Umeandika yote kwa usahihi lakini chanzo cha yote ni UMASIKINI NA BAJETI ULIYO NAYO ISIYONYUMBULIKA.
Mtu kuja kwako lazima atoe taarifa hili naunga hoja kwa 100% ndiyo mfumo wa maisha.
Lakini mtu anapokuja bila taarifa ameshakuja tayari, hatuangalii madhaifu ya kuja bila taarifa muda huo tunakabiliana na shida ya kuja kwake bila taarifa.
Mtu msitaarabu na mwenye uwezo na bajeti ya ziada ambaye hayana dhiki na umasikini, atamkaribisha mgeni atampeleka nyumbani, atampa maji,chakula na mengineyo, haijalishi utamlaza sebuleni, kwenye ukumbi wa nyumba, jikoni kwenye korido siku kwanza ipite.
Kukicha au ucku ule ule unamwambia nashukru umekuja lakini ulijisahau kuja bila kuniambia.
Kwangu hakuna nafasi kwa sasa ya kutunza mgeni hatakama nafasi ipo utatumia lugha ya kiutu.
Hivo utakaa hizi cku 3 kwa shida ili tutafute nauli urudi au kama una nauli ya kurudi itabidi urudi siku fulani.
Kama wote hamna nauli hilo sasa ni tatizo ambalo mtajadili kama familia wewe na ndugu zako huko alikotoka kuwa huku hakuna nafasi ya yeye kukaa na wote maisha ni magumu, uzeni mbuzi huko, kuku, bata, njiwa au gunia la mahindi mtume nauli arudi nyumbani.
KUMZIMIA MTU SIMU, KUMKIMBIA STAND NI DALILI ZA UBABAISHAJI, UJANJA UJANJA, UELEWA MDOGO NA UPUUZI.
Pokea simu mwambie ukweli bila kupepesa macho full stop.
Mwisho.
Umasikini ni kitu kibaya sana unaweza kuongozwa na umasikini huo ukahisi uko sahihi maamuzi yako kumbe tu ni umasikini.