Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

NA SERA YA VILLAGIZATION YA KUWAKUSANYA WANAVIJIJI KUISHI PAMOJA KWENYE VIJIJI VYA UJAMAA NI JAMBO LILIKUWA NA LIMESABABISHA ATHARI MBAYA ZA KIMAENDELEO IKIWEMO UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA. KUJUA HILI WEWE CHUNGUZA MIKOA ALIYOPITIWA NA SERA HII NA AMBAYO WALIMGOMEA MZEE JULIUS MIKOA YA MBEYA (TUKUYU), KILIMANJARO, ARUSHA (ARUMERU), KAGERA. MAENEO HAYO AT LEAST BADO YAKO SAAFI. KWA MFANO UKITEMBELEA TUKUYU KITU KITAKACHO KUSHANGAZA NI NAMNA UOTO WA ASILI ULIVYOTUNZWA HADI LEO. MITO YA ASILI BADO INATIRIRIKA MAJI VIZURI KABISA, CHANIKIWITI NI MUDA WOOTE!
Hii nchi kusema kweli ingekuwa uwezo wangu tungeanza upya kila kitu
 
La kwanza kabisa ni Nyerere kudai uhuru 1961, alitukosea sana yule mzee na mitamaa yake ya uongozi. La pili ni kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar, hapo ndo tulikosea mazima.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Naona wajinga leo mmeamka na Nyerere baada ya lile la udini kufeli, na hapa mtafeli pia, najua mmetumwa kuzima moto wa bandari zetu unaoendelea kuwawakia nyie wasaliti na vibaraka wa shetani.

Iko hivi; unapomlaumu Nyerere leo, miaka zaidi ya 20 baada ya kifo chake, na miaka zaidi ya 30, baada ya Nyerere kutoka madarakani, unaonesha ulivyo na akili mfu, na hilo sio kosa la Nyerere kama ulivyoandika, ni kosa la wazazi wako kukupeleka shule za hovyo.

Kwasababu ukitazama vizuri hiyo miaka, utakuta kuna miaka karibia 40 tangu Nyerere aondoke madarakani, sasa kitu gani kinawashinda kubadili hali hiyo hata baada ya miaka yote hiyo kupita?

Hebu tuambie, ni kipi kati ya hayo yote uliyoorodhesha hapo juu kinachohitaji kubadilishwa baada ya miaka zaidi ya 50 ili tumlaumu Nyerere? na kama sio unakurupuka tu, ni nini kingine?

Tena wewe Lord denning ndie chawa mzembe unayepigia debe ule mkataba wa hovyo wa bandari zetu watanganyika, wenye terms za kinyonyaji kwetu, halafu kwa ujinga wako unamlaumu Nyerere! kwamba Nyerere ndie alikutuma uwe mjinga kupigia debe ule mkataba wa hovyo?

Hauna akili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee mimi nakukubalia asilimia 150 uzi wako umeenda sana shule sijui kama watu wanakuelewa haswa uamuzi wa kuhamia Dodoma mji ulio sehemukame tena kwa uharaka waajabu sana na pia Muungano wa hovyo kabisa! These are facts na siyo opinion ni ngumu mtu kukujibu kwa ufasaha hizi hoja zako!
Mbona Dubai ilikuwa jangwa na sasa hv pakoje?
Hv sisi watanzania tuna laana au yaani kuna mijitu mijinga mijinga sana
 
Niliwahi kujisemea nisije pewa uwaziri wa ardhi. Maana ntavunja nyumba za watu hadi wataniona mwehu
Mbona wa Maliasili wanakunja tu na kuhamisha watu kuwa wamevamia hifadhi wakati umeme ,maji ,vituo vya kupigia Kura na shule serikali imepeleka Leo wanawavunjia mf.Morogoro ..hii ya hovyohovyo sana..
 
Mbona Dubai ilikuwa jangwa na sasa hv pakoje?
Hv sisi watanzania tuna laana au yaani kuna mijitu mijinga mijinga sana
Somaga kitu uelewe ndo utoe comment yako.
Hoja kuhusu Dodoma imejikita kwenye gharama za kupapendezesha. Hata Dubai wanatumia gharama kubwa sana kupafanya kuwa pazuri jambo ambalo kwa Tanzania halikuwa na ulazima kwa sababu tuna mikoa ina hali nzuri ya hewa na kijani kinachopendeza
 
hapo kwenye kuruhusu kiswahili kuwa lugha ya taifa na lugha ya kufundishia shule ya msingi upo sahihi 100%.

madhara yake ni makubwa sana, tumebaki kutumia hoja dhaifu kujifariji. unakuta mwanasiasa anazungumza eti hata wachina, waitaliano na wajerumani hawazungumzi kingereza na wapo mbelea kauchumi, seriously!?
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
The worst of all ni jiwe kupewa urais.
 
Somaga kitu uelewe ndo utoe comment yako.
Hoja kuhusu Dodoma imejikita kwenye gharama za kupapendezesha. Hata Dubai wanatumia gharama kubwa sana kupafanya kuwa pazuri jambo ambalo kwa Tanzania halikuwa na ulazima kwa sababu tuna mikoa ina hali nzuri ya hewa na kijani kinachopendeza
Kwa hiyo hiyo seehemu nyingine isingetumika gharama? Unajua maana ya Dodoma kufanywa makao makuu ? Ndio maana nasema Tanzania kuja kuendelea ni ngumu coz kuna majitu majinga mengi sana yasio na uelewa kama wewe
 
Muogope kama ukoma mtu yeyote anaye chukka ukomonosti na ujamaa. Ni mbaguzi mbinafsi, sana. Kwa taarifa yako. USA, China, Russia. Wanaanda Dunia mpya kijamaa na kikomonisti.kwa jiba Democratic socialism
 
Muhimu hili la muungano lipo hoja zako zote naziunga mkono.

Pia na vita ya uganga nayo imetuweka sehemu mbaya kwa kiasi chake.
 
Kwa hiyo hiyo seehemu nyingine isingetumika gharama? Unajua maana ya Dodoma kufanywa makao makuu ? Ndio maana nasema Tanzania kuja kuendelea ni ngumu coz kuna majitu majinga mengi sana yasio na uelewa kama wewe
Maana gani ya msingi ya kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu?

Ndo hiyo mnadai mkoa wa katikati mwa Tanzania?

Katika karne hii ya sayansi na teknolojia hiyo hoja ina msingi gani?
 
Back
Top Bottom