Kwa mtu mzima ambaye amekuwa kiongozi kwa muda mrefu, naamini Mh Job Yusto Ndugai ataamua kuachia ngazi ili kulinda kaheshima alikonako. Asipoachia ngazi kabla ya Bunge kuanza basi mambo mawili yanaweza kumtokea:
Ima CCM imuite, imuhoji na kumnyang’anya uanachama na hivyo kupoteza Uspika na Ubunge ama Bunge litoe hoja ya kumvua Usipika na kubaki na ubunge wake. Vyovyote itakavyokuwa, sioni Ndugai akikalia kiti cha Uspika kwenye kikao kinachoanza mwishoni mwa mwezi huu ama mapema mwezi ujao. Ndugai anaondoka, atumie busara kuchagua anaondoka vipi. Aondoke kwa kupokwa uanachama wa kijani ba hivyo kukosa Ubunge na Uspika au ajiuzulu Uspika na kubaki na ubunge wake au wabunge wamuondoe! Bora aondoke mwenyewe as this option is a lesser devil for his situation.
Kwa upande mwingine nilimsikia Mh Rais akisema nyumba ya akina Kassim ilikuwa inasema serikali yake ni ya mpito. Kassim (naamini ni PM), ni kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni, sasa kama Bunge, ambalo yeye ni Mbunge No 1, linamsema Mh Rais basi ni vyema PM naye akaangalia busara katika hilo na hivyo kuachia tu ngazi ili Mh Rais apate nafasi ya kuunda serikali upya kama atataka kumrudisha basi atamteua. Pia Mh Rais kasema kuna Mawaziri wanaoangalia 2025 badala ya kufanya kazi na hivyo atawatoa; PM kama mkuu wa Mawaziri anatakiwa kutumia busara na kuandika kwa Mh Rais ili akae kando na kumpa nafasi Mh Rais kupanga vyema Serikali yake na kuondoa wale wote wenye matamanio ya 2025. Kumbuka PM akijiuzulu Baraza la Mawaziri linapoteza uhalali hivyo kumlazimu Rais kuunda upya serikali kuanzia PM.
Ni imani yangu kwamba kwa hali ilivyo hawa wakuu wawili wanatakiwa kutumia busara na kuamua kumpisha Mh Rais.