Hii thinking ni ya Japan au Old Europe na USA lakini sio Afrika

Yes... Kiongozi unang'ang'ania vichwa panzi kwenye baraza la mawaziri maana wameombewa na godfather. Inaonyesha mwenyewe huna uwezo imetokea kwa bahati mbaya tu. Itakapofika muda litendee taifa wema kwa kuhakikisha tunapata mtu wa kutuvusha.
Na hilo Baraza la Mawaziri pamoja na Bunge zima ni chaguo la Hayati Magufuri yaani mpandaji ni yeye.
 
Hakika umenena vyema JPM ni mwanaume wakati SAMIAH ni mwanamke lazima matendo na akili viwe tofauti kwa asilimia 76%
 
Akaona haitoshi akataka kumpiku Mungu akaingia lab akaja na solusheni ya kuuwa wote waliompinga.
 
Wakati jakaya anahangaika na wabrazil kutaka kujenga Hilo bwawa,bado ulikua unakunya nje kule maswali!?..
 
Kama ningekuwa nawafananisha sura zao, hapo ningekubaliana na madai yako kwamba kila mmoja ana muonekano wake tofauti wa sura, kulinganisha na mwenzie.

Lakini tunapokuja kwenye suala la utendaji serikalini, hapa mjomba tusidanganyane, kuna standard lazima ifikiwe ili kuhakikisha panakuwepo na uwajibikaji ili kuondoa uzembe serikalini.

Lakini kinyume na hapo, ni kuliangamiza taifa, na hatuwezi kuangalia taifa likiangamizwa kwa kigezo chepesi tu kwamba kila mmoja ana style yake ya uongozi, huku ni kutokujielewa.
 
Kwenye nchi zinazojitambua wanatakiwa sana na wanalindwa na karibia kila mtu Mkuu. Labda kwa nchi kama zetu hizi ndo hawatakiwi na wachache wenye nguvu
 
Atasimuliwa vizazi hadi vizazi, kumwelezea inahitajika filisophia kubwa sana, alikuwa mnara mkubwa sanaa huyo mwamba
Kweli kabisa.
Ipo siku zitapewa heshima anayostahili.
Ngoja kwa sasa tujifanye kumnanga na kumsema vibaya bila kufikiria kwamba ndo tunampaisha na kumfanya azidi kujulikana zaidi na asisahaulike kama tunavyotamani!
 
Kweli kabisa
 
Na la SGR nalo lilikuwepo toka enzi za Nyerere?

Na kutumia umeme wa Stiglers ili kuendesha SGR nalo lilikuwepo toka enzi za Nyerere?

Wakati mwingine naona mnajitesa sana.
Kwani ni lazima watu wapotee watishwe wabaguliwe, wauawe ndo kiongozi afanye maendeleo ?
 
Huo uzembe umekuwepo serikalini kabla hata JPM hajazaliwa ukumbuke hilo. Na utaendelea kuwepo siku zote,

Wapo wenye kuona afadhali awamu ya Samia na wapo wenye kuiona awamu ya JPM ilikuwa bomba na kila kundi linazo hoja zake.
 
MRADI WA TANGU ENZI ZA MWALIMU ......

Mradi wa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), Tanesco wametumia upembuzi yakinifu uliofanywa miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway. Wakala pia wametumia mpango wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na M/S Hafslund na M/s Norplan (wote kutoka Norway)

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Magufuli hakuwasikiliza, akasimamia kile alichokiamini, leo tunaambiwa Bwawa linakaribia kujaa, tena tunatangaziwa hivyo na mpinzani aliyeamua kukubali ukweli ili asijitese nafsi yake, tena linajazwa na zile mvua walizosema zisingenyesha.
'Single' inayotamba kwa sasa hivi ni uwepo wa vyanzo mbalimbali "diverse sources of electricity", na vinatakiwa viwepo haraka sana ili kufikia 2025 tuwe na uwezo wa kuzalisha 5000MW". Na mtu huyo huyo hakuelezi umeme wote huo ni nani atakayekuwa anautumia, na ni nani atakuwa analipa gharama za huo umeme wa ziada!

