Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Nimeisoma hii safu ya Viongozi wa ACT-Wazalendo ikanifikirisha sana kuhusu hatma ya ACT-Wazalendo kama chama kinachojiandaa kupewa dola nchini baada ya Uchaguzi Mkuu 2020!

Kuna msemo usemao, ‘’Mwenye macho haambiwi tazama’’. Nimeitazama hii orodha ya viongozi wa juu na kuniacha na maswali mengi!

Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa ngazi ya juu wa ACT-Wazalendo;
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo-Zitto Kabwe

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo-Maalim Seif

Mshauri Mkuu wa chama-Shaban Mambo na Juma Saanani

Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu-Ado Shaibu na Nassoro Ahmed Mazrui.

Wakuu wa Idara na Jumuiya za chama:

Mwenyekiti ngome ya wanawake- Mrs Mkiwa Kimwanga

Mwenyekiti wa ngome ya Vijana-Abdul Nondo

Idara ya Sera, Utafiti na Mafunzo-Idrissa Kowesa na Hassan Mosoud

Idara ya Habari na Mahusiano ya Umma-Salim Bimani

Idara ya Oganaizesheni na wanachama-Shaweji Mkato na Omari Ali Shehe

Idara ya Fedha na Uchumi-Abdalla Bakari na Rachel Kimambo

Idara ya Kampeni na Uchaguzi-Mohamed Masaga na Said Rashid

Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum-Pavu Abdalla na Mbarara Maharagande

Idara ya Amani-Mohamed Babu na Mohamed Noor

Idara ya Mambo ya Nje-Fatma Fereji na Boniface Mapunda

Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa-Hamad Mussa Yusuf na Edgar Mkosamari.

Je, wana Jamiiforums mnayaona haya ninayoyaona katika hii safu ya viongozi wa chama?
Ukisajili majina makubwa si ndio hao kesho wanakutema wanaunga mkono juhudi, ni kuanza grass-roots level. Tunakuza wachezaji kama Arsenal wakiboreka tutauza kwa hela kubwa.
 
Umerudia kusoma kwa sauti na kimya kimya hiki ulichokiandika!!?
Mkuu umechambua vizuri Sana kuhusu hii mada ya taswira ya udini kwenye Vyama vyetu hivi

Binafsi naungana nawewe kwenye kile ulichotaja propaganda ya Chama tawala, Tanzania enzi za Udini na ukabila pia ukanda tulishazitupa miaka na Tukamshukuru Mungu Kwa haya

Jambo lingine ambalo naendelea kuungana na wewe kwamba propaganda za CCM kuhusu kupandikiza chuki za Udini kwenye Vyama vingine ni pale hata wao wanaposahau kwamba hata katiba yetu imesema, Tanzania haina dini Ila katiba yetu mahali iilipomalizia kwamba (Watu wake ndio Wana dini)

Hiyo ndiyo aret ya mtu mwenye busara zake kutembea Nayo hasa linapokuja swala la kitaifa, Vyama vyetu kivyovyote vile vinapaswa vibebe taswira ya Kitaifa, vishughurikie matabaka na dosari zote ni mhimu kuzingatia

CCM, wao tayari ndio wanaoshika Dola, ili kuwanyima agenda kuvisema Vyama vyetu hivi ni kuhakikisha unakuwa smart kuliko wao, Kwa hiyo usiishie tu kulaumu kuhusu CCM na wapambe wake kuvisema Vyama pinzani kuwa havina taswira ya Kitaifa

Mkuu, Vyama pinzani sjui Kwa nini mara nyingi vinakuwa havitaki kujifunza, mfano mdogo tu kwamba, CUF ilikuwa na mwelekeo kama huu ambao leo Chama ambacho kinataka kuwa mbadara wa CCM kinafuata mfumo uleule ulioshindwa,

Tanzania haina Dini Ila watu wake wanadini, Watanzania hatujivunii uzuri wa dini zetu, Bali tunajivunia ule umoja wetu, na umoja wetu uligharamiwa, sasa mtu akiacha kuthamini gharama hiyo, Watanzania watamwadhibu Kwa kumpuuza hata kama lengo lake ni jema

