Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Habari za mchana wapendwa.

Habari za kusikitisha - NHIF wamebadilisha mifumo yao ya matumizi ya card.

1- Tegemezi wengi wameondolewa,

2- Card itumike x 3 tu kwa mwezi.

3- Kama umetibiwa Jana au juzi, ukienda hospitali nyingine utatakiwa uende na Referral toka hiyo hospitali ulikotibiwa mara ya mwisho.

Makorokoro kibao yamebadilika. Tunaendelea kuwasikiliza. Ni shida tupu.

HII SIO HAKI MTU ANACHANGIA AFU HUDUMA ANAPANGIWA ATIBIWE KTK KITUO KIMOJA TU KWA MWEZI NA NA MARA TATU TU KWA MWEZ HII SIO HAKI. BASI WATUMISHI WARUHUSIWE KUJIUNGA NA MIFUKO MINGINE ISIWE LAZIMA NHIF ILI AFUATE HUDUMA SEHEMU ANAYOONA INAFAA
Kuwa na mifuko mingine ndiyo njia pekee ya kutuokoa! Irudi kama ilivyokuwa kabla ya kipindi Fulani.
 
Mtanzania yuko wapi huyo wa kuandamana? Ni rahisi ku mobilize wanafunzi wa sekondary kuliko ku mobilize mijitu mizima kusimamia haki zao kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Mtanzania aliekula ugali dagaa akashiba na kahela ka bando anako sahau kuhusu kuandamana.
Hapa ndio wa Tz tunatakiwa tuamke na kuingia barabarani kama ilivyokuwa Srilanka!
tatizo letu wa Tz tu manyangau sana na wazito kuhoji!
 
Kw
Woga na hofu nyingine ni za kipuuzi kabisa. NHIF inataka bima iwe kama lile "duka la Mhindi" zama za ukoloni na enzi ya Mwalimu ukitaka ukitaka bidhaa/huduma chukua usipotaka acha na huna pa kwenda pengine.

Hivi kweli mtu anaweza kupenda tu kuzurura kwenye hospitali bila kuwa na hitaji la kujua afya yake. Na unamuwekea pingamizi la kijinga kama hili la kutokwenda hospitali nyingine mpaka kwa mizengwe! Pamoja na sisi watumiaji tutaumia. Nadhani kutakuwa na kilio kwa hospitali nyingi za binafsi ambazo zimejiunga kutoa huduma kupitia NHIF.

Kuna watu wanatamani tuwe "Wasirilanka" kwa kweli.
Kwa maana ingine mjitegemee kwa swala la afya!
 
TAARIFA KUHUSU BIMA ZA WAGOJWA KUKATAA KUWA AUTHORISED KWENYE MFUMO

Utaratibu wa mfuko wa NHIF umebadilika ili kuzuia polyvisit za wagonjwa pamoja na polyservices zingine za wagonjwa wetu

Kuanzia sasa mteja atakua na nafasi ya VISIT 3 TU KWA MWEZI kwa kituo husika na mteja hawezi kujiamulia kuhama Kituo cha kutolea huduma(Hosp,H/na disp) moja kwenda nyingine kwa kujiamulia, mfano mgonjwa akianza kutibiwa Kituo X basi atakua wa X tu mpaka pale X tutakapo amua sisi mrefer mgonjwa kwenda sehemu nyingine la sivyo mgonjwa hataweza kwenda sehemu nyingine ,kama kuna emergency kutakua kuna utaratibu kwenye mfumo wa kuruhusu huduma ziendelee

Aidha mfuko utaweka pia utaratibu wa wale wagonjwa ambao ni wa refill ili kama amekuja kwa ajili ya refill asiweze kuchomekea kitu kingine cha kimatibabu

Kwa huduma za physio, meno kutawekwa utaratibu maalumu ili huduma kama hizo ziendelee

Mfuko unataka kubana wale wa watu wanaozunguka kila kituo kufanya vipimo, kuona madaktari na kulinganisha huduma za madaktari

Ni hayo tu ndugu zangu,muwe ka kazi njema.

Watu wa mapokezi mutakua munawaelekeza kwa upole wateja ambao kadi zao zimepata changamoto hizo.

NHIF.
Kama ni kweli basi ni changamoto.
Maana kuugua hakuna taarifa wala muda maalum.
Halafu kwa mfano mtu ni mtumishi haugui mara kwa mara na hata akiugua hatumii bima! Ana mtegemezi wake mmoja ambaye ni mtu mzima, anatakiwa kupata huduma mara kwa mara, kisha unmpangia muda wa matibabu what if akiugua zaidi ya hapo???
I wish isiwe kweli!
 
Hivi unamdhibiti vipi mtu kuumwa??
Yani unawezaje kumpangia mtu muda wa kuumwa?
AAR na STRATEGIES wateja wao huwa hawana tabia za kujirudia rudia kwenye vituo vya afya kupata huduma,, ila NHIF leo yupo hapa, kesho pale, kesho kutwa huku, ndyo maana wameamua kuwadhiti, hata wewe jiulize ndugu yangu, mtu hata dose hii hajamaliza kashahamia kwingine, huko nako hajamaliza dose aliyopewa kaenda kwingine, unakuta mtu mmoja kahudhuria mara 10 au zaidi vituo vya afya kwa mwezi!

