Hii inamaanisha nini, BUNDI kukaa nje ya Nyumba zaidi ya Mwezi kila Usiku na haondoki?

Km unamaanisha kweli na una uhakika kwamba BUNDI anakula Popo nahisi sasa nimeshajua kwanini hawa BUNDI wamekuja kuweka kambi hapa.. ila km ni vinginevyo BUNDI anakula panya, anakula mende, anakula nini kingine?
Kuna panya maeneo ya karibu. Bundi hupenda kuwinda kwa kuvizia, anakaa sehemu moja tuli kwa muda mpaka panya ajichanganye atoke na yeye anamnyakuwa. Khusu bundi kuhusishwa na msiba, kuna ukweli kwa namna fulani, japo siyo kama watu wanavyoamini. Ngoja nikumegee. Zamani sana, enzi za mababu zetu, wakati hakuna hospital wala nyumba za kuhifadhia wafu, wagonjwa wengi walikuwa wanauguzwa nyumbani. Pia waliofariki walikuwa wanawekwa ndani. Sasa fikiria mtu eg anayeumwa sana, madonda yametoka, ni lazima ananuka. Pia kuhifadhi mwili nyumbani ni lazima kuwe na harufu. Harufu ilikuwa inavutia scavengers na ndege wala mizoga (huwa wana uwezo wa kunusa hata wakiwa mbali). Hii ilifanya watu wahusishe misiba na ndege kama bundi au walao mizoga.
 
Mnaishi polini
 
Mkuu, hapo kunusa cell zilizo kufa unaweza kuwa unatembea mzima lakini bundi akawa ananusa kua celi zako nyingi zimekufa hivyo ukapata msiba.

Mambo ya bundi kwa SISI waafrika inausishwa na BAD LUCK...

NB.MWAKA JUZI NIKIWA HOME SIKU IYO YALIKUJA MAPAKA YANALIA KWA KUNUN'GUNIKA KWA UCHUNGU MKUBWA..YAKAZUNGUKA KWA JIRANI YANGU YAKILIA SANA AISEEEE KESHO KUTWA YULE MZEE MSTAAFU AKAKUTWA JIONI NA MKEWE AMEDONDOKA CHUMBANI KAPIGIZA KWENYE TALES NA KUFARIKI DUNIA NILISHANGAA SANA YALE MA PAKA YALILETA UJUMBE
 
Bundi sometime huwa anakula mizoga!
Na ana uwezo mkubwa wa sense smell ya mzoga, dead body au kiumbe anayekaribia kufa,

Mara nyingi anapoonekana sehemu moja jua yupo kwenye mawindo ya chakula au ame sense Kuna kiumbe anakaribia kufa eneo Hilo maana huwa wanasense mbaka cells zilizokufa kwenye mwili wa mtu,(hapo ndo watu wanasema uchawi)
 
Mhm najua tu bundi ana uwezo zaidi wa kusikia hata mapigo ya moyo wa mnyama na kuona kwa uwezo mkubwa hii ya kunusa kazidiwa mpaka na mbwa.
 
Uwezo wa bundi zaidi ni kuona na kusikia ,kunusa sio silaha yake kubwa
 
Hio ya Mapaka imeshatokea ila ubaya hayo mapaka tunayajua na hapo yalipokua yanapiga kelele ni sehemu ya kiza kinene sana na kwa kawaida wanasema ukisikia paka wanalia ile milio ya majibizano basi jua hapo kuna paka yupo kwenye joto yaan hot period anataka kupigwa miti kwa hio anabembeleza sana apigwe mimba mpaka akishatiwa ndio kelele zinaisha yaan hata ukifukuza watatoka hapa wataenda kulia sehemu nyingine au watarudi tena hapo ni mpaka watiane ndio wanaacha kupiga makelele, hapo kwenye bad luck ya bundi ungefunguka kidogo mkuu maana kuna limitations za kiimani pia ndizo zinazotuzuia kuamini baadhi ya mambo unaweza ukafafanua vizuri kwenye hio bad luck how is it?
 
Many owls tend to stick to familiar, safe roosts for long periods, but habits vary by species and season, with some preferring solitude and others communal living, but site loyalty is a common trait.

Your house is your home and the tree is the owl’s home. Just live in harmony and enjoy the ecological balance!
 
Basi nimeshajua kwanini BUNDI wameweka kambi hapa na hawaondoki kuna Popo nadhani ndio wanaowawinda kila siku usiku, yes hapa Popo wapo kila siku usiku lazima Popo waje, je Popo wanakula nini kingine ukiondoa Mapapai?
Una mti unaoitwa mharadani?
Kama hujui hilo jina, angalia picha za Muntingia calabura. Popo wanapenda hayo matunda na pia wanapenda mazambarao, embe, mitini, mapera, papai, tende n.k
 
Binafisi mim nikikutanisha macho na bundi mwili wote husisimka kwa barid kari na nywere hunisimama, macho yake makari baraa.

Ila bundi kama atakuja usku au ahsubh nakuanza kulia, hutoa taarifa mbaya inakuja.

Kuna bundi huwa anakuja jiran nilipo kuna mti mkubwa na kuanza kulia.
Hazipit siku
Nyingi mtaa wetu unatokea msiba.
Hadi nimesha mnotice nikimsikia tu analia najua tiar kumekucha.
 
bundi ni ndege tuu, alikuwa anakuja saana karibu na ninapo ishi ila siku hizi simuoni na hamna kilichotokea.
 
pia bundi huota mambo yajayo na wapi kutakua na mzoga siku zijazo.
Waganga na wachawi huchanjiwa ubongo wa fisi au ndege fulani hv cjui ni tai au bundi huwafanya watabiri yajayo, pia wanafunz baadh huchanjiwa nakuwa vizur kwenye masomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…