Hii miradi siyo ya Hayati Magufuli, ni ya nchi. Waziri Makamba kuwa makini sana

Huyu MTU hana hoja kabisa!! Acha Waziri wetu afanye Kazi, Siku zote ukweli hukuweka huru! Mwenda Zake hakuwa Malaika, Hivyo alitakiwa kushirikisha taasisi zote kufanya maamuzi kwa niaba ya nchi
Chief Hangaya kavaa viatu vya marehemu, alafu havimtoshi, dah
 
KATIBA mpya suluhisho ya yote, huwez kurupuka kitandani na boksa yako ukatuletea mipango yakp badala ya mipango ya watu milioni 60, never!
 
Hatuitaji watu wajinga kama nyinyi kuwa viongozi katika mataifa yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pythagoras ana hoja.. Na ndiyo hoja yangu na chuki yangu ya msingi kwa JPM. Hakukuwa na haja ya kukatisha maisha ya wapiga kelele, alikuwa na option ya kuendelea kupiga kazi zake vizuri kabisa na kuwapuuza wapiga kelele.. Ikumbukwe, wakati yeye anakula mema ya nchi serikali ya awamu ya 4 kama wengi mnavyosema, wapiga kelele ndiyo waliokuwa wanaibua upigaji wa ESCROW, etc..
 
Aisee mimi.mwenyewe nawashangaa. Nchi iligeuka kuwa mto wa damu. Mauaji kila mahali wameingia watu waungwana lakini kelele kila kona. Watz wengi wanaendeshwa na wivu na roho mbaya.
Mnawekaga chumvi mpaka watu wanakataa kuwaamini, mto wa damu, mauaji kila mahali. Waungwana walifanya nn awamu ya nne ukicompare na awamu moja ya mwamba. Tangible results tu naongelea.
 
Mnawekaga chumvi mpaka watu wanakataa kuwaamini, mto wa damu, mauaji kila mahali. Waungwana walifanya nn awamu ya nne ukicompare na awamu moja ya mwamba. Tangible results tu naongelea.
Tangible results killings, tortures and forced disappearances
 
very good comment.

Na wapiga kelele ndio waliosababisha aonekane yeye ni mchapa kazi mzuri hadi akateuliwa kugombea urais.
 
Fatma... hivi unaifahamu kweli nguvu alizonazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Hayo unayosema yanawezekana kwenye nchi zenye MIFUMO IMARA ambayo Mtendaji HAOGOPI kutimuliwa kazi na rais... kama ilivyokuwa Marekani!

Tanzania hii, ambao hata Wakuu wa Idara Nyeti nao wanajipendekeza kwa watawala halafu utarajie wanaweza kufanya yale yaliyo kinyume na matakwa ya watawala... my friend, UNAJIDANGANYA!!
Basi ambacho hufahamu ni kwamba, JK ndie alipigania JPM awe rais! JK alianzisha miradi mingi sana ambayo mingine ilikuwa imeshaanza kama vile ujenzi wa barabara, madaraja, Mlonganzila, na mingine ilikuwa haijaanza lakini ilikuwa hatua za awali zote zimekamilika kama hiyo SGR, Gesi, na Bandari ya Bagamoyo!

JK alimwamini sana JPM kwenye suala zima la usimamiaji, kwahiyo aliamini ni JPM tu ndie atakayeweza kutekeleza hiyo miradi!! Tatizo wengi walidanganyika na janja janja ya Bernard Membe ambae alifanikiwa kuwaonesha watu kwamba yeye ndo chaguo la JK!

Watu wanashindwa kufahamu ni kwanini hata ile Sheria ya Mafuta na Gesi ilipitishwa haraka haraka wakati JK anatarajia kuondoka madarakani!!

JK alishapanga kumkata Lowassa, na alishafahamu akimkata Lowassa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Lowassa kwenda CHADEMA!!

JK alifahamu Lowassa akishaenda CHADEMA, uchaguzi ungekuwa mgumu sana, na yeyote kati ya Lowassa au JPM (asikudanganye mtu, huyu alishakuwa chaguo la JK) angeweza kuingia Ikulu!!

