Hii miradi siyo ya Hayati Magufuli, ni ya nchi. Waziri Makamba kuwa makini sana

Hii miradi siyo ya Hayati Magufuli, ni ya nchi. Waziri Makamba kuwa makini sana

hizi nchi zetu za dunia ya tatu zina shida sana, hao wenye nchi zao (kama kweli wapo km unavyodai) ni heri wangejikita kutengeneza taasisi imara watasaidia sana badala ya kuweka mtu mmoja ainyooshe nchi haitasaidia chochote maana mtu hadumu km tulivyoona ila taasisi zipo milele,
Taasisi mbona zipo tayari, tatizo ni watu walio kwenye hizo taasisi wengi wanawaza upigaji tu, hawafanyi kazi kwa weledi na uzalendo. Utashangaa taasisi muhimu Kama TAKUKURU baadhi ya watumishi pia wanakula rushwa.
Kwa hiyo ishu siyo kutengeneza taasisi tu bali kazi kubwa inayotakiwa kufanyika ni kubadili mindset ya watanzania, tupate watu wenye weledi na wazalendo kweli kweli wataoweza kusimamia hizo taasisi.
 
Taasisi mbona zipo tayari, tatizo ni watu walio kwenye hizo taasisi wengi wanawaza upigaji tu, hawafanyi kazi kwa weledi na uzalendo. Utashangaa taasisi muhimu Kama TAKUKURU baadhi ya watumishi pia wanakula rushwa.
Kwa hiyo ishu siyo kutengeneza taasisi tu bali kazi kubwa inayotakiwa kufanyika ni kubadili mindset ya watanzania, tupate watu wenye weledi na wazalendo kweli kweli wataoweza kusimamia hizo taasisi.
ni kweli na wengi tunaamini katika mtu kuliko system, ila lakin wala rushwa wapo sn ht kwa wenzetu lkn system zao zinawadhibiti? ht netanyahu ana kesi mahakamani ila kwetu huku sisi tunawapa kinga yaani ni sisi wenyew tunajirudisha nyuma
 
Sijui nikusome vipi Fatma Zehra, kama mchambuzi makini au ... (nimekosa maneno ya staha kuyajaza hapo).

Nakumbuka, nimewahi kukusoma humu JF, angalau mara moja, bila shaka jungu lako linao ukoko wa kutosha.

Ninakubaliana na wewe, huyo kaka yako akichezea lile bwawa haponi. Kama hana akili ya kupambanua na kujua kwamba pamoja na ukichaa wa Magufuli, kuna miradi ambayo inampambanua kwa ujasiri wake kuitekeleza.

Kuna mambo mengi umeyaweka mule, natamani kuyagusa moja moja, lakini ngoja niyaweke pembeni kwa sasa.
 
Mbona watu wanamuatacck sana January wa watu? Watanzania tuna guts na wivu sana. Inanifanya kuwaza zaidi ya kuondolewa kwa mtangulizi wake kwenye hiyo nafasi zaidi ya utendaji wake. Ni lini umeme ulikuwa haukatiki. Humu humu zilikuja kejeli za hiyo Train ya SGR kuwa waweke power bank enzi za Kalimlima. Hapa kuna namna kuna kundi limeundwa kwa kukejeli uwaziri wa February. Bora zingewekwa namna za kumfanya aboreshe utendaji wa wizara badala ya kum attack personally.
Kuchafuana kumeanza mapema sana. Hapa si utendaji wa January, hapa suala ni kwa nini January amekuwa Waziri na anapata platform ya kisiasa. Walitaka asiwe na nafasi yoyote ya uwaziri ili afutike kisiasa. Hapa ndipo unaposikia Usiye mpenda kaja. Sasa vita ni vita mura wanataka wammalize.
 
Hadithi yako inatufundisha nini?
Acha kujidanganya na hadithi za kufikirika ,hao watu unaosema " wenye nchi yao"hawapo!

Magufuli hakuna aliyemtengeneza kuwa Rais hizo ni hadithi za wachumia tumbo fulani tu!
Mimi binafsi nilipata kuongea na Magufuli miaka kadhaa kabla ya kugombea Urais na nikajua dreams zake na calculation zake!

Magufuli angekuwa na papara ya Urais kama January na Mwigulu angegombea Urais 2005, kumbuka ndiye alikuwa askari was mwavuli wa Rais Mkapa,lakini alijua mipango yote ya na Lowassa na JK asingetoboa!

Wanaojua siasa wanajua aliyempa Magufuli Urais ni Lowassa! Magufuli alijua hilo hadi anakufa na muda wote alimuheshimu sana Lowassa! Kama hujui basi leo jua hilo!

