Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Ndugu zangu wa Singida wanazembea somewhere. Wangetumia fursa ya uadimu wa mafuta kulima alizeti, wangetoka. Wizara ya kilimo ikapige kambi Singida ku boost kilimo cha alizeti.
Alizeti inalimwa lakini hakuna support kutoka serikalini
 
Umeandika mlimba hiyo mlimba ya morogoro? Mbona kilombero umeiyacha, ina maana makusanyo ya tanesco na kilombero suger hawaingizi kipato cha kutosha?
sina uhakika km Tanesco wanapozalisha umeme wa Kidatu wanalipa kwa Halmashauri au Sugar wanapouza sukari Nchi nzima naona malipo yanaenda Serikali kuu
 

Mmeambiwa watumishi muache kuvujisha nyaraka za Serikali, hiii kauri huwa siielewi kabisa mie
 
Mmeambiwa watumishi muache kuvujisha nyaraka za Serikali, hiii kauri huwa siielewi kabisa mie
Hii sio nyaraka ya kuwa siri ipo kwenye tovuti ya Tamisemi,nimeambatanisha mada hii na pdf kutoka kwenye hotuba ya Waziri wa Tamisemi
 
Pdf hii ya wizara ya TamisemiView attachment HOTUBA YA WN OR TAMISEMI 2021.22.pdf
 
Kweli kabisa sasa hivi mufindi Kuna viwanda vingi vya mchina kwa vijana wanaotafuta maisha bila kujali ugumu wa kazi njoo mufindi hakika hautojuta
Shida ya huko baridi Kali balaa na vumbi LA kutosha
 
Ni kweli ukizigawa moja moja Dom inazipita vizuri tuu,nakumbuka ule mwaka juzi Dom waliuza Sana viwanja wakapiga bil.73 ndio iliongoza kwa Halmashauri moja moja watu wakapagawa.

Dom unakuja Kazi Sana na viwanda vinajengwa Sana
Kuna watu walishasema wanauza viwanja wakaambiwa kwani nyinyi hamna viwanja. Kuna sababu Dodoma wanauza na kuhamia serikali na wafanyakazi wote hiyo ni boost kubwa sababu nchi hii bado katika kukopesha wafanyakazi wa serikali wanapata urahisi na biashara inawafuata.
 
Moshi inatia huruma na zile safari za kuhesabisa hamna kitu ,kimji cha kizamani kimechoka kama taulo la guest
Japo 'umewaua' kwa kuwa ni ngome ya watani zako kisiasa ila kiukweli Moshi ni moja ya miji isiyo na fursa kabisa.

Hakuna ardhi, ukabila unaathiri sana uwekezaji wa watu kutoka maeneo mengine kwa kuwa biashara zinafanyika 'kindugu'. Moshi nadhani jamii kutoka maeneo mengine kwa zaidi ya 90% ni watumishi.

Ndiyo maana watu wa Moshi/Kilimanjaro wamesambaa maeneo mengine ya nchi kusaka fursa kwa kuwa kwao ni 'mtihani'.

Moshi unaweza itafuta buku hata wiki nzima, kitu labda cha maana kwa mtu wa kuja ni lile soko la mitumba (King George Memorial) na hapo uwe unaenda kuuza nje ya mkoa wa Kilimanjaro.

Pia watu wa Kilimanjaro wana namna fulani ya 'ubahili' kwenye purchasing ya bidhaa na huduma. Kitu pekee wananunua bila kuwaza ni bidhaa za pombe na nyama ambazo nazo wanaangalia ni bar ya nani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Then unaskia sera za majimbo unabaki kujiuliza hayo majimbo yangefanya maendeleo kwa mapato gani?
Taarifa km hizi ni muhimu sana watu kua nazo kabla hawajaropoka kuhadaa uma.
Tena Majimbo ndio yangesaidia Sana mikoa dizaini ya Singida ku maximize their full potential kuliko saizi ambapo wanajua hata tukikusanya mia watapata ruzuku ya serikali kuu sasa hii sio fair
 
Kelele nyingi moshi hakuna jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…