The Establishment iliogopa zaidi watu waliomzunguka Lowassa, especially Rostam Azizi kuliko ilivyomuogopa Lowassa mwenyewe! Watu walishafahamu shauku ya Rostam Azizi kuingia kwenye gas industry. Sasa kwavile waliona pia kuna uwezekano wa Lowassa wa kuingia madarakani... Lowassa Swahibu mkubwa wa Rostam Azizi; hapo ndipo Sheria ya Mafuta na Gas ikapitishwa fasta ili kuzuia uwezekano wa influence za Rostam unless waamue wenyewe kuifumua sheria!
Hapa upo sahihi lakini vilevile Mkapa aliingia madarakani na "mguu mzuri"!

In 1995, IMF, World Bank and Paris Club walianzisha the so-called Highly Indebted Poor Countries (HIPC) Initiative! Taasisi hizo zilikubaliana zisamehe madeni kwa 38 maskini zaidi duniani, na moja ya nchi hizo ni Tanzania!

Wakaweka conditions za namna gani selected countries zitakuwa approved, na Mkapa alipoingia madarakani, kupitia Reforms mbalimbali, hatimae akafanikiwa kuwashawishi Donors na hivyo kupungiziwa debt burden!

Kwamba RA ndie kamwaribu Mkapa, you might be right lakini sio aliyemfanya Mkapa asihamie Dodoma!

Lau kama Mkapa angesema ahamie Dodoma kwa kasi ya JPM, hata huko kwenye HIPC Initiative tungekuwa DISQUALIFIED instantly kwa sababu IMF na WB wasingekubali wao wasamehe madeni halafu mtumie mabilioni ya pesa eti kujenga majengo ya makao makuu ya nchi!
Kwa mfano, alitamani kujenga SGR but akawa hana pesa.
Hakuwa na pesa kivipi?!

JK wala Mkapa hawakushindwa kujenga SGR bali kwa miradi mikubwa kama hii, mambo yanaenda hatua kwa hatua! Kwa mfano, idea ya kujengwa SGR ilitokea awamu ya Mkapa! Alipoingia JK, wakaanza feasibility study, na hadi JK anatoka, feasibility study ilikuwa imeshakamilika, na ndo maana JPM alianza kujenga moja kwa moja!!

Lakini JK sio tu aliishia kwenye feasibility study bali alishapata hadi Contractor na Financier! Kampuni ya China Railway ikashinda na kupewa tenda ya ujenzi wa SGR ambayo ingekuwa financed na China EXIM Bank!

JPM alipoingia madarakani akakutana na wajuaji!

Wakamwambia KIkwete kahongwa na Wachina, kwahiyo tenda waliyopewa Wachina ni ya Kifisadi! Mbaya zaidi, wakamwambia hata Mikopo ya Wachina inatakiwa kuogopwa kama sumu kwa sababu, Wachina wakikupa pesa baada wanakuja kukunyang'anya miumdombinu waliyogharamia ili kujilipa madeni yao!!

Hapa watu wakaanza kusambaza habari za Wachina walivyoipora Bandari ya Hambantota, kule Sri Lanka kuonesha ni namna tunapaswa kuogopa mikopo ya Wachina!!

Jambo ambalo halikufahamika na "Wazalendo" hawa, habari za Bandari ya Hambantota zilikuwa ni Propaganda za Serikali ya Marekani chini ya Donald Trump ili kuzitisha nchi duniani zisiingie kwenye Belt and Road Initiative iliyokuwa imeasisiwa na China, ambayo ni threat kweli kweli kwa US!

Watu tuliposema hizo habari hazina ukweli wowote... tukaitwa MAFISADI!

Na kama kawaida ya JPM ya kupenda kufanya maamuzi kwa mihemuko, akawapiga chini Wachina akaanza mchakato mpya wa kutafuta Contractor mwingine na ndipo akapatikana Mturuki!!!

Watu tukaonya hapa kwamba mradi lazima utasua sua kwa sababu Mturuki hana pesa ya kutosha kama Mchina, na pia Uturuki as a country, isn't that stable!!

Kilichotokea?! Tukaanza kutanga tanga kutafuta mikopo, na hapo tukadondokea:-
DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzania is in talks with banking giant Credit Suisse for a $300 million loan that would go towards financing infrastructure projects, the country’s finance minister said on Saturday.
Na pia:-
Dar es Salaam. The government and Standard Chartered Bank yesterday signed a $1.46 billion (Sh3.3 trillion) loan agreement for financing the second phase of the standard gauge railway (SGR).
Yaani, leo hii wanataka kutuaminisha Mikopo ya China ni ya Kinyonyaji zaidi kuliko mikopo ya Benki Binafsi za Kimagharibi!

