Hii ndio orodha ya mashirika yanayostahili kubinafsishwa bila hata kuuliza ili tusonge mbele

Hii ndio orodha ya mashirika yanayostahili kubinafsishwa bila hata kuuliza ili tusonge mbele

Hawa NIDA wanatatizo kiukweli. Jana nimeenda NBC bank kufungua akaunti, ndani ya dakika 15 nilijaza taarifa zangu zikaingizwa ndani ya mfumo nikapewa ATM card. NIDA wangejifunza NBC
Unataka mtu apewe uraia ndani ya dk 15,nadhani ungesuggest waweke mfumo ambao sio sumbufu,lakini kutoa NIDA bila verification ni hatari
 
Unataka mtu apewe uraia ndani ya dk 15,nadhani ungesuggest waweke mfumo ambao sio sumbufu,lakini kutoa NIDA bila verification ni hatari
Lakini mkuu verification inaweza kufanyika kwa muda mfupi. Au wewe unasemaje
 
Mimi ni Mtanzania na sasa nina miaka minne sijapewa kitambulisho changu tangu nikiombe. Kama ili nipiwe hicho kitambulisho na wasio Watanzania wanaweza pewa pia basi nipewe tu, I don't care.
Binafsi kimebakiza miaka 3 ya renew
 
Mkuu tatizo kubwa la kukwama kwetu sio mashirika bali ni sisi watu na mifumo yetu...

Sisi wabongo ni wavivu, walafi kama mchwa na wabinafsi...

Tunasoma vizuri shule, tunapata utaalamu kwenye fani mbalimbali lakini tukishakabidhiwa vitengo ufanisi zero...
Mkuu umemaliza kila kitu,hii thd kila mtu atalaumu shirika fulani.

😀 😀
 
Na hivi vyuo vyote vyenye hadhi ya kata vinavyosajili wanafunzi bila kujali uwezo wa chuo kuhandle idadi ya wanafunzi pia soko la ajira Nchin, wao wanasajili tu maelfu ya wanafunzi ambao baadae ndio hawa wanaosumbuka na mabahasha kuomba ajira hivi vyuo vibinafsishwe.

Shirik la TTCL hawa hakuna kuuliza

Vituo vyote vya stendi za mabasi hivi ikiwezekana viwekewe sheria kali huku mapato yanajificha.

Shirika linalodeal na Mipango miji wapewe watu wenye akili timamu.
 
Kwanini uwe na mawazo ya kuwapa wageni, wakati tuna soko letu la hisa DSE? Serikali iuze hisa zake wadau tuzinunue, tuteuwe board tunayoiamini ili itusaidie kupata management yenye ufanisi.
Wanabodi wa jamii forums,

Yapo mashirika kadhaa ambayo yana stahili kubinafsishwa ili tuweze kuleta ufanisi wa utoaji huduma Tanzania. Haya mashirika ni wazi tungewakabidhi wageni Watanzania tungeishi maisha mazuri sana.

1. Mimi naanza na mashirika ya maji wakuu, maji kila siku yanakatika na huku tunalipia fedha zetu za bill. Tusipolipa kwa wakati wanatufungia huduma ya maji lakini wao wakikata maji hatuwezi wafanya chochote.
2.
3.
4.

Mimi nimeanza na hilo moja, kama unalijua lingine liweke hapa toa na sababu kwanini hilo shirika libinafsishwe. Wapi linapopwaya.

Usisahau kutaja shirika:
Ambalo tukibnafsisha hata haliumi
 
Back
Top Bottom