Hii Simba SC hata ukitangulia goal 4 lazima upigwe TU kila GoTi litapigwa 😁

Hii Simba SC hata ukitangulia goal 4 lazima upigwe TU kila GoTi litapigwa 😁

Watu hawajamshtukia huyo Ngunguboy. Yeye anajua kabisa hagombei kutokana na katiba kumbana lakini anapambana aingize mtu wake ili yeye arudi Simba kwa mgongo wa kwenye nafasi za uteuzi. Kwa hiyo wanasimba wakichanganya tu huyo Ngunguboy mtakuwa naye sana.
Huyu hawezi kuwa kamwee pale simba tena, mamluki hana chake kabisa.
 
Penati ni Mbeleko wa wazi , FVS takataka

Refa alionekana tokea alitoa Kona mbili za Bure kwa Simba .

Naacha kufuatilia NBC nalinda IQ yangu , mpira wetu ni maigizo , tukutane michuano ya Kimataifa aibu kubwa itakuja
Mkuu unaumia ukiwa wapi😁😁
 
Hongereni Simba kwa comeback na poleni Namungo kwa kuzembea mlikuwa na uwezo wa kumuua tembo kwa ubua. Simba bado kuna mizaha mingi sana kiasi unajiuliza hawa jamaa wapo serious wanautaka ubingwa? Walitafuta sana goli bada ya kulipata tu wakaanza mizaha yao kama waliyokuwa wanafanya kipidi cha Fadlu. Wakashusha tempo kabisa wakaanza udambwidambwi badala ya kufanya jukumu mama la kuimaliza ile mechi mapema. Simba walikuwa na uwezo wa kuimaliza ile mechi ndani ya dakika 15 halafu ndio waanze ule upuuzi wao. Wacheaji wa Simba wakumbushwe kuwa football ni kama masumbwi tu kibonde anaweza kukuotea halafu ikawa ndio imeenda hiyo unabaki unasoma namba.

Kila siku nasema Rushne ni bonge la beki lakini huyo jamaa tokea apewe tambala siku hizi hata zile slide tackling huzioni washambuliaji wanafunga mbele yake anazatazama. Ni kama vile kawa bosi hataki kuchafuka. Halafu anatabia ya kukaa na mpira muda mrefu bila sababu za msingi. Aukanyage mpira kwanza matokeo yake anaipoozesha timu wakati wenzake gari limewaka kule mbele na katikati ya uwanja wanasubiri pasi. Yule Nindi naye atapotea muda sio mrefu. Kacheza mechi mbili tatu naye anajiona superstaa naye akipewa mpira anatembea nao na yeye aukanyage kwanza kama Rushine.

Chama umri umeshaenda sana ni wakati sasa benchi la ufundi la Simba limpunguzie majukumu ili aweze kusaidia Simba kwenye nyakati ngumu na pia aweze kutumika msimu mmoja zaidi ili Simba wapate nafasi ya kupata mchezaji ambaye walau atakuwa na uwezo kama wake kwa asilimia hata 75%. Vinginevyo wakiendela kumtumia jinsi wanavyomtumia sasa nina hakika hata msimu huu atamaliza kwa shida. Benchi la ufundi ni vizuri wakawa wanaanza na Abraham Morice kwa sababu naona kama ameimarika sana na ameanza kuwa mbunifu wa kutengeneza nafasi za magoli na pia ana energy ya kutosha. Kwa Chama yeye hata akiwa anapewa zile dakika 20 za mwisho zinamtosha sana kufanya maajabu yake na hata kubadilisha matokeo pale timu inapokuwa imebanwa.

Kipa naye ni tatizo kubwa pale Simba hasa wanapoenda kwenye mechi za kimataifa. Yaani huyo kipa asipojirekebisha atatunguiliwa sana magoli ya mbali kwa sababu anapenda kusogea mbele ya goli bila sababu za msingi. Pia anapenda kuka sana mpira miguuni mwake wakati footwork yake ni mbovu. Na ile tabia yake ya kupiga pasi kati kati badala ya pembeni ndio hatari zaidi hasa Simba wakikutana na timu inayofanya pressing kuanzia juu na yenye washambuliaji wenye kasi. Mpaka leo sijajua ni kwa nini Sinba hawakusajili kipa mwenye viwango wakati dirisha kubwa.

