Tupo karne ya 21 mkuu. Huyo bundi anakuja kujitafutia chakula hao popo, na wengine walioongezeka kawaita wenzake nao waje wajipatie chakula. Hamna cha uchuro wala nini, mamtoni kuna watu wanawapa hadi wenzao bundi kama zawadi, bundi ni ndege kama ndege wengineo, mawazo ya kijima zamani tuliaminishwaa huo upuuzi eti bundi analeta nuksi kumbe ni uongo tu wa ngozi nyeusi kuamini ushirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