Drifter,
Mkuu umechambua vizuri Sana kuhusu hii mada ya taswira ya udini kwenye Vyama vyetu hivi
Binafsi naungana nawewe kwenye kile ulichotaja propaganda ya Chama tawala, Tanzania enzi za Udini na ukabila pia ukanda tulishazitupa miaka na Tukamshukuru Mungu Kwa haya
Jambo lingine ambalo naendelea kuungana na wewe kwamba propaganda za CCM kuhusu kupandikiza chuki za Udini kwenye Vyama vingine ni pale hata wao wanaposahau kwamba hata katiba yetu imesema, Tanzania haina dini Ila katiba yetu mahali iilipomalizia kwamba (Watu wake ndio Wana dini)
Hiyo ndiyo aret ya mtu mwenye busara zake kutembea Nayo hasa linapokuja swala la kitaifa, Vyama vyetu kivyovyote vile vinapaswa vibebe taswira ya Kitaifa, vishughurikie matabaka na dosari zote ni mhimu kuzingatia
CCM, wao tayari ndio wanaoshika Dola, ili kuwanyima agenda kuvisema Vyama vyetu hivi ni kuhakikisha unakuwa smart kuliko wao, Kwa hiyo usiishie tu kulaumu kuhusu CCM na wapambe wake kuvisema Vyama pinzani kuwa havina taswira ya Kitaifa
Mkuu, Vyama pinzani sjui Kwa nini mara nyingi vinakuwa havitaki kujifunza, mfano mdogo tu kwamba, CUF ilikuwa na mwelekeo kama huu ambao leo Chama ambacho kinataka kuwa mbadara wa CCM kinafuata mfumo uleule ulioshindwa,
Tanzania haina Dini Ila watu wake wanadini, Watanzania hatujivunii uzuri wa dini zetu, Bali tunajivunia ule umoja wetu, na umoja wetu uligharamiwa, sasa mtu akiacha kuthamini gharama hiyo, Watanzania watamwadhibu Kwa kumpuuza hata kama lengo lake ni jema
Inawapasa viongozi wetu kuzingatia haya, hasa katika maswala yanayojumuisha halaiki ya watu