Mwisho benchi la ufundi la Simba nalo liwafundishe washambuliaji wao kutumia nafasi wanazopata. Washambuliaji hawana utulivu kabisa mbele ya goli na ni kama vile kila mshambuliaji anakuwa na papara na kutaka afunge yeye tu. Simba inapata nafasi kumi za wazi halafu wanazotumia kupata magoli ni mbili/tatu basi. Kwenye CAF CL nafasi zikipatikana sana sana utakuta ni mbili/tatu kwenye mchezo mmoja kwa hiyo usipozitumia kikamilifu hupati matokeo. Kwa hili Simba ni lazima watafute mshambuliaji wa viwango vinginevyo wataishia kuwa wasindikizaji.

Ni mtizamo tu.
Uko sahihi
 
Huyu hawezi kuwa kamwee pale simba tena, mamluki hana chake kabisa.
Paka huwa ana roho saba. Unaweza kumpiga ukadhani umeshamuua ukashangaa baadae kafufuka. Umeshawahi kujiuliza ni kwanini kila siku anafanya press wakati ameshawatangazia baadhi ya watu kuwa hagombei tena. Vipi alifanya mkutano Bunju akafikia mpaka kuunda bodi mpya wakati yeye hagombei. Na je vipi ni kwanini alifikia mpaka kutaka kuongezewa muda ili uchaguzi ufanyike baada ya AFCON.

Endeleeni kumchukulia poa ila msije mkashangaa ndio akaja kuwa mwenyekiti wa bodi ajaye kama sio mjumbne wa bodi.
 
Bando langu limebaki la Jf tu, nimegoma kuweka bando leo .

Labda niliangalia kwa haraka , ila nilivyoona Iko hivi ukitizama kwa nyuma ni Clear Penat ila kamera ilipovutwa kwa karibu ilionyesha kuwa dhahiri mchezaji wa Namungo alikosa mpira na aliukosa mguu wa Doumbia na wakati mguu unatua chini hajafanya mgusano na Doumbia.

Ngoja nimuite Dada yangu Shadeeya aje atoe maoni yake , alisema kuwa penati ya halali uamuzi wangu nafuta na narudi kufuatilia NBC , akisema ni Mbeleko basi nitakuwa nafuatilia michuano ya CAF pekee kwa Africa na bongo ligi zao naacha naacha rasmi 😂 😆
Nimekuja ndugu jana nilikuwa busy nikatoka sikurudi tena.

Hii imekaa kimbeleko mbeleko ila ombi langu tuendelee tu kuangalia ligi yetu pendwa ya NBC. Usiache.
 
Nimekuja ndugu jana nilikuwa busy nikatoka sikurudi tena.

Hii imekaa kimbeleko mbeleko ila ombi langu tuendelee tu kuangalia ligi yetu pendwa ya NBC. Usiache.
Naanzaje kuacha kuangalia Yanga hii na Shalulile ? 😂

Nashangaa wachambuzi hawaongelei , FVS wangekuwa wanavuta kwa ukaribu angle zote ile isingekuwa tuta , ile ya Taifa stars na Morocco ya Nado kila mtu duniani alisema ni clear Penalty lakini wenzetu wanavuta kwa karibu sana waligundua Nado alianza kujirusha kabla ya movement.

Juzi nilicheki El Classico Kuna moment nilisema kabisa ni Penalty ila VAR ilivuta kila angle katika slow motion nzuri mpaka unaona kabisa haikuwa Penati
 
Naanzaje kuacha kuangalia Yanga hii na Shalulile ? 😂
Ewaaaa. Haya ndo maneno sasa. 💃
Nashangaa wachambuzi hawaongelei , FVS wangekuwa wanavuta kwa ukaribu angle zote ile isingekuwa tuta , ile ya Taifa stars na Morocco ya Nado kila mtu duniani alisema ni clear Penalty lakini wenzetu wanavuta kwa karibu sana waligundua Nado alianza kujirusha kabla ya movement.

Juzi nilicheki El Classico Kuna moment nilisema kabisa ni Penalty ila VAR ilivuta kila angle katika slow motion nzuri mpaka unaona kabisa haikuwa Penati
Inatakiwa hiyo FVS waiboreshe ili haya mapungufu na hizi sintofahamu ambazo hazipatiwi ufumbuzi ulio sahihi zisijitokeze.
 
Back
Top Bottom