Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Vyuma havisuguani mkuu,wanatumia tech ya MAGnetic LEVitation (MAGLEV) uliza zaidi kuhusu hiyo tech, ni ya ajabu kidogo
Sahihi mkuu,hii technology,wheels na rails hazina contact.Yaani magurudumu yanakuwa suspended kwa gepu fulani.Hii inatumia nguvu ya usumaku kama vile unapotaka kugusanisha Sumaku N kwa N au S kwa S,hamna vyuma kusuguana.
 
Unajua si jambo dogo mzee. Speed ya KM 1000 ni kasi ya kimaendeleo. Hiyo mwanza unaenda na kurudi kama vile unaenda mbezi tu hapo.

Hizi ndio vitu tunataka kuona katika uchumi wetu. Aisee nina uhakika mzee wetu mpendwa Magufuli angelikuwapo huku tungefikia tena ndani ya miaka michache ya baadae. View attachment 3064296View attachment 3064295
Hivi hawawezi kuja kuwekeza TZ miradi kama hii!! 💪🏽💪🏽😜
 
You might be right! Ila kumbuka JPM alikuwa na ndoto ya kuona TZ inapiga hatua. Hili kubali au kataa, hiyo ni husda wako kwake. Usisahau wakati ule mlikuwa mnampinga kuwa yeye anaangalia maendeleo ya vitu si watu. Hata TL alikuwa anaipigia kelele. Wenye akili tulikuwa tunawaeleza kuwa maendeleo ya nchi ni vitu (infrastructure) kwanza
Itakuwa hizi treni za mwendokasi, uhakika wa umeme tumeletewa na baba yake labda ndo maana kajiropokea, is overrated kwa sauti ya puani
 
China imekamilisha jaribio la usafiri wa treni aina ya maglev yenye kasi ya juu (UHS), kuashiria hatua nyingine muhimu kwa aina hiyo ya usafiri inayoweza kusafiri kwa kasi ya hadi maili 621 kwa saa sawa na kilometer 1,000 kwa saa.

View attachment 3064287

Jaribio hilo lilifanyika katika mkoa wa Shanxi unaopatikana kaskazini mwa China.

Hili lilikuwa jaribio la kwanza na kubwa lililokamilika kwa mfumo wa usafirishaji kwa kutumia umeme wa bomba pana lililo wazi (utupu) UHS.

Mojawapo ya mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa jaribio hilo ni kwamba ilithibitisha kuwa mazingira ya uwazi uliopo kwenye bomba hilo kwa umbali mrefu yanaweza kufanya spidi kuwa kubwa zaidi na kudumisha kwa kiwango kikubwa.

China ilianza kujenga mfumo wa usafiri wa UHS maglev katika Kaunti ya Yanggao mwaka wa 2022, mfumo huo unalenga kuunganisha teknolojia ya anga na mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kuendesha treni kwa kasi ya maili 621 kwa saa.
Na huko haluna kiboko ya wachawi,mwamposa,suguye wala nabii shillah.
 
Itakuwa hizi treni za mwendokasi, uhakika wa umeme tumeletewa na baba yake labda ndo maana kajiropokea, is overrated kwa sauti ya puani
Tunawajua watu humu ukitamka jina tu! Wanaumia, hata siku moja hawawezi kubali ukweli. Tanzania hadi sasa tulikuwa na marais wawili wazalendo, Nyerere na Magufuli. Wengine wanapita tu
 
Back
Top Bottom