Inawapasa viongozi wetu kuzingatia haya, hasa katika maswala yanayojumuisha halaiki ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
This is too low for you johnthebaptist
Hivi kwa nini wafuasi na watetezi wa CCM na serikali yake wa awamu hii mko hivi!?
Sitaki kuamini kuwa CCM ya sasa imechukua "millenials" ambao ni "empty" vichwani. Ninachoamini ni kuwa CCM inawatumia masikini kama mtaji wake wa kuendelea kuwa madarakani.
Hahahaaaa........au aanzishe kabakwata kake!
Zaburi 1:1
" Heri Mtu Yule Asiye Kwenda Katika Shauri La Wasio Haki, Wala Hakusimama Katika Njia Ya Wakosaji, Wala Hakuketi Barazani Pa Wenye Mizaha, Bali Sheria Ya Bwana Ndiyo Impendezayo, Na Sheria Yake Huitafakari Mchana Na Usiku, Nae Atakuwa Kama Uliopandwa Kandokando Ya Vijito Vya Maji Uzaao Matunda Yake Kwa Majira Yake Wala Jani Lake Halinyauki, Na Kila Alitendalo Litafanikiwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu akubariki mkuu.
Suala la kuangalia majina ya watu limezungumzwa miaka mingi na watanzania. Ni suala ambalo wakoloni walilitumia kutugawa ili watutawale

Changamoto inakuja kuwa wakati tabaka moja likitahadharisha tabaka jengine linajimwambafai kuwa nyie hamjasoma.

Lkn hao wasiosoma wakijipanga wale wanaanza kusema ' mnaleta udini' mnataka kuleta wenye ndevu ndefu kutawala.

Sasa mimi nadhani hayo mtayaona kwa kila chama yapo na kubwa tunalopaswa kuangalia na kujitofautisha ni kifalsafa za vyama hivyo.

Na moja ya falsafa kubwa ya vyama vyetu Tz ni kama ifuatavyo;-

Ccm, act, cuf ni vyama vya kikumunist na kilibelari.

Misingi ya vyama hivi mikuu

1. Kutoamini mungu - Secularism State
2. Ndoa za jinsia moja.

Sasa whether wana kubaliana na na kupractice falsafa hizo au laa, kitendo cha kuwa kwenye mrengo huo ni laana. Na ni Ukafiri.


Kwa upande wa pili wa shilingi falsafa ya chadema ni demokrasia yenye kulinda misingi ya kifamilia. Kukubali tofauti tulizonazo za kidini, kikabila na jinsia nk na kuzijuisha zote - Devercity State

Cdm inaamini ktk Demokrasia ya wengi wape na waache wajiamulie mambo yao. Kama act wanataka kuungana na wafuga ndevu waache wafanye hivyo, kama wanataka kukataza kuuza pombe, kamari na uzinzi hadharanj iwe sehemu ya sheria hao na sio lockdown au curfew waachwe wafanye hivyo ilimradi na wale wenye ustaarabu tofauti na huo wakiona uzito watatafuta jimbo litakaloruhusu mambo hayo.

Na ndio maana CDM inahimiza serikali ya majimbo. Ili tusiogopane, na kila raia akaishi jimbo lenye ustaarabu unaofata. Kama nilivyoona kule mufindi nguruwe zinambea tu mitaani, basi wanaoamini ustaarabu huo wataenda kuishi jumbo litakalounganishwa na mufindi.

Kwani Suala la kuangalia majina ya watu linawatisha wengi, ukiangalia sasa safu ya wizara na taasisi zake utakuja kuona 80% ni wa dhehebu moja. Ndio utajiuliza kuna shughuli gani za kitume zinaendelea humo, na kwanini walio nje ya dhehebu hilo ndio wenye manung'uniko zaidi. Hivyo ili tujiepushe na kasumba hizi za kikoloni suala ya kwanza la kulikimbilia ni serikali ya majimbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngumu sana kuliona hili,ukanda,udini ila nafikiri pia mleta mada una tatizo katika mtazamo wako...
Mimi nilichofanya ni kuuliza maswali!

Kama unadhani nina tatizo basi naomba ulitatue!
 
NiliwahI kutabiri way back 2013 humu kuwa ujio wa Rais mkristo wa awamu ya 5 utaiua CHADEMA! Na hicho ndicho kinachotokea sasa. Nguvu kubwa ya CHADEMA ilikuwa upinzani dhidi ya KIKWETE ( dini yake) na sio CCM! No wonder jumuia za makanisa zilikuwa mstari wa mbele katika upinzani huo lakini sasa WAMETULIA wanakula mema ya nchi na kelele za UDINI zimeisha ilhali DINI moja ndio imeshika hatamu! Matokeo yake (i) kudhoifika kwa CHADEMA (ii) KUIMARIKA kwa CMM ...

Ni ajabu hata "wanafikra" wetu wa JF wameingia katika mtego huu. Amin nawaambia, kwa kuituhumu ACT kuhusiano UDINI anayedhoofika ni CHADEMA, maana Wakristo watapigia kura Serikali kama kawaida, baadhi ya Waislam mtawasukuma ACT, wanaobaki wanapigia kura CCM!!
 
Back
Top Bottom