Hii ndo tathimini kuelekea January 22 katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Lissu anakubalika na wana harakati wa nje ya nchi ambao hata hawajawekeza TZ, ndani ya CDM hana nguvu ya kisiasa na ndiyo maana wapambe wake wanakialia hapa kika siku sababu wanaijua nguvu ya Mbowe ndani ya CDM.

Ushindi kwake ni ndoto za mchana - cha msingi aanze kuongea na Zitto mapemaa kabla halijachwea - otherwise mwendo wa siasa kwake ndani ya CDM ushagota.

BOX linakwemda kumfanyizia tena asubuhii.
 
Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na wewe. Kitu cha kuongezea ni kuwa CCM na vyombo vya dola vitahakikisha Mbowe anashinda kwa gharama yoyote. Hii ni kwa sababu wameona ni fursa nzuri ya kuiua CHADEMA kuliko wakati mwingine wowote. Nyongeza: uchaguzi ujao Mbowe ataachiwa ashinde baadhi ya majimbo ili bunge liwe na wabunge ambao ni friendly kwa serikali ya Samia. Mbowe yeye hatakuwa na hasara kwa sababu nia yake kubwa ni ruzuku itakayoongezeka.
 
Iki chama nilikiona cha ivyo 2020 mbowe alipo sema lissu akishinda mimi nitakua waziri mkuu 😅😅
 
Ni bora aanzishe chama chake ambacho kitakuwa very pure kama alivyo yeye very pure na ndio maana anawananga wenzake kuwa ni impure au sio?
Hawezi kupachs usajili usimpoteze huko.....msajili wa vyama ana maelekezo miaka yooote....ndio maana Maalim Deif ( RiP) hakuweza kupita njia kuanzidha chama bali ilibidi aende ACT bila kupenda
 
Unafikiri kwa nini Maalim hakuanzisha chama chake akaenda ACT ? Msajili yuko pale kibaraka wa chama kileee.....tusijitoe akili....
 
Hawezi kupachs usajili usimpoteze huko.....msajili wa vyama ana maelekezo miaka yooote....ndio maana Maalim Deif ( RiP) hakuweza kupita njia kuanzidha chama bali ilibidi aende ACT bila kupenda
Hujui unachoongea Dogo.
 
... Kwahiyo Mbowe atapoteza kundi kubwa sana la watu mtaani.
Hilo kundi atakalopoteza mtaani, alikuwa nalo kabla ya uchaguzi huu? Mbona hadi tunaingia katika uchaguzi huu Mbowe amekuwa ni Mwenyekiti? Kwa nini hilo kundi lisipotee katika kipindi chote alichokuwa mwenyekiti, ila lije lipotee atakapokuwa mwenyekiti?
 
Verry poor thread and analysis in general,

Mbowe anaungwa mkono na baadhi ya wajumbe wa kamati Kuu.

Wapiga kura wajumbe wa mkutano mkuu wapo mikoani kwenye kanda mbalimbali.

Wanajua ukweli, kwamba huyu bwana Mbowe hafanyi siasa kwa lengo CHADEMA ichukue dola, huyu anafanya biashara,na Samia na CCM, watu wanamjua, this time hatoboi hata CCM watoe rushwa, wajumbe wanakula hela na kura kwa Lissu.

Uchaguzi wa CHADEMA, ni Lissu, utafanana na ule wa MWABUKUSI bkuwa Rais wa TLS, wa Lissu kuwa Rais TLS, kila mtu alisema hawashindi!! Wakashinda.

Mbowe hauziki, kama umekuja kupima upepo mpe majibu, MBOWE MUST GO kwa afya ya CHADEMA na mustakabali wa nchi.
 
Sema wewe chawa wa mbowe ndiyo humpendi sisi wengine tunampenda.
Halafu mbona humshauri mbowe kuhama? Kwani yeye ndiye alianzisha Chadema? Au ndo tuanze kuamini yale maneno ya saccos ya Mbowe
 
Kuanzisha chama sio njia ya uhakika wa yeye kupambana na Ccm.

Kinachohitajika ni kuwa na platform ya kuongelea mambo yake .

Itakuwa haileti maana Sana endapo kila anayekosa nafasi Chadema akimbilie kuanzisha Chama.

Naungana na wewe Bwana Haya...

Au badala ya kuanzisha chama kipya kabisa, basi wavi assess hivi vyama vingine vidogo na kukiboost!!

Ila changamoto ninayoiona ni kwamba, hata vyama hivi vidogo bado ni mali za watu binafsi!!

Kimsingi, bado hatuna vyama pinzani ambavyo kimsingi ni mali ya umma!!
 
Kuna uwezekano wa ACT kuchukua nafasi ya chadema.
Hata mimi hilo nimelifikiria muda mrefu.
Hadi sasa ACT wana nguvu Zanzibar.
Japo Lisu sijui kama anaweza kukaa ACT wakaelewana na Zito lakini wafuasi wake wanaweza kwenda ACT siyo kwamba wanamkubali Zito bali kumkomoa Mbowe! Kuna uwezekano Lisu kuchukua maamuzi ya Dk Slaa ya kujitenga na siasa za vyama.
 
Umemaliza, chadema ikumbuke ikimaliza uchaguzi Bado itahitaji wananchi kiujumla kuisapoti.Huo ndo ukweli, wakivuruga kwenye uchaguzi wao wasitafute mchawi
 
ukweli ni kwamba TAL hawezi kushinda, Ccm kupitia tiss imepandikiza mamluki wengi Sana kule Chadema. mamluki hao watampigia kura mbowe. MboWe amekuwa akipewa pesa nyingi za ufadhili kutoka Ccm.
 
Lissu atashinda ,mapema sana , Mbowe mwenyewe atampigia lissu kura, jichanganye , hamjui dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…