Hii mbunga imekimbiwa awamu hii, watu wanaishi mjini

Hii mbunga imekimbiwa awamu hii, watu wanaishi mjini

Makazi ya Tanganyika hayo na Rais wa pili wa Tanganyika Tundu Antipas Lissu ataweka kambi hapo baada ya 2025. :KasugaYeah:
 
Kwa hili la Ikulu na Ofisi za serikali Dodoma mi binafsi namsifu Magufuli, tatizo ni succession plan zetu ndio huwa hazijulikani.

Kwamba Magufuli aliweza kubana matumizi Mabovu na alikusanya sana na alivyovianzisha vilikuwa vinakimbia, alitangaza vita hadharani kwamba hataki seminars, warsha zisizo na manufaa, safari za viongozi na watumishi wa serikali nje ya nchi zilihitaji kibali kutoka kwake au ofisi ya rais.

Sasa angalia sasa hivi, makongamano,warsha, seminars na mikutano hata haina tija inaandaliwa wanapiga pesa kinachowakutanisha hakieleweki, utasikia wiki ya Madini, mara wiki ya NIDA, mara Wiki ya Vipimo, na n.k. Hizi wiki zinaandaliwa wanakutana Dodoma na kulipana posho bila sababu yoyote ya msingi.

Hizi pesa zingefanya mambo mengi ya maana lakini watawala walifuata, ni kama walifurahishwa na msiba ule, maana sasa wana komba kabisa.

Majumba ya watu binafsi yanakimbia sana, lakini miradi ya serikali inakwama.

Wanaotakiwa kusimamia, na kutuonyesha njia ndio wanaoongoza makongamano, na seminars.
 
Well, ukitaka kulinganisha, tungeanzia kwenye uhalisia wa maisha kitaa...achana na number za ccm.

Mimi ni mtu wa pay cheque to pay cheque, niliona nguvu ta 10k nimeona ilivyoanza kudorora, najua 10k ilipo kwasasa kinguvu ya manunuzi!

Nyumba nilizopanga kwa 250k tabatq, zote ni 400k

Achana na hayo, rudi nyuma kidogo, Mkapa anakabidhi nchi, mkate ulikuwa sh 150, soda sh 250 nadhani, unga robo sh 150 etc, dollar 1 ikiwa chini ya sh 1,800 nadhani.

Miaka 5 ya JK, mkate ukagonga sh 750 mpaka sh 2000 anapotoka. Dollar 1 ikiwa sh 2240 nadhani.

Haya, baada ya March 2021, tukiwa hatuna lolote la kutishia uchumi, tuliona pesa inafurika kwa wachache mtaani, ambao wakasabibisha inflation kubwa. Soko likayumba, wakasema nchi imefunguliwa, wakauza mazao nje kwa pesa ya madafu, mgeni anaingia shambani kujumua, hakuna control...BBT ikaja, ghala likafunguliwa, sukari ikaagizwa, guess what? Nafuu ikawa kwa wale walioko kwenye mifereji tu ambao ni wachache.

Kwa miaka 3, nchi ikakopa kuliko miaka 10 ya raisi yoyote kuwahi kutokea...
  • Sababu wanazokupa, miradi ya kimkakati iliyoachwa na mwamba.
  • Ukiwauliza, kama miradi ilishaanza, advance payment ilishafanyika...tuambieni, mradi huu umelipwa kiasi fulani, umekamilika, malipo yaliyomaliziwa ni kiasi fulani; hivyo mradi huu na ule na ule, jumla malipo yake ni Trilioni 39.

Vinginevyo, ni upumbavu tu na wewe kuelewa, lazima utakuwa umekabidhi ubongo kwa mwenyekiti kama ilivyo ada AU ni mnufaika wa MFEREJI.
Acha ngonjera nime kuuliza bei ya bidhaa alizo zikuta ndo alivyo ziacha?

