Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Nanga mkono hoja✍️✍️✍️
 
hili ni tatzo kubwa
 
Vp kuhusu wale waliokua scattered huko maporini walivokusanywa pamoja kwenye vijiji vp haikua sawa kurahisisha utoaji wa huduma kwa urahisi na kusave gharama za kuunda miundombinu kufikia wananchi wengi?
Huduma gani zilirahisishwa? Unajua hata hospitali na zahanati nyingi zimekuja kuanza kujengwa kwenye maeneo mengi kuanzia awamu ya 4 na ya 5?
 
2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

hili ni tatzo kubwa
Hili jambo linatuumiza sana kwa kweli
 
Sijawahi ona mama mjamzito kafa kwa Corona ulitafuta kichaka tu cha kuficha ukilaza wako tu .
Ulitaka mama yako mjamzito afe kwa corona ndiyo uamini kuwa corona inauwa wajawazito?
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Natofautiana na wewe kwenye hilo la mwisho...

Pia ongeza namba 8, uamuzi wa kuingia vitani dhidi ya Iddi Amin
 
Wewe ndo mjinga.
Huelewi gharama za kupendezesha sehemu zenye ukame? Umeishia darasa la ngapi?

Nikupe mfano. Sehemu ambayo mvua zinanyesha miezi 2 kwa mwaka na sehemu ambayo mvua zinanyesha miezi 6-7 kwa mwaka wapi ni nafuu kuweka bustani ya majani?
Kwa hiyo gharama zipi zinatumika kuondoa ukame au wanaumwagilia mkoa
Kuhusu Elimu nina elimu ya kawaida ila nina akili kushinda ukoo wenu wote
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Kuuza bandari kwa wajomba
 
Namba tano kwa kweli inasikitisha.

Nakumbuka kipindi cha corona kuna mama majamzito alifia hospitalini kwetu kwa sababu ya corona.

Sasa mimi ni kaandika kuwa sababu ya kifo ni korona. Weeeh. Wanasiasa waliniwashia moto eti mkuu wa nchi ameshasema hamna corona. Sasa wewe unachafua mkoa wetu na sisi tutakuchafua. Issue ile iliniudhi sana maana hata ndugu walijua kuwa mgonjwa wao amekufa kwa korona sasa mwanasiasa anakataa. Wanasiasa ni shida.
Acha uongo kwa hiyo ulitaka lock down au
Colona ipo wap now????
 
Naona wajinga leo mmeamka na Nyerere baada ya lile la udini kufeli, na hapa mtafeli pia, najua mmetumwa kuzima moto wa bandari zetu unaoendelea kuwawakia nyie wasaliti na vibaraka wa shetani.

Iko hivi; unapomlaumu Nyerere leo, miaka zaidi ya 20 baada ya kifo chake, na miaka zaidi ya 30, baada ya Nyerere kutoka madarakani, unaonesha ulivyo na akili mfu, na hilo sio kosa la Nyerere kama ulivyoandika, ni kosa la wazazi wako kukupeleka shule za hovyo.

Kwasababu ukitazama vizuri hiyo miaka, utakuta kuna miaka karibia 40 tangu Nyerere aondoke madarakani, sasa kitu gani kinawashinda kubadili hali hiyo hata baada ya miaka yote hiyo kupita?

Hebu tuambie, ni kipi kati ya hayo yote uliyoorodhesha hapo juu kinachohitaji kubadilishwa baada ya miaka zaidi ya 50 ili tumlaumu Nyerere? na kama sio unakurupuka tu, ni nini kingine?

Tena wewe Lord denning ndie chawa mzembe unayepigia debe ule mkataba wa hovyo wa bandari zetu watanganyika, wenye terms za kinyonyaji kwetu, halafu kwa ujinga wako unamlaumu Nyerere! kwamba Nyerere ndie alikutuma uwe mjinga kupigia debe ule mkataba wa hovyo?

Hauna akili.
Wewe unataka wote tufikiri kama wewe ndo tutakuwa na akili.
Wewe baki na hilo la bandari huku hakukufai...
 
Kwa hiyo gharama zipi zinatumika kuondoa ukame au wanaumwagilia mkoa
Kuhusu Elimu nina elimu ya kawaida ila nina akili kushinda ukoo wenu wote
Hiyo elimu unaipata hata you tube tu. Maeneo yenye ukame hayapendezi. Yanahitaji ufanye vitu vingi ili kuyapendezesha kama kujenga artificial livers. Dams, lakes etc.

Saudi wanajenga mji mpya jangwani , Misri pia kama walivyofanya Dubai. Kwenye hii miji vinajengwa vitu vingi sana artificial ili kuipendezesha na ionekane mizuri. Hapo ndo gharama zinapokuja.
 
Ulitaka mama yako mjamzito afe kwa corona ndiyo uamini kuwa corona inauwa wajawazito?
Hakuna hiyo data na hawakuwa kwenye risk yoyote nenda kawaombe msamaha ndugu za huyo mama .
 
muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu.

Muungano wa serikali moja wa nini ?

Halafu tuendeleze stress za nani kamfunika mwingine, ya nini yote hayo ?

Zanzibar wana nini cha kuifaidisha Tanganyika ? Muungano uvunjwe, nukta.
 
Kwa utafiti wangu mdogo nchi nyingi zenye muungano zinaulinda sana muungano. Nimeona hata Spain na UK na German pia.

Ila kuweka serikali 2 hapo mimi naona ndo hakukuwa na hoja ya msingi zaidi ya watu kutafutiana ulaji tu. Kwa mujibu wa nyaraka za historia zinasema hata Karume alitakaga Serikali 1. Na hii ingepunguza sana gharama za mzigo wa kuhudumia Serikali na viongozi wake
 
Kwa mfano nchi gani zinaulinda sana Muungano ?

Nchi gani zinalinda Muungano wa kijinga kama huu ?
 
Back
Top Bottom