Hii kitu ya mabasi yote kuhamia stendi ya Magufuli imeumiza wengi

Hii kitu ya mabasi yote kuhamia stendi ya Magufuli imeumiza wengi

Mkuu Sasa kuna Abiria atakaeshuka Hapo Magufuli ?
Kwasababu mfano mimi nakaa Sinza siwezi kushuka Magufuli nikiwa na Mizigo nitabski kwenye Bus mpaka Shekilango na Abiria wa Mabibo, Manzese, Magomeni wanafanya hivyo hivyo yani Bus litakua linaingia ndani Stand ya Magufuli na kutoka bila Abiria kutelemka
Huu ndio utaratibu uliokuwepo sijui kikatokea Nini wakalazimisha mabasi yote yaanzie Mbezi.
 
Chalamila ni mkurupukaji wa hovyo kabisa.

Imagine abiria anayetoka Mwanza na bus, afike Dsm saa saba usiku, atoke Magufuli Stand aende nyumbani Mbagala ambapo bus alilokuja nalo linaenda pia Mbagala kwenye yard yao.

Bus linaenda Mbagala tupu huku abiria akitakiwa kuteremka tena atafute usafiri mwingine wa kumpeleka Mbagala, huku bus alilokuja nalo likienda tupu!.

Chalamila amezidi ujinga.
Yule jamaa mjinga sana. Mbona kulikuwa hakuna shida yoyote.
 
Ajabu kuna wajinga kama Chalamila wanamtetea mjing mwenzao.

Huku bei za mafuta zimepanda, nauli zimepanda, bado abiria ajilipie nauli ya kumpeleka Magufuli Stand na bado ajilipie nauli ya bus la kwenda mkoani.

Wakati mwanzo ilikuwa mtu anatoka na bus mf. Mbagala anaenda zake mkoani moja kwa moja ana save nauli ya kwenda stand.
Bado hujalipia kiingilio cha stendi.
 
kuna wilaya zinatoa basi kwenda dar via stend kuu ya mkoa mf babat-dar,moshi-dar,makete-dar,ifakara-dar,kahama-dar FULSA MPYA KWA MKOA WA DAR ni kigamboni-mkoa flani,mbagala-mkoa flani kupitia stend kuu ya magufuli
 
Ishu sio mapato tu. Kwa namna Jiji la Dar lilivyo, kuruhusu mabasi kuzagaa mitaani hakuna tofauti na mbwa waliokosa mfugaji.!

Lazima sheria ifuatwe na sio kila mtu kufanya lake.

Kwanini stendi ilihamishwa kutoka Ubungo kwenda Mbezi? Na kwanini sasa wenye mabasi wanalazimisha warudi Ubungo? There is something 'fishy' hususani kwenye mizigo ambayo haina ukaguzi.

Naamini serikali ipo macho, itajua tu. Na njia ya kwanza ni kulazimisha wote kurudi Magufuli na kufuata taratibu.
Hivi walizagaa mtaani au walikuwa kwenye ofisi zao?.
 
kuna wilaya zinatoa basi kwenda dar via stend kuu ya mkoa mf babat-dar,moshi-dar,makete-dar,ifakara-dar,kahama-dar FULSA MPYA KWA MKOA WA DAR ni kigamboni-mkoa flani,mbagala-mkoa flani kupitia stend kuu ya magufuli
Bado Chalamila atapinga. Anataka mtu atoke Kigamboni aje Mbezi mwisho wa mji wakati Kigamboni Kuna ofisi za mabasi pale.
 
Huu ndio utaratibu uliokuwepo sijui kikatokea Nini wakalazimisha mabasi yote yaanzie Mbezi.
Tatizo kampuni zililundikana Eneo moja na pakaonena Mazingira mabaya no ya hovyo yani ukipita pale Shekilango unaona Mazingira siyo Mazuri watu ni wengi na Mabus Yameegeshwa hovyo.
 
Zaman uku make ili uende dar kulikua mtihani maana ilikua upande gari makete ukashuke njombe upande tena gari uende dara ila leo kunja bas ya makete dar via njombe watu wa moro ifakara zaman ilikua apande basi ifakara to msavu ashuke apande nyingine tu dar apo mtu yupo na watoto na mizigo ila leo kuna basi la ifakara dar via msamvu
 
Hata mwanzo watu walikataa kuhamia Digitali kwenye visimbuzi walitaka wabaki kwenye Analogue lakini kwasasa kila mtu anapenda DIGITAL ,no chenga wala kuzungusha Antena.


Watu huwa wanapinga kwasababu ya mazoea ila kadri muda unavyoenda wanazaoe na kuwa kawaida.

Mabasi kwenda Magufuli ina faida nyingi sana kuliko hasara.
Umeshamfikiria mtu anayekaa chanika, gezaulole au tuangoma na anataka kusafiri kwenda mwanza ua arusha
 
Kwanza ni usumbufu, mtu kama unakaa zako geza kigamboni, mwanzo ilikua unatoka na gari geza mpaka mkoani kwako, kwasasa itabidi uanze kutoka geza uitafute magufuli.

Tunarudi enzi za miaka ya nyuma za abiria Kuanza kupoteza mizigo, mfano mtu una mizigo Yako umeipakia kwenye bus kutoka rombo, mwanzo ilikua inakufuata Hadi chanika/mbagala na kwingineko, sasahivi itakubidi utoke huko ulipo ufunge tena safari ya kwenda magufuli kuchukua mizigo.

Gharama itapanda sana ya kusafiri, wale wasumbufu wapiga debe wa pale mbezi ni kitu inayokera sana wanavyogombania mizigo.

Kuna ambao wanasema mbona mnatoka kote huko mnaenda kipawa kupanda ndege, sasa najiuliza uchumi wa mtu anaepanda ndege na anaepanda bus ni sawa? Na huwezi kufananisha usafiri wa anga na wa ardhini, Wanaosema hivi nadhani wengi ni wapiga debe, wanufaika na wanaoishi karibu na mbezi mwisho.

Hii kitu itaondoka na kichwa cha mtu, dar sio kama mikoa mingine Kuna watu wengi sana, stendi Moja haitoshi.

Ngoja tuone
Ushauri wangu kwako,mwombe mtoa maelekezo mbadilishane Hali na hadhi kama kila moja alivyo sehemu unayoishi wewe iwe take na take hapa mjini iwe yako,na hata nyimbani kwenu mkoani mbadilishane,halafu mpeane mrejesho kidogo safi kuwa kila moja amejifinza nini.Halafu wote kwa pamoja mje na mrejesho hapa jukwaani.Nakuomba wewe umshawishi huyu mtoa maelekezo.
 
Hata suala la kuwa na stand ni la kidunia, sidhani kama hata nchi zilizoendelea kila kampuni ya mabasi ina stand yake.
Unalinganisha vipi miundombinu ya wenzetu na hii ya kwetu?

Ina maana mtu anaetoka Mbagala kwenda Mwanza lazima awahi bus masaa manne au matano kabla ya safari ili kuepuka kuchelewa, wakati angeweza kupandia bus hapo Mbagala ajiepushe na usumbufu.

Sijui mnajitahidi kutetea kitu gani hapa!.
 
Back
Top Bottom