Magufuri kipindi anaingia madarakani kakuta kg ya sukari ni 1800 lakini mpaka anaondoka kg ya sukari ilikuwa 3000,kakuta bati moja bati moja lina uzwa sh 7000 mpaka anaondoka aliacha bati moja linauzwa 16500,kakuta mfuko wa siment unauzwa 13000 mpaka anaondoka kaacha mfuko wa siment mfuko wa siment unauzwa 22000 hizo ni baadhi tu.
Hizo pesa unazo lalamika kukopwa si zinakopwa kwa ajili kukamilisha miradi iliyo anzishwa na huyo mungu wenu au ulitaka samia aiche?
Alafu mbona Magufuri alikopa pesa nyingi kwa miaka mitano kuliko kikwete aliye ongoza miaka kumi mbona hilo huliongelei.
Ww unadhani kila mtu ana ishi kwa kutegemea uchawa kama nyinyi mlivyo kuwa mnaishi kwa uchawa kipindi cha jiwe sasa hayupo mmebaki na sonona mioyoni mwenu maana mirija imehamia kwingine?
Alafu kipindi cha JPM si ndo nchi ilijaa machinga na boda boda kila pembe ya nchi?
 
kwani hakukuanzishwa mradi wa umeme? tatizo bongo kila mtu na mpinzani tuu pasipo kujua hata anapinga nini
Tatizo sio sisi tunao pinga bali tatizo lipo kwenu nyinyi mnao muona Magufuri kama mungu kiasi cha kufikiri kuwa kila alicho kuwa akikifanya basi alikuwa sahihi na alikiwa hakosei.
Kwahiyo nchi kubwa kama Tz ndo ya kujivunia kuzalisha umeme wa megawat 2000?
Hivi unajua ni adha gani ya maji wanayo kumbana nayo watz hasa wa vijijini?
Shule za serikali zina hali mbaya madarasa utadhani ni mabanda ya nguruwe, hakuna vifaa vya kutosha kufundishia.
Hivi ulisha enda vijijini kipindi cha mvua ukaona wananchi wanavyo teseka kwa sababu ya ubovu wa barabara?
Vipi hayo matirion yaliyo enda kujenga mahekaru ya kifahari ambayo mpaka sasa hayana watu na ndege ambazo mpaka sasa hazijulikani hata zinafanya kazi gani zaidi ya kuitia hasara nchi, yange tumika kutatua angalau %40 ya hayo matatizo niliyo yaandika hapo ni mamilioni ya watz wangapi wange pata unafuu wa maisha?
Unaenda kutumia bilion 700 kujenga daraja la busisi hali ya kuwa jiji la mwanza limejaa barabara mbovu.

Mradi pekee ulio anzishwa na Magufuri ambao unagusa maisha ya wana nchi moja kwa moja ni bwawa la umeme na SRG kwa mbali kidogo lakini mingine iliyo baki ni ilikuwa ni ufujaji wa pesa za uma.
 
sasa ndio umeongea nini mkuu, kwa hiyo daraja sio miundo mbinu? unajua umuhimu wa hilo daraja kiuchumi? anyways unapokua na chuki jaribu na kua positive, hii negativity na ujuaji wetu ndio maana tunashindwa hata kuwatoa CCM maana wati wengi ikiwemo wewe wanaishia tu kua keyboard warriors ambao hata kuchukua hatua ndogo hawawezi zaidi ya kuishia kua wachambuzi na kubwabwaja tu huku hiyo serikali unayoilalamikia ikiendelea kukutawala wewe mpaka vitukuu vyako
 
Hao
Hao viongozi wengine ambao hawakujenga ikulu wa kununua ndege wala kujenga mwabwa ya umeme walilifanyia nini taifa na wamelifanyia nini taifa kama siyo matapeli tu
Kuna kiongozi Kila mwaka alitoa mikopo iliyotosheleza Kwa wanafunzi wa elimu ya juu na akaweka Makubaliano ya marejesho kuwa asilimia nane ya mshahara, na atahakikisha zaidi ya asilimia 80 wanaipata Ajira za kueleweka.
Focus kubwa ikiwa kwa walimu na sekta ya afya! Kila mwaka Ajira zilikua za kupangwa na watu wakiwa vyuoni waliletewa fomu maalumu ya kujaza unalotarajia kwenda kufanya kazi! Akaja Mungu mtu akaongeza Mankato ya bodi ya mkopo kufikia asilimia 15 huku kukiwa na ongezeko la asilimia 6 Kila mwaka kama retention fee! Mbaya zaidi akazuia Ajira zote kwa takribani miaka sita ya utawala wake!
Nadhani unaweza kuona tofauti kubwa sababu yupo aliyewatangulia wote kwa kutumia tu kilimo (GAPEX) Akawasomesha elimu ya juu ya Bure kabisa huku akiwapa mahitaji muhimu!