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hilo! But how far did we go katika kuachana na Mchina? The answer is HERE👇👇👇
Sounds like MAFISADI ndio wamewarudisha Wachina kwenye SGR baada ya JPM kufariki, right?! Anyway, heading ya hiyo habari ni hii hapa:-

Kwanini Serikali ya Magu ikaamua kurudi tena kwa Mchina yule yule waliyesema ni Mnyonyaji na huwa anapora infrastructure alizogharamia ili kufidia pesa yake?

Akili za Mbayumbayu, changanya na zako!!

Mkuu Titicomb, nilikuahidi nitakuletea utafiti wa taasisi za Wataalamu wa Marekani wenyewe kuhusu mikopo ya Wachina na suala zima la Bandari ya Hambantota (Sri Lanka)! Sijasahau... nitakupatia!

Huo ni utafiti uliofanywa na Wamarekani wenyewe baada ya kugundua na wao kumbe walikuwa wanadanganywa na Serikali ya Trump... propaganda ambazo pia zilitumika na "Wazalendo" kumtisha JPM kuhusu Wachina!

Lakini wakati naahidi kutoa hiyo ripoti, wasome kidogo Harvard Business School kwenye publication yao ya February 2021...


Abstract ya hiyo publication inasema:-
Lakini wasomi wetu, wakachukua propaganda za Trump na Timu yake wakaitumia kumtisha Magufuli!

Wengine tukajitahidi sana kuelimisha wafuasi wa JPM kuhusu uongo huu wa Marekani lakini kama kawa, ni kwavile tu tumevaa ngozi ngumu ndo maana tuliendelea kuelezea ukweli!

Nikipata wasaa, nitapekua kuitafuta ile ripoti ambayo imeelezea hadi Mikopo ya China vs Mikopo ya International Funding!
Bwawa la umeme hakuwa na pesa lakini pia alikuwa ni darling wa western world. Hakutaka kuwakwaza wakubwa.
Inawezekana ni kweli Hakuwa na Pesa lakini ufahamu kwamba, ingawaje tunadanganywa Bwawa la Nyerere tunajenga kwa pesa zetu lakini uhalisia tunajenga kwa mikopo!!!

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba JPM ambae sera zake zilikuwa UNPREDICTABLE ndo alikuwa more bankable kumlinganisha na JK!

Remember, moja ya criteria zinazotumika na financial institutions kukopesha nchi ni Government Policy! Nchi ikishakuwa na unpredictable president, financial institutions zinakuwa even more cautionary kuikopesha kuliko nchi yenye kiongozi fisadi!!

Nakubaliana na wewe kwamba JK alikuwa ni Western Countries' Darling, na kwahiyo inawezekana hakutaka kuwakwaza kwa sababu wao walikuwa wanaupinga zaidi mradi! Hata hivyo, wakati JK akiendelea na harakati za Bwawa la Nyerere huku Brazil wakiahidi ku-finance mradi, kiwango kikubwa cha gesi kikaendelea kugundulika!!

From Economic Point of View, uwekezaji kwenye sekta ya gesi ni bora maradufu kulinganisha na uwekezaji kwenye Nyerere Dam!

Trillions of Shilings tunazowekeza kwenye Nyerere Dam, end product is just ELECTRICITY! Umeme ambao pia utategemea sana masuala ya sura ya nchi in terms of climate!

Kinyume chake, Gesi sio tu inakupatia umeme wa uhakika bali yenyewe kama yenyewe ni nishati inayoweza kutumika majumbani, viwandani na kwenye magari! On top of that, ukishafanya natural gas processing, unapata by-products za aina mbalimbali zinazoweza kuchochea ukuaji wa sekta zingine za uchumi....

Kwa mfano, soma hapa:-
Kwamba, moja ya by-product inaweza kutumika kujenga viwanda vya kuzalisha mbolea, na ndo maana kuna mpango wa kufungua hicho kiwanda chenye thamani ya zaidi TZS 4 Trillion!

As of now, Tanzania hatuna kiwanda kikubwa cha kufikia hata nusu ya hicho!! Na uzalishaji wa mbolea ni sehemu tu ya namna gani by-products zinaweza kutumika!! Hapo hatujazungumzia up-stream benefits of the gas industry, wala mdi and downstream!!

Faida kama hizo HUWEZI kuzipata kwenye Mradi wa Bwawa la Nyerere ambao utaishia tu kuzalisha umeme ambao pia unaweza kuzalishwa kwa gas!!

