Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Tumuongezee pua uongozi wa CHADEMA wakristo 90%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeahindwa ku comment mkuu

mwongo atofautiani Na mchawi
 
CCM hawatawali Kwa wingi wa kura ila Kwa nguvu za dola pamoja na madhaifu ya upinzani, CCM ni MUMIANI wananchi wanalitambua hilo
 
Huyo Babu yako alikueleza maelezo ambayo yanapingana yenyewe!

Yaani mtu anakuzidi kila kitu halafu eti tena akuogope kwa sababu una uwezo anautamani! Ni sawa na kusema mtu tajiri lakini anautamani umasikini wako!

You must be out of your mind!
Najua unajibalaguza tu ila unajua kwanini hasa nasema mnatuogopa... Achilia mbali hayo mafungu ya watu wenye itikadi fulani mnaoziita dini! Uislam ni zaidi ya dini kwa kua ni MFUMO KAMILI WA MAISHA YA BINADAMU HAPA DUNIANI NA HUKO AKHERA.

Uislam ukiongoza sehemu yeyote lazima utakutana na misingi thabiti ambayo ni;

UTU, WAJIBU, HAKI, UPENDO, SHERIA NA HUKUMU ambavyo dunia ya leo mmekua mnavitafuta kwa kuunga unga na bahati nzuri hivyo vyote Muumba wa Mbingu na arshi yu radhi navyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba, ubaguzi wa rangi upo, ubaguzi wa mataifa upo, udini upo, ukabila upo, uchama upo, ukanda upo, kujuana kupo, undugu upo kila mahali.

Unataka ndio hivyo , hutaki ndio hivyo. Ukikutana nao pambana nao, ukishindwa epukana nao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cheo cha makamu Zanzibar kilifutwa? Ni najua yupo makamu bara na makamu zanzibar!
 

Ukihukumu Siasa au Uambo lolote lile kwa Imani ya Wazanzibari basi utakosea.

Sifa ya Wazanzibari ni Kuishi kwa Imani (Uislamu) kwa Jambo lolote lile.

Mimi Nimeishi Zanzibar kwa Miaka 32.
Nilichoshuhudia ni kuwa CCM inatangazwa Misikitini na Wafuasi wake, Na CUF/ACT inatangazwa Misikitini na Wafuasi wake! Ikitokezea Chadema ikapata Wafuasi Zanzibar pia itatangazwa Misikitini na Wafuasi Wake! You know why?
Kwasababu Uislamu Wazanzibari ndiyo Mila yao.
 
Ila Mbowe hanao huo udini? Hiyo CCM haina huo udini? Au kwa tafsiri yenu safu ikiwa na Waislamu wengi ndio Udini ila ikiwa na wakristo huo sio udini!

Rejea kada zote za uongozi za vyama vyote vya siasa pia kada zote za uongozi hata hapo kazini kwako ulipoajiriwa kisha uje na hoja ya udini wa Zitto kabwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr. Ramadhan Dau pale NSSF alijitahidi kuweka uwiano wenye weledi mkapiga yowe dunia ikajua. Ukienda Wizara na idara zote unazozijua wewe kisha leta uwiano kati ya wakristo na waislam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mfano Mdogo katika Ofisi/Idara ninayoifanyia Kazi kwenye Halmashauri X tumo Waislamu 2 na Wakristo 21.

Sasa unakuta Mtu anafungua Kwaya kwenye PC au Simu wengine wanafatisha Mistari.
Pia wanaweka Clips za Wachungaji mbalimbali na kusikiliza kwa Loud Speaker.

Lakini itokezee wewe Muislamu ufungue ile Kasida tu Basi Ofisi inasima kwa muda na kukuambia usilete mambo ya Udini Ofisini.

Sasa Nchi linapotokeza Jina la Muislamu tu ndiyo shida inapoanza.

Halmashauri ninayoifanyika Kazi.