Ni tofauti kweli sababu hata Ben alipunguza deni la nje kwa asilimia kubwa sana kutaka kuipeleka nchi kujitegemea na ndiye mwanzilishi wa TRA unayoiona sasa hivi. Lakini Jiwe na wenzie wakaigeuza kuwa kikundi Cha uhuni Cha kupora hela za watu Kwa kisingizio Cha Kodi, watu wakafunga biashara! Licha ya takwimu zinazotolewa Kila mwezi kuonesha tra kuvunja rekodi ya makusanyo hakuna reflection kwenye ujuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja isipokua magari esta na sahihi ya madelu kwenye noti.
 
Maghufuli Chenga sana , sema mambo mengine yabaki tu hvyo hvyo madam ashapita zake, ila jamaa hakuwa na talent ya uongozi alikuwa na kipaji cha usimamizi
 
Hata Magufuri naye alikurupuka. Haiwezekani nchi ambayo wanachi wake hawana umeme wa uhakika ,%kubwa ya watu wake hawana maji safi na salama, miundo mbinu ya elimu ni chakavu, mamilion ya vijana wake hawana ajira ,alafu unachukua matirion ya pesa za walipa kodi na kwenda kujenga ikulu na majengo ya kifahari na kununua ndege ambazo mpaka sasa hazieleweki zinafanya nini zaidi ya kuleta hasara za mabilion ya pesa kila mwaka.
Kiufupi Tz tangu uhuru tuna ombwe kubwa sana la uongozi wenye uwezo wa kuchanganua na kufanya maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya raia.
Usizungumze usichokijua kabla hamjaamua kumlaumu kiongozi yeyote kwenye miundombinu na miradi inayoanzishwa jiulize dira ya maendeleo ya miaka mitano 2016-21 na 2021-26 unaifahamu. Kama hauifahamu jilaumu wew kwanza Kwa kutokujua dira ya maendeleo ambayo ilitumia Kodi Yako kutafuta wataalamu na wadau wengine waliokusanya taarifa na kuziwasilisha na ambazo kwasas zinatekelezwa. NB Kama wananchi mnapaswa kuhoji matumizi sahihi ya mapato ya serikali ktk hyo miradi
 
sasa ndio umeongea nini mkuu, kwa hiyo daraja sio miundo mbinu? unajua umuhimu wa hilo daraja kiuchumi? anyways unapokua na chuki jaribu na kua positive, hii negativity na ujuaji wetu ndio maana tunashindwa hata kuwatoa CCM maana wati wengi ikiwemo wewe wanaishia tu kua keyboard warriors ambao hata kuchukua hatua ndogo hawawezi zaidi ya kuishia kua wachambuzi na kubwabwaja tu huku hiyo serikali unayoilalamikia ikiendelea kukutawala wewe mpaka vitukuu vyako
Ww usiye keyboard warriors umesha chukua hatua gani mpaka sasa?
 
Usizungumze usichokijua kabla hamjaamua kumlaumu kiongozi yeyote kwenye miundombinu na miradi inayoanzishwa jiulize dira ya maendeleo ya miaka mitano 2016-21 na 2021-26 unaifahamu. Kama hauifahamu jilaumu wew kwanza Kwa kutokujua dira ya maendeleo ambayo ilitumia Kodi Yako kutafuta wataalamu na wadau wengine waliokusanya taarifa na kuziwasilisha na ambazo kwasas zinatekelezwa. NB Kama wananchi mnapaswa kuhoji matumizi sahihi ya mapato ya serikali ktk hyo miradi
Kama dira ya maendeleo ya utawala wa Magufuri ilikuwa ni kuchukua matirion ya pesa kujenga mahekaru ya kifahari kwa ajili ya viongozi na familia zao hali ya kuwa watu vijijini wanatembea km 15 kutafuta maji basi alikuwa kiongozi wa hovyo na asiye na akili.
 
Apumzike nini huyo shetani aungue moto wa milele, km si yeye matrilioni ya watanzania yasingeangamia huko kwa wagogo. Dunia ya leo unahangaika kujenga makao makuu ya nchi katikati ya nchi? Moscow iko katikati ya Urusi? Na Washington iko katikati mwa USA? Tusijepata Rais mshamba tena km yule.
This is rude and arrogant, tuangalie maneno ya kutumia kwa marehemu
 
Back
Top Bottom