NSSF wao huo utaratibu wa kutibiwa kituo kimoja tu na mara 3 wanao muda mrefu Sana, wateja wao hawasumbui washazoea.

Kwa Sasa kinachowafavour AAR na STRATEGIES, wao hawanalimit nyingi hasa upande wa dawa na vipimo, kwa hyo unaweza tibiwa vizur ukakaa Zaid ya miezi 3 hospital hupajui!

Ila Kuna viashiria nmeviona juzi juzi ndyo maana nasema Ni suala la muda huko kwao
 
Huna hoja kwa kuwa leo nipo morogoro na najisikia kuumwa niitaebda hospital hapo morogoro. Baada ya wiki nikasafiri kwenda Dodoma nikajiskia kuumwa nitaenda tena hospital, baada ya wiki mbili nikaenda dar na nikajiskia kuumwa si ntaenda tena hospital?

Sio haja ya kuweka limit, kwa kuwa so far nachojua wanaotibiwa ni wachache kuliko ambao hawatibiwi. Kuna watu wana miaka minne hawajui hospitali ipoje. Huyo nae utasema arudishiwe oesa yake ya miaka minne?
 
Natibiwa JKCI kwa kuhudhuria clinic kwa huu ujinga nikipatwa na mafua niende kwenye hospital ya moyo?
Soma vizur maelezo ndgu, Kuna special Case zinazohitaji clinics , kama hiyo ya shda ya moyo unayozungumzia, kwa hyo utahitajika kahudhuria hapohapo JKCI unapofanyia clinic, lakin kwa mambo madogomadogo kama mafua, kikohozi, malaria, UTI tafuta kituo chako pendwa kimoja TU, in case hali yako Ni mbaya Sana unapewa rufaa, utaratibu sio mgum hata kidogo boss
 
Huna hoja kwa kuwa leo nipo morogoro na najisikia kuumwa niitaebda hospital hapo morogoro. Baada ya wiki nikasafiri kwenda Dodoma nikajiskia kuumwa nitaenda tena hospital, baada ya wiki mbili nikaenda dar na nikajiskia kuumwa si ntaenda tena hospital?

Sio haja ya kuweka limit, kwa kuwa so far nachojua wanaotibiwa ni wachache kuliko ambao hawatibiwi. Kuna watu wana miaka minne hawajui hospitali ipoje. Huyo nae utasema arudishiwe oesa yake ya miaka minne?
Ndyo maana ikawekwa mara tatu mkuu kwa mwezi, au hakijaeleweka Nini?
 
Nawaunga mkono NHIF, maana Kuna wateja ambao ni wazururaji kwenye vituo vya afya, leo yuko huku, kesho kule , kesho kutwa kule, yaan daily yeye ni kuugua kweli?

Hawa wateja wa namna hii wanatia hasara Sana katika vituo vya afya kwa makosa ya double claiming!

Unakuta katoka kituo A Jana na shida ambayo kesho anakwenda nayo kituo B, na dawa anapewa zilezile, matokeo yake kituo B kinakatwa!

Kwenye hili halihusiani na Mama Samia!

NB: hata hiyo mara 3 kwa mwezi Ni offer nzuri naomba mlio katik utumishi wa umma mpokee hivyo hivyo, maana dawa so chakula, pengine wamefanya hivyo kudhibiti matumizi ya dawa hovyo

HONGERA NHIF KWA KULIONA HILI, hayo mengine simo
Kweli wewe ni nyumbu uliolamba asali ukashiba. Fikiria kwa kichwa sio makalio. Wafikirie watu ambao wana CP na matatizo ya figo ambao wanatakiwa kwenda kuhudhuria clinic mara 3 na zaidi. Kuna hospitali zingine huduma zao ni mbaya hazikizi mahitaji utaenda hapo hapo tu? Muhimbili yenyewe rubbish huduma yake ni chini ya kiwango. Kama wewe umezikuta kwa Baba ako na Mama ako wengine atujazikuta tunafight kwa nguvu zetu.
 
Huna hoja kwa kuwa leo nipo morogoro na najisikia kuumwa niitaebda hospital hapo morogoro. Baada ya wiki nikasafiri kwenda Dodoma nikajiskia kuumwa nitaenda tena hospital, baada ya wiki mbili nikaenda dar na nikajiskia kuumwa si ntaenda tena hospital?

Sio haja ya kuweka limit, kwa kuwa so far nachojua wanaotibiwa ni wachache kuliko ambao hawatibiwi. Kuna watu wana miaka minne hawajui hospitali ipoje. Huyo nae utasema arudishiwe oesa yake ya miaka minne?
Kwahiyo wewe utakuwa unasafiri safiri hovyo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kweli wewe ni nyumbu uliolamba asali ukashiba. Fikiria kwa kichwa sio makalio. Wafikirie watu ambao wana CP na matatizo ya figo ambao wanatakiwa kwenda kuhudhuria clinic mara 3 na zaidi. Kuna hospitali zingine huduma zao ni mbaya hazikizi mahitaji utaenda hapo hapo tu? Muhimbili yenyewe rubbish huduma yake ni chini ya kiwango. Kama wewe umezikuta kwa Baba ako na Mama ako wengine atujazikuta tunafight kwa nguvu zetu.
Usikimbilie matusi, utaratibu unaelezaje kwa case kama hiyo?
 
Back
Top Bottom