Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Hii ndiyo treni yenye spidi ya kasi sawa na ndege, nilidhani uongo kumbe kweli

Sisi pia tumepiga hatua kiasi chake pamoja na changamoto zetu za ufisadi na Umasikini tulionao

Miaka ya 1961 wengi wa Watanzania ilikuwa tunatembea Kwa miguu

Baadaye 1975 ndiyo baadhi wakaanza kuendesha Baiskeli Tena Kwa uchache mno

Miaka ya 1985 wachache wakaanza kuendesha pikipiki hasa wafanyakazi

Miaka ya 1995 wenye uwezo wakaanza kununua na kuendesha magari binafsi

Mwaka 2024 Kwa mara ya kwanza tukaanza kupanda treni la Mwendokasi 🙌

Hopefully wale watakaojaaliwa kufika Mwaka 2100 huenda wakaanza kupanda hizo Treni zenye hiyo spidi ya 1,000km/h kutoka Tanzania 💪
 
JPM hakuwa na mipango endelevu, haswa kwenye econimic development, ingefika kipindi angekata pumzi tu. Mikopo aliyokuwa anakopa bila ya kuendeleza vyanzo vipya vya makusanyo, asingetoboa mbali kabisa.
Hiyo upo sahihi na ndiyo maana alianza kukumbatia akina Rostam Azizi baada ya kuelewa ukweli kuwa mambo si rahisi kama alivyofikiria. Na hilo kosa lilicost maisha yake.
 
Hata ndege za ATC nyingi haziendi kwa cruising speed ifikayo 1000kph!

Kwa treni hii saa moja na dakika chache uko Mwanza!
Hapa bongo tungepata hata ya uhakika ya km 350 kwa saa, alafu tupate reli za Dar-MWZ. Dar-MBY, na Tabora-Kigoma. Nchi ingefunguka balaa. Kwa siku tuwe na ruti tatu tu asubuhi mapema, mchana na jioni na ziwe za uhakika. Hiyo ya Km 1000 ni ndoto ya mchana, wala tusiifikirie leo wala kesho
 
Inahitaji wasomi kwelikweli, Yani hayo madude yanahitaji tuwe na wasomi wabobevu kweli...China hawakutaka wafanyiwe kama ilivyo huku kwetu, binafsi kitu Bora zaidi ni wewe/sisi kuwa na elimu ya kufanya vitu viwe kuliko kujengewa na wageni Kila siku, hivyo basi wakati tukiwa kwenye hii transition basi serikali iwekeze kwenye kuhamisha ujuzi wa wenzetu kuuleta Kwa watu wetu na kuweka mazingira mazuri ya ubunifu, lakini ni kitu ambacho hakipo na hamna juhudi za vitendo kufanikisha Hilo, hivyo basi ni kwamba sisi kufika huko ni mpaka hiyo teknolojia Yao iwe outdated.
 
Sisi pia tumepiga hatua kiasi chake pamoja na changamoto zetu za ufisadi na Umasikini tulionao

Miaka ya 1961 wengi wa Watanzania ilikuwa tunatembea Kwa miguu

Baadaye 1975 ndiyo baadhi wakaanza kuendesha Baiskeli Tena Kwa uchache mno

Miaka ya 1985 wachache wakaanza kuendesha pikipiki hasa wafanyakazi

Miaka ya 1995 wenye uwezo wakaanza kununua na kuendesha magari binafsi

Mwaka 2024 Kwa mara ya kwanza tukaanza kupanda treni la Mwendokasi 🙌

Hopefully wale watakaojaaliwa kufika Mwaka 2100 huenda wakaanza kupanda hizo Treni zenye hiyo spidi ya 1,000km/h kutoka Tanzania 💪
Good analysis that's written by the GT of JF.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Raisi wao aliwahi kusema biashara pekee tunayoiweza waafrika ni kujenga makanisa ya mabilioni na kuwa very superstitious. ila tumeitelekeza sayansi na teknolojia, anatushangaa sana.
Tuache ndugu, Jpili ifike haraka tukapate miujiza, tukanunue na maji ya upako, chumvi na mafuta.

Maendeleo yana faida gani kama hatujamshimda shetaini na mbawa zake ili asiruke kutufikia.
 
Back
Top Bottom