jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Jambo la Mwisho saaana huku mashamba Bado ni mengi mno, kama Maeneo ya uvinza -nguruka unaweza uziwa ekari moja kwa 50,000/= nikifanikiwa kwenda kibondo huko mashambani sikuona tractor Bali nguvu kazi ni watu nilivyouliza wenyeji wakanambia wanaolima wengi ni wakimbizi kutoka Burundi wanalimishwa hekari moja Kwa SHILINGI 30,000/_40,000/= warundi ni watu wenye roho mbaya sana na makatili story niliyoipata huko ni kwamba hawapendi dhuruma ukimlimisha Shamba alafu umcheleweshee malipo yake basi jiandae kukutana na kitu kizito sana Huwa hawapendi masikhara kwenye haki Yao, story iliyopo huku ni kwamba Zamani kulikua Kuna watekaji wengi walitokea Burundi, serikali ilijitahidi sana kupambana nao hao maharamia kwa Sasa hizo story za utekaji ni kama hazipo...
Kutoka kigoma kwenda dar, ni safari ya masaa 24 non stop Lakini ukitoka daresalam kuja kigoma lazima mtalala pale kaliua -tabora kwa sababu ya usalama, pale mbele kidogo ya kaliua Kuna mbuga na misitu Pamoja na vichaka kwahiyo watu wenye Nia ovu ni rahisi kutimiza adhima yao.
Wafanyabiashara wengi wakubwa huku lazima awe anapeleka mzigo congo na kwenda congo njia nyepesi lazima uvuke maji so kama sio katili au mtu wa fitina basi omba Mungu tu maana mnavuka kwenye mitumbwi na usalama wa huko sio guarantee sana.
Kigoma fursa zipo Lakini usiwe na jicho tu la Kuona fursa lazima Uwe na jicho la kujikinga na mazindiko ya kutosha, huko mtu kuongea swala la ndagu ni kugusa tu wala sio jambo la ajabu.
Anyway karibuni sana kigoma
Waha sifa moja tu ya msingi ni wapambanaji sana.