NGAZI YA MKOA:
1) RC - Mkristo (RC)
2) RAS - Mkristo (RC)
3) Mkuu PCCB - Mkristo (RC)
4) RPC - Mkristo (RC)
5) RMO - Mkristo (RC)
6) RSO - Mkristo (TAG)
8) Mwenyekiti CCM - Mkristo (RC)
9) Mwenyekiti Chadema - Mkristo (RC)

NGAZI YA HALMASHURI:
1) DC - Mkristo (RC)
2) DAS - Mkristo - (RC)
3) DSO - Mkristo - (RC)
4) DED - Mkristo (Lutheran)
5) Mkuu PCCB - Mkristo (RC)
6) OCD - Mkristo (RC)
7) DMO - Mkristo (RC)
8) Mwenyekiti Chadema - Mkristo (RC)
9) Mwenyekiti CCM - Muislamu (Bakwata)

Sasa hapo hakuna anayehoji kuhusu Udini hapo na kila Mtu anaona ipo sawa.

Lakini inapokuja kwenye huyo M/Kiti CCM Wilaya imekuwa ugomvi kila siku Majungu.
Kuna Wakati DAS alikuwa Muislamu walifanya Fitna mpaka akaondolewa.

Yani Jamaa wanahisi Muislamu hana haki ya kuwepo popote pale! Na Akiwepo tu wanatafsiri ni Udini.
 

Teuzi za Ngosha ni udini mtupu
 
Ok, hebu tuzame zaidi. Hivi, Udini ni kuwa na watu wengi wa dini fulani, au ni mwelekeo wa fikra? Kwa Zanzibar, idadi kubwa ya wakazi ni waislamu, hivyo haishangazi kwamba chama chenye ushawishi mkubwa Zanzibar, viongozi wengi ni waislamu. Lakini haimaanishi kwamba kwa hoja hiyo tu, chama hicho kina Udini. Katika viongozi wa CCM Zanzibar sidhani kama kuna mkristo, sina hakika.

Lakini misingi aliyoweka baba wa taifa ni kutoruhusu ubaguzi wa aina yoyote, ili hata pale viongozi wa imani fulani wanakuwa wengi, hatuna haja ya kuhofu.

Kwa hiyo, tukemee hasa pale unapofanyika ubaguzi wa kidini, badala ya kuishia kutazama idadi. Tukemee matendo ya ubaguzi, badala ya orodha ya majina. Ninavyojua tuna sera ya 50 - 50 katika mambo ya idadi ya wanawake katika uongozi. Hatuna sera ya 50 - 50 katika dini za viongozi.

Lakini nasema hizi ni propaganda tu kwa sababu nakumbuka kuna wakati mh. Lukuvi aliwahi kwenda kanisani na kutoa kauli kali za ubaguzi wa kisiasa, CCM hawakulaani Bali walitetea. Kardinali Pengo anajulikana kushambulia serikali zinazoongozwa na marais waislamu, na kuwa kimya kwa marais wakatoliki, hata pale wanapofanya makosa makubwa. Sasa huo ndio Udini wa kukemewa.

Serikali ya CCM sasa hivi inasimamia ubaguzi mbaya sana wa kiitikadi na kikabila. Rais Magufuli anatamka waziwazi mchana kweupe, "akina Mushi siyo wa kuwaamini", na pia "makosa ni yenu kumchagua mtu wa upinzani" wakati anasisitiza "maendeleo hayana vyama". Huo ndio ubaguzi wa kukemewa, siyo mtu anaona orodha tu analia Udini. Badala ya kufanya utafiti hao viongozi wamefanya matendo gani ya kuwatia katika hatia ya Udini? Maana wamechaguliwa au hata kuteuliwa, hawajajichagua wao.
 
Mpeni Nchi muone Mambo,sura yake tunaijua ndio maana awamu hii amekuwa mpingaji wa Kila kitu.
 
Act wazalendo imejaa viongozi waandamizi wa kiislamu wote kwahili zito kabwe kachemka mno.ACT ni mbadala wa Cuf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama kuna ubaya kwamba asilimia 98% kuwa muslim endapo wote wana nia moja ya kuikomboa nchi yetu tanzania.[emoji1241]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…