Unaweza kuona ni propaganda lakini kuna wengi hawaoni hivyo. Ni kweli siyo tuhuma mpya lakini bado zina uzito. Chama cha CUF kabla ya kujiunga na UKAWA kilivutia sana waislam. Na siyo propaganda ila ndiyo ukweli wenyewe. ATC wazalendo nayo kiongozi wao Zitto ni mtu mwenye udini sana japo anafanya kwa kisiri. Mashabiki wa ATC wanaweza wakasema ni propaganda lakini kuna watu wengi wanaona ukweli fulani kwenye tuhuma.
Ok, hebu tuzame zaidi. Hivi, Udini ni kuwa na watu wengi wa dini fulani, au ni mwelekeo wa fikra? Kwa Zanzibar, idadi kubwa ya wakazi ni waislamu, hivyo haishangazi kwamba chama chenye ushawishi mkubwa Zanzibar, viongozi wengi ni waislamu. Lakini haimaanishi kwamba kwa hoja hiyo tu, chama hicho kina Udini. Katika viongozi wa CCM Zanzibar sidhani kama kuna mkristo, sina hakika.
Lakini misingi aliyoweka baba wa taifa ni kutoruhusu ubaguzi wa aina yoyote, ili hata pale viongozi wa imani fulani wanakuwa wengi, hatuna haja ya kuhofu.
Kwa hiyo, tukemee hasa pale unapofanyika ubaguzi wa kidini, badala ya kuishia kutazama idadi. Tukemee matendo ya ubaguzi, badala ya orodha ya majina. Ninavyojua tuna sera ya 50 - 50 katika mambo ya idadi ya wanawake katika uongozi. Hatuna sera ya 50 - 50 katika dini za viongozi.
Lakini nasema hizi ni propaganda tu kwa sababu nakumbuka kuna wakati mh. Lukuvi aliwahi kwenda kanisani na kutoa kauli kali za ubaguzi wa kisiasa, CCM hawakulaani Bali walitetea. Kardinali Pengo anajulikana kushambulia serikali zinazoongozwa na marais waislamu, na kuwa kimya kwa marais wakatoliki, hata pale wanapofanya makosa makubwa. Sasa huo ndio Udini wa kukemewa.
Serikali ya CCM sasa hivi inasimamia ubaguzi mbaya sana wa kiitikadi na kikabila. Rais Magufuli anatamka waziwazi mchana kweupe, "akina Mushi siyo wa kuwaamini", na pia "makosa ni yenu kumchagua mtu wa upinzani" wakati anasisitiza "maendeleo hayana vyama". Huo ndio ubaguzi wa kukemewa, siyo mtu anaona orodha tu analia Udini. Badala ya kufanya utafiti hao viongozi wamefanya matendo gani ya kuwatia katika hatia ya Udini? Maana wamechaguliwa au hata kuteuliwa, hawajajichagua wao.