I wish ungeona tangazo la TPDC likitangaza tenda ya usambazaji wa gas infrastructure across the country kisha u-digest mwenyewe economic impact ambayo ingepatikana!!!

Hata Muhungo alipozungumzia "uchumi wa kisasa unahitaji gas" alimaanisha hayo... we're not talking about electricity but economic multiplier effect inayoweza kupatikana kwenye gas industry investment as compared to itakayopatikana kwenye Bwawa la Nyerere!
Hivi kuna mahali January amesema anaachana na Mradi wa Bwawa la Nyerere?!

Hivi ni uchumi wa aina gani mnaozungumzia wenzetu wa kuona Bwawa la Nyerere ndo Alpha and Omega to the point mengine yoooooooooooote yasifanyike but Bwawa la Nyerere?!

Kwani January akiendeleza na mipango ya uwekezaji kwenye gesi, inazuia nini kuendelea na Bwawa la Nyerere?!

The problem watu mlilishwa sana propaganda, na zikawakaa barabara!!!
 
Mkuki kwa nguluwe,saiv zamu yake kusemwa mabaya
 
Kama tunaweza kupata Rais ambaye hajaandaliwa kama mnavyodai, basi sisi siyo taifa na tuna shida sana. Na kesho yetu ipo mashakani sana. Mimi naamini bado mmoja kati ya mleta uzi na Jasusi Chachali angalau kwa asilimia 30% yupo sahihi.
 

Suala la kuwa ni serekali ya majizi ya kura, wala sihitaji ww udhibitishe hilo, maana hivyo ndivyo ilivyo regdless unakubali hukubali.

Tuje kwenye hayo maelezo yako ya kutaka kusifia mtu na sio mifumo. Tuanze na reli ya SGR, hiyo reli kipande cha Dar-Moro alisema itakamilika Nov 2019, je mpaka anafariki hicho kipande kilikuwa kimekamilika ambapo ni ni mwaka na zaidi? Unatarajia muujiza gani kwa wale ambao walikuwa sio sehemu ya maamuzi yake. Mgao wa maji, yeye angekuwepo angefanyaje iwapo hakuna mvua, na hakuna water reserve yoyote kukabiliana na hali hii? Alipoingia madarakani 2016 kulikuwa na ukame mkali na mgao wa maji ulikuwepo pia, yeye alifanya miujiza gani?

Unapotosha kuwa malori yalikuwa yamefichwa sasa yamerejea kwa kasi, ni kwamba hiyo SGR ilikuwa inafanya kazi hayo malori yakaaondoka, na sasa hayupo treni imesimama ndio malori yamerudi ama? Unasema hujui kama SGR itaisha, yeye alikopa zaidi ya 15y+, mbona hakumaliza hiyo SGR & SG respectively?

Unasema Tony Blair alikuja hapa nchini kutushauri, kwahiyo alikuja kutushauri tuwe na mgao wa maji na umeme!? Toka lini ushauri ukawa shuruti kwa viongozi wetu? Au unadhani wote ni hamnazo kwa kuchomekea sababu zisizo na kichwa wala miguu?

Arrogance kwenye taasisi za serikali imerudi tena, kwani iliwahi kuondoka au uhuru wa vyombo vya habari tu uliminywa kuripoti habari hizo negative? Kama kuna tofauti, basi ni ndogo sana kwa yeye kutokuwepo. Kwani hatukuona watu wakitekwa na kuuwawa, bila kupata majibu ya mambo hayo? Tulishuhudia chaguzi za kishenzi na kihayawani chini ya tume ya uchaguzi, au hiyo tume ya uchaguzi sio taasisi ya umma? Huenda unachanganya ufanisi na hofu+ maigizo. Bei ya mafuta ya kula na petroli yalipanda maradufu wakati wake, ajira kulikuwa hakuna nk. Au ni ubora gani unaongelea?

Gazeti la financial times limeanza kutusifu tena, kwani likitusifu sasa kuna ubaya gani kama wanaona utawala wa kishenzi umeondoka? Isitoshe gazeti la Financial Times lina madhara gani hapa nchini wakati halina hata wasomaji? Mbona magazeti ya uhuru, habari leo nk yanayochwapwa hapa nchini na kusomwa hadi sasa, yanasifia kwamba mambo ni mazuri toka utawala huu uingie? Je tukuamini ww na sio hayo magazeti ya serikali yanayosema mambo ni mazuri? Kama kweli unasema mambo ni mabaya hadi unashangaa financial times kuisifia nchi yetu, mbona kinachoandikwa na magazeti ya ccm na serikali kusifia hali ni nzuri hakikushangazi?

