Hii inamaanisha nini, BUNDI kukaa nje ya Nyumba zaidi ya Mwezi kila Usiku na haondoki?

Hawa hua hawalii wanakaa tu, saa 2 nimeona tayari wamefika wapo nje hapo muda huu kwenye mti wao wanaangalia angalia
 
Sasa si ushukuru Mungu amejileta mwenyewe ili umuone anavyogeuza shingo
Make kama ungetaka kwenda national park ingekugharimu fedha nyingi
Duuh hivi unajisikiaje unakatisha unapishana na bundi anakutazama tu ukitembea anageuza shingo mpaka unapoelekea kakukazia macho? Ukimsogelea sana anapaa..
 
Hawaondoki hawa nimefukuza wanarudi tena hapa hapa wamefanya km kwao
Lakini pia niliwahi kusikia kuwa binadamu huwa hafi siku Moja
Kuna process zinatokea kabla ya kifo chake
Hivyo basi Kuna viumbe wamejaaliwa kuhisi hyo hali kabla haijatokea
Na ndio maana unaweza kuwa sehemu fulan ukaanza kushangaa viumbe fulani wanakuja mara kwa mara mfano hao bundi ,Tai nk
N kwamba hao wanahisi mzoga kwahy wanajisogeza pale kwa ajiri ya kupata kitoweo
 
Hapa hakuna mzoga wote tunaoishi hapa ni wazima wa afya kabisa, hakuna mgonjwa anaekaribia kufa hapa ninapoishi kwa hio hio ni negative..
 
Hapo kwenu kuna mawindo mazuri ya bundi.

Kama kuna
1. Panya
2. Mijusi
3. Popo
4. Wadudu

Basi hapo kashafika haondoki.
Cha kufanya fanya usafi wa mazingira na ondoa vivutio vya popo. Weka taa za nje kata hiyo miti ya haradali (popo ndio wanaipenda).

Hizo panya buku nazo weka sumu zidanji.

Baada ya wiki njoo hapa utupe mrejesho.
 
Hapa sasa nimekuelewa vizuri mkuu
 
Mrushie kigae cha chungu hatarudi tena
 
Kata huo mti anapotua
Hata ukimfukuza hapo ukakaa wewe anahamia kwenye mti mwingine haupo mti mmoja, ukiondoka anarudi kwenye huo mti kukaa sasa hivi yupo kakaa tayari mida fulani kwenye saa 2 nilimfukuza akapaa sasa hivi amerudi tena sio mdogo ni mkubwa ila unaweza kumsogelea sema ukimsogelea sana anapaa hataki umsogelee sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…