Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Nimeongelea power tiller wewe unaingelea trekta. Ama kweli, majungu yapo hadi mitandaoni
 
Tatizo waswahili wanajua kusanehewa ni kuanza kupewa hela.
Mimi kuna ndugu zangu wala sina shida nao,tukikutana story tunapiga..ila mazoea sitaki na siwezi wapa hela yangu abadani.
😅😅😅😅
 
Ushauri wangu mimi hao ndugu zako waache kama walivyo ila Mama yako Mzazi msaidie kwa kila hali hata kama alikulaumu kivipi? Wewe tekeleza wajibu wako kumuangalia Mama yako mzazi kwani umetoka nae mbali sana. Ukikosa kumsaidia mama yako mzazi ujuwe utaharibikia kila kitu chako ulicho kipanga huo ndio ushauri wangu ukiweza ufuate usipo weza uachilie mbali upite zake.
 
Mmmh ndugu Sina hamu Mimi. Nilifirisiwa kwa siku 1. Sikuyaamini macho yangu. Nimesamehe Ila ukaribu noo.
 
Ahsante mkuu
 
Oya skia hapo ushatoboa maisha njoo sasa tule bata maneno ya mama yatimie utapanye pesa mpka zikukome
 
Kuna kitu hakipo Sawa kwenye hii Hadithi yako maan Hadithi ya kuanzia utotoni haiwezi kuisha Kwa mistari michache ulioiandika,
Otherwise kuna kitu unatuficha.
Pili, Kwa nin unaamini kwamba Dada yako alikuwa na uwezo wa kukusomesha?
Imani uliyokuwa nayo kwamba Dada yako ana uwezo ndo Imani hyo hyo ambayo Mama yako aliamini ulikuwa na Pesa isipokuwa uliitumia kuhonga.
Kama hutaki kuwasaidia ndg Kwa kigezo cha kwamba umetoboa basi wewe kausha,
Maana Kwa maelezo yako hujalazimishwa kuwasaidia Ila unajihisi Tu kwamba Kwa kuwa sasa hv wanakupigia cm basi wanatak msaada,
Hao watu wameishi Maisha Yao Bila hata msaada wako ambao unahisi Una umhimu,
Ikifikia hatua ukaona kwamba Mama yako hafai Basi subili Tu kufundishwa na Ulimwengu,
Yaani mtu (Mama) ambae unakiri kabisa kwamba alihangaika na wew tangu ulipoachwa ukiwa mchanga,
Leo hii Kwa sababu Tu za kununua heka 50 cjui na PT ndo unaona hakufai?
Are you serious?
Mama yako japo simjui naamini ataendelea kuishi hata Bila huo msaada wako,
 
Pole kwa magumu uliyoyapitia,
Ila katika Dunia hii,"no body owes you anything"
Sio lazima watu wakupe msaada,wakikupa,Sawa,ukinyimwa,songa mbele.
Kitu nilichojifunza,bahati mbaya kwa kuchelewa ni kwamba kwenye haya maisha,mtu wa pekee atakaekuja kukuokoa,ni wewe mwenyewe tu,
Ndugu ni binadamu tu,huwa tunakeleka wanaposhindwa kutusaidia kwa sababu tunaweka matumaini makubwa sana kwao kwa vile tumezaliwa tumbo moja,ni baba,ni mama,tunasahau hizo zote ni lebel tu,they are just Human beings.
 
Mama ni mama siku zote, mtunze mama achana na hao wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…