Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Kumchagua mgombea mwenza kwa kigezo cha jinsia bila kuzingatia uwezo.
Kuuza bandari zote za Tanganyika kwa DP World kwa muda usiojulikana na faida isiyojulikana.
 
Ikiwa hili lilikuwa kosa, dawa yake ni kuuvunja. Uvunjeni basi kuondoa maamuzi ya ovyo, ila hamfanyi kwani mna mawazo ya kikoloni kutaka kuitawala Zanzibar.
Huwa naona aibu kwamba na wazanzibar eti ni sehemu ya nchi yetu, yaani watu legelege, watu walalamishi, wavivu na wazembe, wasiojua nini hawataki na nini wanataka, wasio na msimamo wao kupenda mahaba na kula tu basi
 
Hapo umekosea.
Hakuna Bandari iliyouzwa
Samahani kama nimekosea haya kugawa bandari zote za Tanganyika kwa waarabu kwa muda usiojulijana na faida isiyojulikana. Samahani nilisema kuuza wakati sijaona malipo ukweli ni kwamba zimegawiwa bure.
 
Huwa naona aibu kwamba na wazanzibar eti ni sehemu ya nchi yetu, yaani watu legelege, watu walalamishi, wavivu na wazembe, wasiojua nini hawataki na nini wanataka, wasio na msimamo wao kupenda mahaba na kula tu basi
Huo ni ubaguzi ndugu. Sio jambo zuri
 
Weka na mifano
Mifano hana. Hajui hata Arusha waliazimia nini, Hajui maana halisi ya Ujamaa.

Kiufupi anataka kulazimisha Jamii ya Mtanzania iwe kama Jamii zingine hususani za Ulaya kitu ambacho hakiwezekani, hakitaweza kufanyika.

Mambo yaliyo orodheshwa si Vigezo au Vichocheo vya maendeleo Afrika au Bara lingine lolote lile hapa Duniani.

Anachokisema LD ni kile kinachoitwa kitaalamu kuwa ni "Shaming" ni Ukatili unafanywa na makundi fulani kwa lengo la kuwakatisha Tamaa wenzao. Hana utaaluma wa Siasa, Jamii, au Uchumi. Ni mpiga ramli tu. Ni mdhalilishishaji(soma na kufuatilia Uzi zake)

Udhalilishishaji huu unaofanywa na LD ni wa makusudi ambao lengo lake kuu ni kukufanya mlengwa kuacha, tena kwa aibu, mambo yote yaliyo katika Utamaduni wako na kufuata ya wengine.

Shaming inahusisha kudhalilisha, kufedhehesha, kutukana, kuaibisha, na hata kuwadhalilisha wengine

Itoshe, hakuna lelote aliloliorodhesha ambalo limetajwa katika Vyanzo vyovyote vile Duniani kuwa ndivyo vikwazo vya moja kwa moja kwa maendeleo ya Kisiasa, Kijamii au Kiuchumi Tanzania.
 
Hiyo elimu unaipata hata you tube tu. Maeneo yenye ukame hayapendezi. Yanahitaji ufanye vitu vingi ili kuyapendezesha kama kujenga artificial livers. Dams, lakes etc.

Saudi wanajenga mji mpya jangwani , Misri pia kama walivyofanya Dubai. Kwenye hii miji vinajengwa vitu vingi sana artificial ili kuipendezesha na ionekane mizuri. Hapo ndo gharama zinapokuja.
Kwa hiyo unataka Dodoma itelekezwe
Una akili ndogo sana
 
Huo ni ubaguzi ndugu. Sio jambo zuri
Kama ubaguzi ni kutaja sifa za mtu au kikundi cha watu basi mimi ni mbaguzi. Nikimuita mtu mfupi kwamba ni mfupi au mrefu nikimuita mrefu au mnene nikimuita mnene nakuwa nimembagua au nimeeleza sifa yake? Hao niliowataja nimetaja sifa zao za kupenda vya dezo mda wote wanawaza starehe na raha tu, wavivu na sifa nyingine nyingi zisizo nzuri.
 
Hakuna terms zinazotumaliza pale. Ni maneno ya wanasiasa tu maana hiki ni kipindi cha siasa. Mwaka kesho uchaguzi serikali za mitaa then mwaka 2025 ni uchaguzi mkuu hivyo kelele unazozisikia ni maandalizi ya kisiasa tu
hapo ndipo unapokosea. Yaani huuoni kuwa ule mkataba ni m'bovu? waafrika ni nani aliwaloga? akili kuhamia matumboni ni fasta!

