Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Km unaamini maisha ni fumbo basi saidia wenye shida ili na wewe usije kusakamwa maisha yatapokuja kubadilika (sikuombei)

Wengi wetu tumeishi maisha ya manyanyaso ya hapa na pale, na sasa tunawasaidia walewale waliokuwa wanatunyanyasa na kutucheka na maisha yanaenda vizuri tu

Km unaamini katika Mungu basi amini kuwa ukisaidia unapata thawabu, na ujue pia tunapopewa hivi tulivyonavyo sio vyote ni vyetu, vyengine vinapitia tu kwetu ili kusaidia wengine. Ishi maisha ya kutoa ili uwe na furaha
 
Bado unautoto mwingi
 
Mom.is just a mom, msamehe tu na yeye ni binadamu

Help you mummy, sema mwambie alivokua akikutendea but usiache kumsaidia
 
Achana kima zote Ila mama ni mama
 
Mara nyingi kama sio zote ndugu waliowengi hawana shukrani, unaweza kumsaidia kwa kidogo ulichonacho lakini baadaye utakapofikwa na magumu/changamoto katika kipato chako uliokuwa ukiwasaidia ndo watakuwa wa kwanza kukusema kuwa ulikuwa ukiharibu fedha kwa mambo yasiyo maana ndiyo maana hukuambulia hata kujenga nyumba.

Endelea kumsaidia mama namueleweshe kuwa fedha ya boom wala si chochote kwako wewe uliyekuwa ukiitegemea kwa 100%. Nina imani amejazwa.

Hao ndugu wengine wasaidie kwa akili, ukiona yafaa kufanya hivyo.
 
Wengi tulipitia huko ingawa picha tofauti. Unakuwa na ndugu wenye kazi nzuri miaka hiyo ya 80 lakini unaambiwa labda kuku na chips lakini pesa sahau.
Hao hao ukifanikiwa ndo wanakuja mbio mbio hata wale ulikuwa hujawahi kuwa na simu ganja hivyo usingwaslliana nao, utasikia simu inalia ya mezani na msururu wa matatizo. Tuliweza kumeza mate na kusema basi ngoja tufanye ya Mungu. Baba na mama walionisomesha, hakuna hata mmoja alishaniomba hata senti moja. INAUMA SAANA.
 
Hakika safari ya maisha ni fumbo.
 
Mimi alikuwa amechanichota, Ila pale aliposema mama yake alikuwa anamsimanga kwa kutumia boom vibaya, nikajua haya ni majani ambayo hayakuwa blended na kukauka vizuri na kusababisa harufu isio ya kawaida kwenye kinywaji pendwa cha asubuhi.
Kanitukana bana kha🤣
 
Unadhani kuna MTU atakufa kwamba hujamsaidia? Hiyo ni roho mbaya tuu,wewe Fanya maisha yako. Ila IPO siku hali itawakutanisha. Nilidhani ulijifunza kwa dadako kumbe ni ukoo uliobeba laana? Pole.
 
Fanya yote ila lipa wema Kwa mama, hata kubeba tumboni na kuzaa ni kukuonesha upendo, angeweza kutoa mimba.

Yote aliyokuwa anakwambia mama ni kutokana na maisha aliyokuwa anapitia, na huenda huyo dada Yako nae hakuwa anamsaidia mama hivyo mama alitegemea wewe ukimaliza chuo itakuwa afadhali yake. Hivyo wewe kushindwa kupata ajira Kwa muda Fulani ikamuongezea msongo wa mawazo na kuishia kujikuta anakwambia aliyokuwa anakwambia.


Tuna wazazi wanakero zaidi ya mama Yako na tunawapenda hivyo hivyo Kwa kujikumbusha mema Yao machache waliyotufanyia.

Kama unauwezo mfurahishe mama Yako, hakujawahi kuwa na mama wawili duniani mama ni mmoja ila baba unaweza kuwa nao hata sita.

Hivyo hasira zako kamwe zisikufanye usahau wema wa mama Yako.

Wengine wafanyie utakavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…