Bei ya bidhaa ambazo magufuri alizikuta kipindi ana ingia madarakani ndo alizo ziacha?
Well, ukitaka kulinganisha, tungeanzia kwenye uhalisia wa maisha kitaa...achana na number za ccm.
Mimi ni mtu wa pay cheque to pay cheque, niliona nguvu ta 10k nimeona ilivyoanza kudorora, najua 10k ilipo kwasasa kinguvu ya manunuzi!
Nyumba nilizopanga kwa 250k tabatq, zote ni 400k
Achana na hayo, rudi nyuma kidogo, Mkapa anakabidhi nchi, mkate ulikuwa sh 150, soda sh 250 nadhani, unga robo sh 150 etc, dollar 1 ikiwa chini ya sh 1,800 nadhani.
Miaka 5 ya JK, mkate ukagonga sh 750 mpaka sh 2000 anapotoka. Dollar 1 ikiwa sh 2240 nadhani.
Haya, baada ya March 2021, tukiwa hatuna lolote la kutishia uchumi, tuliona pesa inafurika kwa wachache mtaani, ambao wakasabibisha inflation kubwa. Soko likayumba, wakasema nchi imefunguliwa, wakauza mazao nje kwa pesa ya madafu, mgeni anaingia shambani kujumua, hakuna control...BBT ikaja, ghala likafunguliwa, sukari ikaagizwa, guess what? Nafuu ikawa kwa wale walioko kwenye mifereji tu ambao ni wachache.
Kwa miaka 3, nchi ikakopa kuliko miaka 10 ya raisi yoyote kuwahi kutokea...
- Sababu wanazokupa, miradi ya kimkakati iliyoachwa na mwamba.
- Ukiwauliza, kama miradi ilishaanza, advance payment ilishafanyika...tuambieni, mradi huu umelipwa kiasi fulani, umekamilika, malipo yaliyomaliziwa ni kiasi fulani; hivyo mradi huu na ule na ule, jumla malipo yake ni Trilioni 39.
Vinginevyo, ni upumbavu tu na wewe kuelewa, lazima utakuwa umekabidhi ubongo kwa mwenyekiti kama ilivyo ada AU ni mnufaika wa MFEREJI.