Hii ndio orodha ya mashirika yanayostahili kubinafsishwa bila hata kuuliza ili tusonge mbele

Hii ndio orodha ya mashirika yanayostahili kubinafsishwa bila hata kuuliza ili tusonge mbele

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Wanabodi wa jamii forums,

Yapo mashirika kadhaa ambayo yana stahili kubinafsishwa ili tuweze kuleta ufanisi wa utoaji huduma Tanzania. Haya mashirika ni wazi tungewakabidhi wageni Watanzania tungeishi maisha mazuri sana.

1. Mimi naanza na mashirika ya maji wakuu, maji kila siku yanakatika na huku tunalipia fedha zetu za bill. Tusipolipa kwa wakati wanatufungia huduma ya maji lakini wao wakikata maji hatuwezi wafanya chochote.
2.
3.
4.

Mimi nimeanza na hilo moja, kama unalijua lingine liweke hapa toa na sababu kwanini hilo shirika libinafsishwe. Wapi linapopwaya.

Usisahau kutaja shirika:
Ambalo tukibnafsisha hata haliumi
 
Mkuu tatizo kubwa la kukwama kwetu sio mashirika bali ni sisi watu na mifumo yetu...

Sisi wabongo ni wavivu, walafi kama mchwa na wabinafsi...

Tunasoma vizuri shule, tunapata utaalamu kwenye fani mbalimbali lakini tukishakabidhiwa vitengo ufanisi zero...
Ni kweli hili ni tatizo kubwa na linasababishwa na kutokua na elimu ya kutosha. Mkuu niamini kusoma hadi level fulani haimaanishi ndio una elimu.
 
Back
Top Bottom