Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Raisi wao aliwahi kusema biashara pekee tunayoiweza waafrika ni kujenga makanisa ya mabilioni na kuwa very superstitious. ila tumeitelekeza sayansi na teknolojia, anatushangaa sana.
Wasomi wetu wamesaliti taaluma zao wamekimbikia siasa.
Huko kwenye siasa badala kutengeneza sera nzuri tufikie malengo wanaishia kulimbikiza pesa za wizi.
Wakishakwapua wanakimbilia kujenga nyumba za ibada.
Hiyo ndiyo Afrika
 
Unajua si jambo dogo mzee. Speed ya KM 1000 ni kasi ya kimaendeleo. Hiyo mwanza unaenda na kurudi kama vile unaenda mbezi tu hapo.

Hizi ndio vitu tunataka kuona katika uchumi wetu. Aisee nina uhakika mzee wetu mpendwa Magufuli angelikuwapo huku tungefikia tena ndani ya miaka michache ya baadae. View attachment 3064296View attachment 3064295
Hilo treni hata Marekani hawana! Dereva hahitaji kuona mbele, treni linaendeshwa kwa mahesabu matupu.
 
China imekamilisha jaribio la usafiri wa treni aina ya maglev yenye kasi ya juu (UHS), kuashiria hatua nyingine muhimu kwa aina hiyo ya usafiri inayoweza kusafiri kwa kasi ya hadi maili 621 kwa saa sawa na kilometer 1,000 kwa saa.

View attachment 3064287

Jaribio hilo lilifanyika katika mkoa wa Shanxi unaopatikana kaskazini mwa China.

Hili lilikuwa jaribio la kwanza na kubwa lililokamilika kwa mfumo wa usafirishaji kwa kutumia umeme wa bomba pana lililo wazi (utupu) UHS.

Mojawapo ya mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa jaribio hilo ni kwamba ilithibitisha kuwa mazingira ya uwazi uliopo kwenye bomba hilo kwa umbali mrefu yanaweza kufanya spidi kuwa kubwa zaidi na kudumisha kwa kiwango kikubwa.

China ilianza kujenga mfumo wa usafiri wa UHS maglev katika Kaunti ya Yanggao mwaka wa 2022, mfumo huo unalenga kuunganisha teknolojia ya anga na mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kuendesha treni kwa kasi ya maili 621 kwa saa.
Hii ni zaidi ya bullet train nini?!
 
Kwa kasi hiyo, hivyo vyuma si vitawaka moto. Msuguano utakaokuwapo hapo si wa kitoto.
Hakuna friction inaelea magnetism like poles repel kwahio ukizima na kuwasha zile magnets zinavuta kwa mbele
1723123784735.png
 
Back
Top Bottom