JESUS SAVES
 
Mtangulizi wake kumchagua huyu kuwa makamu wake...😎
Usiseme uongo. Hajachaguliwa na mwendazake, CCM tuna utaratibu wetu ni ambao pia ulimchaguwa mwendazake kwa kazi maalum kwa wakati maalum, akasaliti kama yuleee mwendazake wa awali.
 
Mifano hana. Hajui hata Arusha waliazimia nini, Hajui maana halisi ya Ujamaa.

Kiufupi anataka kulazimisha Jamii ya Mtanzania iwe kama Jamii zingine hususani za Ulaya kitu ambacho hakiwezekani, hakitaweza kufanyika.

Mambo yaliyo orodheshwa si Vigezo au Vichocheo vya maendeleo Afrika au Bara lingine lolote lile hapa Duniani.

Anachokisema LD ni kile kinachoitwa kitaalamu kuwa ni "Shaming" ni Ukatili unafanywa na makundi fulani kwa lengo la kuwakatisha Tamaa wenzao. Hana utaaluma wa Siasa, Jamii, au Uchumi. Ni mpiga ramli tu. Ni mdhalilishishaji(soma na kufuatilia Uzi zake)

Udhalilishishaji huu unaofanywa na LD ni wa makusudi ambao lengo lake kuu ni kukufanya mlengwa kuacha, tena kwa aibu, mambo yote yaliyo katika Utamaduni wako na kufuata ya wengine.

Shaming inahusisha kudhalilisha, kufedhehesha, kutukana, kuaibisha, na hata kuwadhalilisha wengine

Itoshe, hakuna lelote aliloliorodhesha ambalo limetajwa katika Vyanzo vyovyote vile Duniani kuwa ndivyo vikwazo vya moja kwa moja kwa maendeleo ya Kisiasa, Kijamii au Kiuchumi Tanzania.
Unakosea sana. Huu uzi hauna nia yeyote na kufanya shaming. Hakuna sehemu kuna matusi na wala hakuna sehemu mtu amedhalilishwa.

Nimetumia haki yangu kutoa maoni yangu kutokana na utafiti nilioufanya na nikajiridhisha.

Labda wewe uniambie hapa Je tulikuwa sahihi kuruhusu watu kujenga kwenye maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa? Usahihi huo unatoka wapi?

Unaona sawa kwa sehemu kubwa ya nchi yetu ilivyojengwa hovyo kutokana na maamuzi haya?

Huoni ubaya wa hili?
 
Nimesikitika kuusahau Mwenge
Mwenge hauwezi kuusahaulika aisee. Ni sehemu ya hoja namba 1.

Hadi leo tunatumia fedha nyingi kufanya jambo ambalo kama tungekuwa wazima kichwani tungezielekeza kufanya mambo ya msingi zaidi
 
hapo ndipo unapokosea. Yaani huuoni kuwa ule mkataba ni m'bovu? waafrika ni nani aliwaloga? akili kuhamia matumboni ni fasta!

JESUS SAVES
Msimamo wangu kuhusu suala la Bandari nilishauweka humu.

Nimeusoma mkataba na kusema kweli sijaona issue yeyote serious kama mapungufu ya kimkataba. Yanayotokea ni siasa tu ambalo ni jambo la kawaida as hiki ndo kipindi cha siasa( kuelekea 2024/2025)
 
Kwa hiyo unataka Dodoma itelekezwe
Una akili ndogo sana
Wapi nimesema hayo? Usiniwekee maneno mdomoni.

Tulifanya makosa na tunamwaga hela katika kuiweka sawa. Ni makosa tulifanya ila hakuna namna. Hoja yangu hapa tujiandae kuona hela zinamwagwa sana pale kwa sababu ili papendeze pale lazima tumwage fedha nyingi sana za walipa kodi.

Hofu yangu wakija kuamka na kupiga hizo hesabu tunaweza kutafutana maana watakuja kuhoji what was the logic behind wakati kuna maeneo mengi yangekuwa mji mkuu wa Tanzania gharama hizo zisingetumika.
 
8. Wakristo na waislamu kuongoza nchi Kwa zamu ya Miaka Kumi kumi. Tunahitaji Ráisi mmoja tu mchapa kazi hata kwa Miaka 30
Muhimu kwao ni hizo nafasi za uongozi wale nao na si kutumikia au kujenga nchi, sasa ukiwaambia mtu mmoja ashikilie nafasi kwa miaka 30 hawawezi kukuelewa.
 
Back
Top Bottom