Makamba na timu yake ni majambazi hasa! Wako kila sehemu wakitafuta wawekezaji, ili umeme hata huo wa bei nafuu unaozalishwa na hilo bwawa uwe wa aghali zaidi!

Mimi natamani hivi karibuni tupate kiongozi ambaye atawatapisha haya yote wanayoyameza sasa hivi. Tena wayatapike kwa aibu kubwa, hata ikipidi kuswekwa ndani wakikutwa na hatia ya ujambazi.
 
Huo uzembe umekuwepo serikalini kabla hata JPM hajazaliwa ukumbuke hilo. Na utaendelea kuwepo siku zote,

Wapo wenye kuona afadhali awamu ya Samia na wapo wenye kuiona awamu ya JPM ilikuwa bomba na kila kundi linazo hoja zake.
Of course, kama wewe ni nyang'anyi haitashangaza kuwa katika kundi la manyang'anyi wenzio, kwani hili nalo liwe na kusita kulitambua?
 
Ni kweli, lakini Kama process inachukua miaka hamsini na wananchi wanataabika kwa kukosa umeme huo ni ujuha!!! Lazima tubadilike!

Kwahiyo unataka kuniambia kama mtoto ameshindwa kutembea kwa miaka zaidi ya hamsini tutegemee kuna kutembea kweli?
Mnataka kutuambia Tanzania haina umeme hadi sasa?
 
Umeme kwanza Makamba alisema shida ni mvua, baadaye akasema mitambo imechoka sasa sina uhakika amekuja na kisingizio hadithi gani?

Biashara na maisha ya wengi zimeathirika wakicheza hii michezo yao na maisha ya watu.
 
Huo uzembe umekuwepo serikalini kabla hata JPM hajazaliwa ukumbuke hilo. Na utaendelea kuwepo siku zote,

Wapo wenye kuona afadhali awamu ya Samia na wapo wenye kuiona awamu ya JPM ilikuwa bomba na kila kundi linazo hoja zake.
Hata kama uzembe umekuwepo kabla, lakini anayejitokeza kuuondoa kwa vitendo lazima apongezwe, na ni ajabu sana kutowashangaa wale wanaokumbatia huo uzembe kwa sababu wameukuta ukiwepo tangu kabla, hapa nawe ukiwa mmoja wao.
 
Wanatengeneza miradi yao kwasababu bosi wao hana shida, wanajua kila wazo watakalompelekea uwezekano wa kukubalika ni mkubwa, hapa ndipo watakapopata pesa wanazohitaji kufanikiaha malengo yao haramu, kama ya kugawa mitungi ya gesi bungeni tuliyoona hivi majuzi.
 
Wenye akili ya kuku hawajui kuwa wazo la umeme wa Stieglers Gorge lipo hata kabla ya uhuru.
Mwalimu alisha anza kuliweka kwenye bajeti kwa kuanzisha RUBADA.
Utoto nao mzigo.
Mkuu 'Jidu', miujiza isemwayo kuwa ipo ndiyo hii tunayoishuhudia mbele yetu sasa hivi.
Huko nyuma, enzi hizo za Magufuli, nilikuwa nikipingana nawe kumhusu huyo kiongozi, sasa hivi tumegeuza pande.

Ngoja nieleze kidogo: hata leo hii sikubaliani na mambo mengi sana, mambo mabaya aliyohusiana nayo Magufuli. Kuna mambo muhimu sana aliyo yafanyia uamzi, kama hilo la Rufiji, ni kati ya mambo ya kijasiri kabisa, yenye maono na kuyatimiza. Haya namtolea heshima yake anayoistahili.
Uthubutu wake katika mambo kama hayo ndiyo yanayomtambulisha kuwa tofauti na hawa wengine, na ndiyo maana inakuwa vigumu, pamoja na madhaifu yake mengi kumweka pembeni.

Kuna mambo aliipigania Tanzania kwa nguvu zake zote. Ninaunga mkono hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…