Magufuli alinufaika na ugomvi wa Kikwete na Lowassa.Lowassa alimzidi Kikwete mipango na Kikwete alimzidi Lowassa madaraka.

Lowassa kupitia Wajumbe aliokuwa nao kama 306 hivi kwenye ile NEC ndo wakampa kura Magufuli kwa hasira na maelekezo ya Lowassa.

Hivyo huo uongo wa eti Magufuli aliandaliwa kuwa Rais acheni labda mdanganyane na akina Paschal Mayalla!
Umenikumbusha mwaka 2005 Magufuli aliulizwa na Waandishi wa Habari kama atagombea Urais akawajibu kwamba mimi naendelea kujenga mabarabara sigombei urais. Wakati anayasema hayo alikuwa site. Kwa kweli Magufuli nadhani hakujengwa na mtu bali alijijenga mwenyewe na mwishowe kabisa ENL akafanya yake. Mengine imebaki historia
 
January kajitakia..huwezi kusema nchi haina lift ya kubeba mziti wa tani 26 wakati watu wanamacranes yamtapakaa yanayiweza kubeba tani hadi 100..So sabb yakusema crane ya kubeba tani 26 haipo nchini hivyo bwawa litachelewa kujaza maji hadi march 2022 hazina maana..ndo maana anashambuliwa
Kila crane na kazi yake mkuu, si kila crane inaweza kufanya kazi katika mazingira tofauti tofauti,
 
Kaka Janu shikamoo.

Naomba leo nikupe ukweli ambao wengi hatuufahamu.

"Wenye nchi yao", baada ya kuona taifa linalegalega, waliamua kumtafuta mwendawazimu mmoja ili alirudishe kwenye reli. Kwa ustadi mkubwa sana walifanikiwa kumchanganya JK kiasi kwamba amekuja kushtuka tayari JPM ni candidate na ana ulinzi mkali sana. Hatimaye, JPM akawa president.

JPM aliwekwa pale kwa ajili ya kusimamia kwa dhati, nguvu, na kwa kutumia kila aina ya njia, utekelezaji wa mipango mingi ya kwenye makabati. Hii ni mifano ya miradi ya nchi ambayo siyo ya JPM na ambayo imefungamana na national interests including national security.

1. Jeshi na taasisi za kiusalama kuwa Dodoma PLUS serikali kuwa Dodoma.
2. SGR
3. Bwawa la Mwl Nyerere
4. Ndege, meli, bandari, na miundombinu mingine mingi mikubwa.
5. Mapambano ya kisayansi ya ufisadi na masuala ya usalama wa taifa.

Hii miradi ilianzishwa na Mwl Nyerere. Mzee Mwinyi hakuifanya sana kwa sababu Nyerere aliacha taifa masikini sana kwa sababu ya sera zake za uchumi na vita ya hovyo na ya kibinafsi ya Uganda. Mzee Mwinyi akashindwa pia kwenda mbali maana alikuwa legelege na ufisadi pia ukaitafuna serikali yake. Ila sera zake ziliitoa nchi katika mateso ya uchumi wa Nyerere kwa kiasi fulani.

Mkapa had a focus. Alikuta nchi haiko stable. He inherited an inflation of 37%. He brought it to 4.1%. Kwa bahati mbaya, mwaka 1995, baada ya kuwa candidate wa CCM, sherehe yake ya kumpongeza kuwa candidate ilihudhuriwa na kijana wa miaka 25 hivi, anayeitwa Rostam. Mimi ninaamini, Rostam ndiye aliyemharibu Mkapa. Mambo aliyotakiwa kufanya Ben, ni pamoja kuhamia Dodoma na alifanya hiyo kazi kiasi flani, miundombinu ya kimkakati, yes he did kiasi chake, lakini pia swala la energy na ulinzi na usalama. Hakufanikiwa sana maana nguvu nyingi zilikwenda kuimarisha uchumi kwanza. Kilichomsaidia ni kuwa na Governer wa Central Bank ambaye alikuwa ana uwezo mkubwa sana kichwani na ambaye alikuwa practicing economist. Hakuwa mwalimu wa uchumi kama hawa waliokariri makaratasi and several western economic models. Hawajui hata nchi inataka nini.

