comrade_kipepe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2019
- 8,748
- 18,096
Kwanza ni usumbufu, mtu kama unakaa zako geza kigamboni, mwanzo ilikua unatoka na gari geza mpaka mkoani kwako, kwasasa itabidi uanze kutoka geza uitafute magufuli.
Tunarudi enzi za miaka ya nyuma za abiria Kuanza kupoteza mizigo, mfano mtu una mizigo Yako umeipakia kwenye bus kutoka rombo, mwanzo ilikua inakufuata Hadi chanika/mbagala na kwingineko, sasahivi itakubidi utoke huko ulipo ufunge tena safari ya kwenda magufuli kuchukua mizigo.
Gharama itapanda sana ya kusafiri, wale wasumbufu wapiga debe wa pale mbezi ni kitu inayokera sana wanavyogombania mizigo.
Kuna ambao wanasema mbona mnatoka kote huko mnaenda kipawa kupanda ndege, sasa najiuliza uchumi wa mtu anaepanda ndege na anaepanda bus ni sawa? Na huwezi kufananisha usafiri wa anga na wa ardhini, Wanaosema hivi nadhani wengi ni wapiga debe, wanufaika na wanaoishi karibu na mbezi mwisho.
Hii kitu itaondoka na kichwa cha mtu, dar sio kama mikoa mingine Kuna watu wengi sana, stendi Moja haitoshi.
Ngoja tuone