Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hapo MAREKANI atajinyonga kwa wivu!!
 
😀 😀 😀 😀 dah kwa gharama hizo ni haiwezekani labda dunia ianze upya. Shida inakuja pale ambapo viongozi wetu ni kama wanatutambia wakiwa madarakani na v8 zao wakiwa wanapita vuu vuu speed kubwa wanaenda kuzindua mradi tuliojengewa na USAID
 
Nime fall in love na sayansi jamani🔥🔥, wanawezaje wezaje hawa?
Wanawekeza, serikali inaruhusu free tech kuzalisha huku yenyewe ikiwasupport na kuhakikisja hakuna mtu anabaki nyuma, pia kukiwa na tech mpya yenye faida kwa taifa serikali inatoa funds.

Angalia kile kigari cha Masoud Kipanya!.
 
Sana tu, JPM sifa ndio zilikuwa nyingi na umimi uliopitiliza. Hizo ndege tu zimetuacha na madeni, bado hasara kila mwaka na hazina ufanisi wowote. Alikuwa na uthubutu ila hakuwa strategic wala hakupenda kushauriwa, ilikuwa ni one man show.
alikua bwege tu. nchi yetu haijawahi pata kiongozi. hata nyerere alikua hovyo.
 
Kwa kasi hiyo, hivyo vyuma si vitawaka moto. Msuguano utakaokuwapo hapo si wa kitoto.
Maglev (magnetic levitation) trains huwa hazigusi chuma huwa zinaelea juu kwa juu zinatumia principle ya eddy current levitation kukamilisha hilo.

kwa mfano mrahisi ukichukua pande mbili za sumaku zinazofanana kisha ukajaribu kuzikutanisha zitakuwa zinakataana(principle of magnetism) sasa wakishakamilisha kule kukataana wanachofanya ni kutengeneza njia ya kupata msukumo (motion ) kupitia hizo hizo sumaku.

Japo eddy current levitation huwa zinazalisha pia joto (eddy current losses) ila nadhani huwa kuna mfumo wa kupooza kupitia maji , japan ,indonesia , malaysia na nchi nyenginezo baadhi za asia walikuwa nazo hizi treni muda tu. ila nadhani kwa spidi china ndiyo atachukua tuzo miaka ijayo.
 
Kweli wenzetu wameadvance, 1000kph sio mchezo hata kidogo. Hapa na Moro ni 0.2hrs yaani 12mins..duh!
Wakati sisi tuko kwa Mwaposa kutafuta upako, na tahasusi kuongezeka za dini kuliko science.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…