Hii kitu ya mabasi yote kuhamia stendi ya Magufuli imeumiza wengi

Kwanza ni usumbufu, mtu kama unakaa zako geza kigamboni, mwanzo ilikua unatoka na gari geza mpaka mkoani kwako, kwasasa itabidi uanze kutoka geza uitafute magufuli.

Tunarudi enzi za miaka ya nyuma za abiria Kuanza kupoteza mizigo, mfano mtu una mizigo Yako umeipakia kwenye bus kutoka rombo, mwanzo ilikua inakufuata Hadi chanika/mbagala na kwingineko, sasahivi itakubidi utoke huko ulipo ufunge tena safari ya kwenda magufuli kuchukua mizigo.

Gharama itapanda sana ya kusafiri, wale wasumbufu wapiga debe wa pale mbezi ni kitu inayokera sana wanavyogombania mizigo.

Kuna ambao wanasema mbona mnatoka kote huko mnaenda kipawa kupanda ndege, sasa najiuliza uchumi wa mtu anaepanda ndege na anaepanda bus ni sawa? Na huwezi kufananisha usafiri wa anga na wa ardhini, Wanaosema hivi nadhani wengi ni wapiga debe, wanufaika na wanaoishi karibu na mbezi mwisho.

Hii kitu itaondoka na kichwa cha mtu, dar sio kama mikoa mingine Kuna watu wengi sana, stendi Moja haitoshi.

Ngoja tuone
Vipi wale wa trenii SGR
 
Nchi Hizi za kijamaa zinajenga hizi mnaita stendi Ili kukusanya pesa Sasa Kila mtu akiwa na stendi yake inakuwa Haina maana.

Binafsi sikubaliani na mambo ya stendi Moja,inakera kama ni lazima kuwa na stendi basi ziwe nyingi kulingana na direction ya njia kuu zilivyo.
 
Leo imekuaje
 
Mwisho wa siku hizi tabu zote chanzo ni kukosekana kwa ujenzi unaofuata masterplan...

Wakazi wamejenga holela, wakati serikali inapambana ku centralize huduma zake...wapi na wapi???
 
Hii ishu ni changamoto Kwa sababu Dar es Salaam ni Jiji 'tata'. Kila sehemu ya Dar es Salaam Ina makazi ya watu wengi sana kulinganisha na miko mingi. Itafutwe suluhu nzuri, mfano, gari zianzie safari Magufuli Bus Terminal, pia zinapotoka mikoani ziingie Magufuli Bus Terminal halafu waombe kwenda huko sehemu nyingine ktk ofisi zao ndogo e.g. Chanika, Gongolamboto, Kigamboni, Shekilango, Mbagala n.k
Mkuu Sasa kuna Abiria atakaeshuka Hapo Magufuli ?
Kwasababu mfano mimi nakaa Sinza siwezi kushuka Magufuli nikiwa na Mizigo nitabski kwenye Bus mpaka Shekilango na Abiria wa Mabibo, Manzese, Magomeni wanafanya hivyo hivyo yani Bus litakua linaingia ndani Stand ya Magufuli na kutoka bila Abiria kutelemka
 
Hata mwanzo watu walikataa kuhamia Digitali kwenye visimbuzi walitaka wabaki kwenye Analogue lakini kwasasa kila mtu anapenda DIGITAL ,no chenga wala kuzungusha Antena.

Watu huwa wanapinga kwasababu ya mazoea ila kadri muda unavyoenda wanazaoe na kuwa kawaida.

Mabasi kwenda Magufuli ina faida nyingi sana kuliko hasara.
Kaka ujue wengine tunaishi mbali na hata kitu inaitwa usafiri binafsi hatuna 😉 halafu kiswahili swahili tukisafiri ni lazima tubebe watoto na mizigo sasa kuanza kuitafuta Mbezi kwenda kupanda basi hiyo ni shughuli pevu hasaa.

Kiufupi kwa wakazi wa nje ya Mji huu ni mwiba mkali.
 
Sasa kwanini iwe kwenye mabasi tu? Mbona hauwahurumii wanaotumia Ferry/Boats na Ndege? Basi wakazi wa Bagamoyo wanaoenda Zanzibar Bakhera awafate Zinga na Wanaoenda Airport/Kipawa basi Serikali iwajengee uwanja karibu na makazi yao siyo kila mtu aende KIPAWA.
Yani bus linafananishwa na ndege, Raha sana
 
daah.

Kaka hao wa ndege ungewatoa hapo.
Nao wana haki sista ya kupelekewa huduma karibu kama wa mabasi wanavyotaka.

Wa kigamboni wajengewe uwanja GEZAULOLE ,wa Bagamoyo/Bunju wajengewe Uwanja KEREGE ,Kisarawe/Pugu/Gmboto watatumia huo huo wa KIPAWA

Wa Mbezi beach/GOBA/MADALE/MBEZI kimara wajengewe uwanja MBEZI MSUMI.
 
Nchi Hizi za kijamaa zinajenga hizi mnaita stendi Ili kukusanya pesa Sasa Kila mtu akiwa na stendi yake inakuwa Haina maana.

Binafsi sikubaliani na mambo ya stendi Moja,inakera kama ni lazima kuwa na stendi basi ziwe nyingi kulingana na direction ya njia kuu zilivyo.
Mkuu ni bora hizi Kampuni zingejenga ofisi zao yani mfano Aboud atatufe eneo lake ajenge Standi yake ila Serikali iweke Muongozo tu na Sheria za Usalama na Mazingira, yani Tufanye kama Timu za Mipira ya Miguu tu Mfano Azam yeye kachagua kujenga Uwanja wake Chamanzi, Simba kachagua Boko, JKT kachagua Mbweni, Hii itasaidia kuwapa Urahisi Wateja na Kampuni za Ma busi watachagua sehemu nzuri ili Boashara zao ziende na Serikali inatakiwa kuweka Vigezo vya Umbali kutoka Kituo A na Kituo B ili kuepuka Msongamano, mfano Kampuni A inajenga Mwenge, Kampuni B inajenga Manzese, na Kampuni C inajenga Banana Ukonga, kampuni C inajenga Chang'ombe.
 
Chalamila ni mkurupukaji wa hovyo kabisa.

Imagine abiria anayetoka Mwanza na bus, afike Dsm saa saba usiku, atoke Magufuli Stand aende nyumbani Mbagala ambapo bus alilokuja nalo linaenda pia Mbagala kwenye yard yao.

Bus linaenda Mbagala tupu huku abiria akitakiwa kuteremka tena atafute usafiri mwingine wa kumpeleka Mbagala, huku bus alilokuja nalo likienda tupu!.

Chalamila amezidi ujinga.
 
Namimi ndio maana naona hii kitu italeta shida sana
 
Back
Top Bottom