Mkapa alipoondoka, nchi ilikuwa imeonyesha mwelekeo mkubwa sana wa kiuchumi. JK alikuta hazina imeshiba. Alianza kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kiasi chake lakini hakufanikiwa. Kwa mfano, alitamani kujenga SGR but akawa hana pesa. Bwawa la umeme hakuwa na pesa lakini pia alikuwa ni darling wa western world. Hakutaka kuwakwaza wakubwa. Kwa bahati mbaya, utawala wake ulighubikwa pia na ufisadi ulioshiba na ajali nyingi za kujitakia za kisiasa. PM wake wa kwanza angalau alikuwa anafahamu wapi taifa linatakiwa kufika. Hata hivyo, yeye na mwenzake, walijikuta serikali yao inakosa focus mapema sana. Maana walitaka kufanya kila kitu. Taifa lilisogea lakini at a declining pace! Sasa kaka January, baada ya kutokueleweka kwa direction ya taifa, ndipo "Wenye nchi yao", wakaja na mpango wa kumpata mtu ambaye siyo tu kwamba ni mwendawazimu, lakini atatekeleza mambo yote yaliyoko kwenye makabati. Mimi kwa uelewa wangu mdogo, ninaamini, JPM aliandaliwa kwa ustadi mkubwa sana mwishoni au katikati ya mwaka 2009. Na aliyetumika kukamilisha mwanzo wa huo mpango wa yeye kuwa President alikuwa ni Premier Pinda. Mizengo alitekeleza bila kujua. Na baada ya mizengo kutekeleza, akaachwa pembeni. Wakaendelea na plan yao.

JPM alipewa kazi ya kutekeleza hayo niliyoyataja hapo juu. Kwa bahati mbaya au nzuri, JPM alikuwa anapenda sifa sana. Aliyatekeleza sana na kwa nguvu na kwa speed kubwa ambayo was not expected na ikaonekana kama hii miradi ni ya kwake. This's the fact. Hii miradi siyo ya JPM. Ni ya nchi. Usipoitekeleza, au kuikanyaga, unaikanyaga nchi na mifumo yake ambayo siyo rafiki kwakweli.

Ushauri wangu: Pamoja na roho aliyokuwa nayo JPM, na pamoja na ujinga wake na uwendawazimu mwingi aliokuwa nao, usifikiri figisu dhidi ya bwawa la Nyerere na miradi mingine itamuacha mtu yeyote salama. You're my brother. "Wenye nchi yao", ambao siyo watu "wema" are watching and monitoring. Nahisi mama kabadilika baada ya kufahamu ukweli. Kindly thank me later bro. My greetings to Wifi. Shemeji yako ananisubiri. Ngoja akapewe anachotaka.
Sizani kama amekuelewa
 
Leo ndio mnajua kuwa miradi ni ya serikali(umma) na haikua ya mtu fulani.ndege za fulani utafikiri hela imetoka mfukoni kwake.
 
Aisee mimi.mwenyewe nawashangaa. Nchi iligeuka kuwa mto wa damu. Mauaji kila mahali wameingia watu waungwana lakini kelele kila kona. Watz wengi wanaendeshwa na wivu na roho mbaya.
Nyie mlizoea kunyonya watu damu na kuwaacha wamekondeana huku mkila bata sas nyie mkikatwa vichwa mnapiga kelele eti nchi ilimwagwa damu,
Nyie mnaowanyonya hiyo dam mnaona ni sawa sio?
 
Kuna ka taarifa fulani kabaya kanakuja kwa baadhi ya watu,ngoja leo nisikaseme!

Natamani wangelitambua wakati uliofaa!
 
Hadithi yako inatufundisha nini?
Acha kujidanganya na hadithi za kufikirika ,hao watu unaosema " wenye nchi yao"hawapo!

Magufuli hakuna aliyemtengeneza kuwa Rais hizo ni hadithi za wachumia tumbo fulani tu!
Mimi binafsi nilipata kuongea na Magufuli miaka kadhaa kabla ya kugombea Urais na nikajua dreams zake na calculation zake!

Magufuli angekuwa na papara ya Urais kama January na Mwigulu angegombea Urais 2005, kumbuka ndiye alikuwa askari was mwavuli wa Rais Mkapa,lakini alijua mipango yote ya na Lowassa na JK asingetoboa!

Wanaojua siasa wanajua aliyempa Magufuli Urais ni Lowassa! Magufuli alijua hilo hadi anakufa na muda wote alimuheshimu sana Lowassa! Kama hujui basi leo jua hilo!

Magufuli alinufaika na ugomvi wa Kikwete na Lowassa.Lowassa alimzidi Kikwete mipango na Kikwete alimzidi Lowassa madaraka.

Lowassa kupitia Wajumbe aliokuwa nao kama 306 hivi kwenye ile NEC ndo wakampa kura Magufuli kwa hasira na maelekezo ya Lowassa.

Hivyo huo uongo wa eti Magufuli aliandaliwa kuwa Rais acheni labda mdanganyane na akina Paschal Mayalla!


Hii ni kweli kabisa Mkuu, Well Said !! Na ndio maana JPM baada ya kupata Uraisi akaungana na Team Lowasa Wakina Rostam Aziz, Bashe na Cornel Apson
 
Back
Top Bottom