Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Hawa wakuu wa jumuiya za ACT mbona wako wawili wawili na haitoshi senior ni yupi.......
Au ndo muundo wenyewe...?
 
Kuna msemo usemao, ‘’Mwenye macho haambiwi tazama’’. Nimeitazama hii orodha ya viongozi wa juu na kuniacha na maswali mengi!
Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa ngazi ya juu wa Chama Cha Mapinduzi;

Mwenyekiti wa CCM- John Pombe Magufuli

Makamu Mwenyekiti Bara- Phillips Mangula

Makamu Mwenyekiti Visiwani- Mohamed Shein

Katibu Mkuu CCM - Bashiru Ally

Naibu Katibu Mkuu Bara- Rodrick Mpogolo

Naibu Katibu Mkuu Visiwani - Abdalla Mabodi

Mkuu wa Itikadi na Uenezi - Humphrey Polepole

Itikadi na Uenezi Zanzibar- Catherine Peter

Mwenyekiti UVCCM Taifa- Henry James

Katibu Mkuu CCM Taifa- Mwalimu Raymond

Katibu Mkuu Uhusiano wa Kimataifa - Ngemela Eslom Lubinga

Katibu Taifa, Masuala ya Uchumi na Fedha - Frank Haule

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi- Edmund Mndolwa

Mwenyekiti UWT Taifa- Gaudensia Kabaka
 
Idea ya yule kijana ilikuwa ni kushika ngome ya waumini fulani, halafu atumie kila hila kuunganisha ngome ya imani nyingine ili kukibwaga chama tawala. Lakini hiyo idea imekuwa nzuri kwenye ndoto tu, kuliko kwenye uhalisia wa siasa za nchi hii.
Kule kwenye Imani nyingine W ametulizana mahala fulani hivyo kaangukia pua na kwa ninavyoifahamu itaumuka balaaa
 
Drifter,
Mkuu umechambua vizuri Sana kuhusu hii mada ya taswira ya udini kwenye Vyama vyetu hivi

Binafsi naungana nawewe kwenye kile ulichotaja propaganda ya Chama tawala, Tanzania enzi za Udini na ukabila pia ukanda tulishazitupa miaka na Tukamshukuru Mungu Kwa haya

Jambo lingine ambalo naendelea kuungana na wewe kwamba propaganda za CCM kuhusu kupandikiza chuki za Udini kwenye Vyama vingine ni pale hata wao wanaposahau kwamba hata katiba yetu imesema, Tanzania haina dini Ila katiba yetu mahali iilipomalizia kwamba (Watu wake ndio Wana dini)

Hiyo ndiyo aret ya mtu mwenye busara zake kutembea Nayo hasa linapokuja swala la kitaifa, Vyama vyetu kivyovyote vile vinapaswa vibebe taswira ya Kitaifa, vishughurikie matabaka na dosari zote ni mhimu kuzingatia

CCM, wao tayari ndio wanaoshika Dola, ili kuwanyima agenda kuvisema Vyama vyetu hivi ni kuhakikisha unakuwa smart kuliko wao, Kwa hiyo usiishie tu kulaumu kuhusu CCM na wapambe wake kuvisema Vyama pinzani kuwa havina taswira ya Kitaifa

Mkuu, Vyama pinzani sjui Kwa nini mara nyingi vinakuwa havitaki kujifunza, mfano mdogo tu kwamba, CUF ilikuwa na mwelekeo kama huu ambao leo Chama ambacho kinataka kuwa mbadara wa CCM kinafuata mfumo uleule ulioshindwa,

Tanzania haina Dini Ila watu wake wanadini, Watanzania hatujivunii uzuri wa dini zetu, Bali tunajivunia ule umoja wetu, na umoja wetu uligharamiwa, sasa mtu akiacha kuthamini gharama hiyo, Watanzania watamwadhibu Kwa kumpuuza hata kama lengo lake ni jema

Inawapasa viongozi wetu kuzingatia haya, hasa katika maswala yanayojumuisha halaiki ya watu
 
Back
Top Bottom