Wakati anapora na kunajisi chaguzi, huku akiharibu mifumo ya kuhoji mliona anafanya kitu cha maana. Hatimaye amefariki akiwa ameua mifumo ya kuhoji,mambo yanazidi kuharibika kwa kasi na hakuna mwenye uwezo tena wa kuhoji, badala ya kujiuliza tumefikaje hapa, mnaanza kuchomekea sababu za uongo ili kumsafisha mtu muovu! Unashangaa rais muovu kusemwa, kwani alikuwa mtu muadilifu, Nape si alitolewa bastola hadharani akiwa waziri, alichukua hatua gani kama alikuwa kiongozi mzuri? Je ni kiongozi au binadamu gani asiyesemwa? Au kwako yeye alikuwa Mungu? Kama alikuwa hataki kuambiwa ukweli, ulitegemea watu wasimsungumze huko pembeni? Huu ujinga wa kutotaja kuambiwa ukweli naona kauacha kwa wengine, Ndugai naye kaambiwa ukweli anaanza vitisho vya ulevi wa madaraka.

Tunaposema tunataka katiba mpya tunamaanisha, bila kuwa na mifumo bora. Kama kungekuwa na katiba bora yale mazuri yake yangebaki, na uchafu wake asingepata nafasi ya kuufanya. Lakini badala yake, mazuri yake yametoweka, na uchafu aliopandikiza ndio umechukua nafasi. Amka dai katiba mpya itakayolinda mifumo, na sio kuamini mtu anayeweza kufanya mazuri machache na maovu mengi.
 
well
 
WASAKA URAIS WA CCM WANAMUOGOPA JANUARI KULIKO KITU CHOCHOTE. WANAJUA DOGO ANA MBINU MILIONI MOJA ZA KUINGIA IKULU.

WATAMCHAFUA KWA KILA HALI.
Ikulu wala hawezi kabisa hata kuisogelea,baada ya Samia CCM wanamleta mkristo
 
Misukule ya marehemu sidhani kama watakuelewa
 
Financial times wanatuandika vizuri baada ya tony blair kupewa bilioni 100 zile hela za mkopo wa imf. ..eti ili tupate sifa nzuru baada ya sifa mbaya aliyotuwekea jpm?.
Hapo ndio ujue jinsi mabeberu wanavyotuchezea. Hapo utakuta tony blair katoa hela kwenye hiyo migazeti yao😂😂.
Kwanza ni uongo sisi tunajua afrika na ulimwengu wa haki na kimapinduzi magufuli na tanzania tulikua na sifa nzuri. Wala kibiashara hatukuwahi kuwa na shida ila mama kaangukia pua kwenye ulaghai wa mabeberu kama tony blair. Hadi wakuibie ndio wakusifu 😂😂
 
Haya maneno: “wenye nchi yao”, “deep state”, n.k. huwa yanapendwa sana na watu wenye akili na ustaarabu finyu (primitive mindsets). Hata kwenye nchi kama USA ndio waenezaji wakubwa wa conspiracy theories. Wafuasi wa Trump waliogoma hadi leo kukubali matokeo ya uchaguzi wa Rais ya 2020 ni sehemu ya watu aina hiyo.

Magufuli aliandaliwa? That’s hogwash. Yule Aliingia madarakani kwa ajali ya uswahili ya “tukose wote”. Huko CCM hakuna hizo strategic smart brains za kupanga mikakati inayovuka miaka mitano tena katika kuandaa vikundi (timu za ushindi) za kufisidi nchi. Watu wanaodukuliana simu kufuatiliana mipasho ndio wawe na mikakati ya muda mrefu ya kuendeleza nchi?
 
Na huu ndio ukweli wenyewe!!. au nasema uongo ndugu zangu
ni ukweli kabisa.yaani unenyoosha kila kitu.

kubwa kuliko yote ni kuwa wenye nchi yao sio watu wema kweli na ndo waliommaliza JPM mwenyewe baada ya kuona tayari ameshafanya wanachotaka na anataka kuoverdose.

Natamani watuletee mwendawazimu mwingine nchi isogee kwa kasi ya kutisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…