Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Kuna vitu wanatakiwa kuboresha
 
Wamesema kwenye kituo kimoja ndani ya mwezi, wakati Kuna watu wanasafiri kila wiki. Na hata hivyo kwa nn mara 3?? Mimi najuaje kamaa nitaumwa mara 4 au 5??
Mleta mada kaleta wakati details hazijakamilika, tusubir mpaka ijumaa tutakuwa tumejua A to Z
 
Hapa ndio wa Tz tunatakiwa tuamke na kuingia barabarani kama ilivyokuwa Srilanka!
tatizo letu wa Tz tu manyangau sana na wazito kuhoji!
Wewe unaona hata akina Mbowe,Lissu,zitto viongozi wa dini na wengine waliojipambanua kuwa wapinzani wa serikali ya awamu ya tano wako busy kumung'unya asali tu hawasemi chochote harafu utegemee mabadiriko hapa nchini kweli?
 
Vipi kuhusu mzazi??
 
Yaani Mgonjwa Anapangiwa Sehemu Ya Kutibiwa Na Aende Mara Ngapi
Uhuni Ukomeshwe Haraka
 
Anyway, Bima zibaki hiari.

Watu wachague sehemu ya kupeleka pesa zao.

Easy
 
Wafanyakazi sijui vyama vyenu huwa vinawasaidia nini.....!!?
Kama mazezeta vile.....!!
Haviwezi kuwahamasisha hata;
1) Migomo
2) Maandamano
3) Basi vitetee maslahi yenu...

Vyenyewe vipo kwa ajiri ya kuwakandamiza tu miaka inaenda vilio ni vile vile....
Ivi huwa mna matatizo gani...!!?

Kama ni mfumo au ni Uongozi si muwakatae hata kwa kuandamana....
 
Nimewapigia NHIF
Wamesema ni kweli yanayosemwa mitandaoni

Muda wa Jubilee, Strategies kuanza vuna watu
 
Wafanyakazi ndo wenye pesa huwezi kumuamulia mwenye fedha kutibiwa anakotaka la sivyo serikali iruhusu mifuko mingine ili mchangiaji awe na uhuru wa kuchagua pa kwenda
 
Wafanyakazi ndo wenye pesa huwezi kumuamulia mwenye fedha kutibiwa anakotaka la sivyo serikali iruhusu mifuko mingine ili mchangiaji awe na uhuru wa kuchagua pa kwenda
 
Kutatua tatizo la mtu mmoja mmoja kwakuumiza wengi wenye huitaji ni ujinga.lakini pia hiyo yawatu kuzunguka kwenye vituo vya afya mbali mbali nikwasababu mtu haridhishwi na aina ya matibabu aliyoyapata kituo A.Mimi kuna mzee namfahamu yuko kwenye matibabu ya cancer ya tumbo sasa hivi na iligundulika baada ya kuhama hospital karibu 4 ya 5 ndo akaambiwa acheki CT scan ndo wakaona tumbo haliko poa.Uko nyuma kote alikopita walikua wanamwambia tu ana vidonda vya tumbo wanamlundika madawa.Kwahiyo angekua nimtu wakuridhika namatibabu aliyokua anayapata siajabu angekufa bila kujua kilichomuua.Watu wenhi magonjwa yao yanakua makubwa kwasababu ya kuridhika na matibabu anayopewa awali hata kama anaona hayaridhishi.Huo mfuko umekosa ubunifu ndo maana wanataka kuja na short cut badala yakufanya maboresho kwa watoa huduma wake.
 
Kumbe unajua kumbe hizo bima zingine zinatoa matibabu mazuri kwa wanachama wake todauti na Nhif.Tatizo ni aina ya huduma anayopata mgonjwa ndio itakayomfanya atulie.
 
Unaongea hivyo utafikiri watu wote wanaishi daresalam au watu wamepandwa sehemu moja.Ila pia pamoja na kuchagua unadhani ni vituo vingapi vitapata wagongwa.Kuna ambavyo vitakua na mlundikano wa wagonjwa huku vingine vikiwa vitupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…