Tabia ya tamaa imewaangusha wanaume wengi sana till date: Tamaa ya fedha, tamaa ya kutaka maisha ya juu kupita uwezo, tamaa ya wanawake, tamaa ya kutaka kuyafikia mambo makubwa kupita uwezo.
Mpaka umri huu nilionao nimeshuhudia marafiki zangu 58 wakipata madhira mbalimbali kwasababu ya tabia ya tamaa; Kati ya hao kuna waliopo jela, mahabusu za muda mrefu, kuna waliotekwa na waliouwawa kwa visasi, waliokufa kwa magonjwa makubwa, wengine wanateseka hospitalini kwa mgonjwa yasiyoeleweka
We mwanaume na kijana unayepambana kufikia ndoto zako Nachotaka kukwambia ni kwamba fanya yote kwa kiasi kwa maana TAMAA IKIZIDI KIASI LAZIMA UTENDE DHAMBI, DHAMBI IKIZIDI KIASI LAZIMA UINGIE KIFONI.
Asanteni