Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii kitu niliisomaga zamani kidogo , BBC wakiandika kua miaka ijayo huenda tukawa na treni inayopita kwenye ombwe kwa kasi..

China hana ajizi, katekeleza.

Sisi tuendelee kusema elimu haina umuhimu, bora vijana waache vyuo wawe machinga.
Je, Kuna mtu yeyote mwenye elimu ambaye amewahi kugundua kitu cha maana hapa Tanzania? Ishu ni akili sio elimu.
 
China imekamilisha jaribio la usafiri wa treni aina ya maglev yenye kasi ya juu (UHS), kuashiria hatua nyingine muhimu kwa aina hiyo ya usafiri inayoweza kusafiri kwa kasi ya hadi maili 621 kwa saa sawa na kilometer 1,000 kwa saa.

View attachment 3064287

Jaribio hilo lilifanyika katika mkoa wa Shanxi unaopatikana kaskazini mwa China.

Hili lilikuwa jaribio la kwanza na kubwa lililokamilika kwa mfumo wa usafirishaji kwa kutumia umeme wa bomba pana lililo wazi (utupu) UHS.

Mojawapo ya mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa jaribio hilo ni kwamba ilithibitisha kuwa mazingira ya uwazi uliopo kwenye bomba hilo kwa umbali mrefu yanaweza kufanya spidi kuwa kubwa zaidi na kudumisha kwa kiwango kikubwa.

China ilianza kujenga mfumo wa usafiri wa UHS maglev katika Kaunti ya Yanggao mwaka wa 2022, mfumo huo unalenga kuunganisha teknolojia ya anga na mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kuendesha treni kwa kasi ya maili 621 kwa saa.
Maendeleo makubwa ya China yalipatikana baada ya kukamilisha mifumo ya usafiri ya kupunguza muda wa kuwa safarini kwa mizigo na abiria.

Hii ikiwemo kutoboa milima ili kupitisha barabara ndani yake na kuondoa safari za mzunguko mrefu za kukwepa milima. Pia, kutumia madaraja ya kuning'inia.

Kwa sasa China inategengeneza ndege zake yenyewe, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafirishaji wa anga. Huku reli ndefu zaidi duniani ikiwa nchi China.

Hili la reli ziendazo kazi limeipa China mafanikio makubwa sana kwenye sekta ya usafirishaji abiria na mizigo yao na kuunganisha miji iliyoemdelea na inayoendelea.

Katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa China, njia za usafirishaji huweza kusafirisha abiria zaidi bilioni tatu, hii ikiwa ni karibia nusu ya watu walipo duniani.

Lakini, kubwa zaidi, miundo mbinu hii imejengwa na Wachina kwa mikono yao huku wakitumia zana zilizobuniwa na wao wenyewe. Ikiwa ni mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 30 tu.

Na hii treni ya kusafiri kwa treni ya ndani ya bomba inazidi kuwaweka Wachina kuwa namba moja duniani kwa usafirishaji wa idadi kubwa ya watu ndani ya kipindi kifupi.

Ova
 
Kwa ufupi iko hivi kanuni ya usumaku ni kwamba pande zinazofanana zinakinzana sasa hapa kinachofanyika ni kwamba mataruma na reli vinasumakishwa kwa umeme ambapo mataruma na reli vyote vinapewa hali ya ufanano kiusumaku kwahiyo vitakinzana na kwamaana hiyo treni ya aina hii mataruma yake ikitembea hayagusani na reli hivyo treni inakuwa kama inaelea kwenye mataruma na pale inaposimama inashuka na kugusa mataruma.
Hii bado sijaelewa mkuu, fafanua zaidi.
 
Marekani ile nchi deep state Ndio wanaiharibu , wanaotafuna pesa za federal government kwenye mambo ya kipuuzi kama vita , racket za kusomba pesa za umma na kunufaisha wazalishaji wa silaha .
Mmarekani hajashindwa kutengeneza hii kitu ni vile Tu failure ya sera zao humo .
Maana hata miundombinu yao ni poor na wanazidiwa na nchi nyingi zilizoendelea ,si train Tu , hata barabara nk .
Biden na ile infrastructure bill sijui walifikia wapi , walikuwa wamepropose serikali yao ifanye heavy spending kwenye miundombinu
Marekani wana mradi wa ujenzi wa high speed railways California, kutoka L.A mpaka San Francisco tangu mwaka 2015, guess what?

Mpaka leo mradi umekua slow sana na gharama zinaongezeka kila mwaka

Zimejengwa km 190 tu mpaka sasa!

Wakati China tangu 2015 imeshajenga km 27,000 za high speed railways
 
Back
Top Bottom