Hii tabia ya wanawake wa siku hizi kupenda uke wenza inasababishwa na nini?

Wanawake baadhi wanatafuta wanaume waliopo vizuri kiuchumi. Wanaume waliopo vizuri kiuchumi wengi wana miaka kuanzia 35 ambapo wengi wao wana familia tayari.
Hii ipo kwa bi wadogo ila bi wakubwa ukiona kakubali uke wenza ujue ana kipozeo chake kwahiyo anafurahia kupata muda mwingi wa kuenjoy na bwana mdogo, halafu wakati huo mume yupo bize na bi mdogo hata muda kumfatilia hana,,,,
 
Hii ni kutokana na uchache wa wanaume
 
Tuwe wakweli sisi watafutaji.
Tunapoenda mbali na sehemu tulipoacha familia.
Tunakuwa wapweke, wakiwa, hatuna sapoti ya ndugu Wala marafiki.
Upo mwenyewe tu kama nyani Mzee.

Unapotongoza binti, anakuwa na muda na wewe
Kwako kama kwake, hivyo hata ukimwambia umeoa hajali.

Ndicho kitumbo kinapotokea, ila Mimi alisema anataka mbegu tu.

Natoa huduma nikiwa nipo vizuri, nikiwa vibaya ananitumia maokoto.

Hivyo fresh tu
 
So mnaleana
 
Hamna wanaume wanao windwa na wanawake kama wanaume walio oa,haijalishi upo mbali na mkeo au laah. Sometimes sio hela, kuna mabinti kibao wanakazi na hela zao bado wamekubali kuwa nyumba ndogo. Yaani unaweza ukawa unapata tabu kipindi upo single kwenye utongozaji, ila ukioa wanajileta wenyewe na ukiona huwaelewi wanakutongoza. Wanawake wengi wana mentality mume wa mtu anajua kucare, kutunza, mara sijui kitandani...... nk na majamaa wakijileta wanawafyatua.
 
Hii inaitwa tutabanana wote humu humu.
 
Nadhani nilikua Mimi miongoni mwao ila ni 1/10

Mimi nilikua na campgne uaminifu ila ni ngumu sana kwa MWANAUME RIJALI KUWA mstahimilivu hasa mke akijifungua na mapenzi yakihamia kwa watoto

Eye eyes
Ulipovunjika mguu, mke wako alikuhudumia wakati ulikuwa dhaifu na hakukuona mzigo. Leo Mungu amekupa afya, umemlipa kwa usaliti.

Usisahau aliyekusimamia wakati wa maumivu kwa sababu ya tamaa ya muda mfupi. Maisha yana mzunguko; siku ukidhoofika tena, utajua thamani ya aliyekuwa nawe.
 
🥺 Umenikumbusha mbali sana basi TU

Narekebisha yotee najua hii DUNIA hakuna wakamilifu

Najirekebisha

Mwenyezi Mungu anisimamie/ aniongozee
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…