Katika rekodi za wafungaji 54 wa muda wote katika michuano ya Caf Champion League
Chama anashika nafasi ya 10 akifungana kwa idadi ya magoli sawa na wenzake wawili ambao wote kwa ujumla wana magoli 17
View attachment 2922657
Hata hivyo baada ya mechi ya leo kumalizika kwa Chama kufunga bao moja, Chama atavuka nafasi hiyo na kuwa nafasi ya 6 au 7
Kama namba zinaongea na bado hamtaki kukubali basi wacha tuongee sisi.
Katika rekodi za wachezaji kufananishwa na mchezaji wa timu nyingine, Chama amekuwa ndio mchezaji pekee aliyefananishwa na wachezaji wengi.
Na kila mchezaji anayefananishwa lazima hao watu wanaompigia promo waje kumkataa siku za mbeleni.
Walimfananisha na Morrison, Chama akaendelea kuwathibitishia kuwa yeye ni high class .
Wakaja na Aucho, kama kawaida ya Chama akaendelea kufanya yake na mwisho maji na mafuta vilipojitenga ndio ukawa mwisho wa hizo stori.
Waka switch kwenda na Feisal, "ooh Feisal ni mkali kuliko Chama". Muda ulifika na hizo stori zikaisha Chama angeendelea na utawala wake.
Wakaja na Kisinda, "aah unajua Kisinda ni mkali sana kwanza ana mbio afu Chama ni konokono"
Hii hata sitaki niiseme sana maana walimfukiza vibaya huyo Kisinda wao na wao wenyewe ndio waliokuwa wakwanza kumsimanga wakisema mchezaji gani anakimbia hovyo kama kibendera halafu hafanyi chochote.
Sasa wakaja kwa Azizi Ki, huyu ndio walimuona mkombozi wao kupita hao wengine wote waliowahi kutangulia.
Hadi baadhi ya media zikawa zinalazimisha Azizi Ki aonekane ni mpinzani wa Chama kwenye ishu nzima ya ubora.
Lakini kama ilivyo ada, jamaa akatupa taulo na Chama akaendelea na ufalme wake.
Saizi wamekuja na Pacome, huyu Pacome tena bora asijue mnyororo wa wachezaji waliowahi kufananishwa na Chama atakata tamaa mapema.
Yanga wote wanajua kuwa hawana mchezaji ambaye anauwezo wa kumfikia Chama, hata Hersi mwenyewe aliwahi kusema Chama ni mchezaji bora na ana ndoto ya kutaka kumuona siku moja anacheza Yanga.
Ndio maana kila msimu unaona wanamsajili wao ila kucheza anacheza unyamani.
So this isn't the first time and it's not going to be the last