Hii video ina-trend ya namna kijana Ali alivyonyanyaswa na kubaguliwa Zanzibar

Hii video ina-trend ya namna kijana Ali alivyonyanyaswa na kubaguliwa Zanzibar

Ndugu

Tumlaumu Nyerere kwa upuuzi alioufanya......ukiangalia kwa umakini muundo wa muungano utagundua Nyerere alikuwa analazimisha!
Kuonewa huruma kutoka utumwani kwenye mikono ya Waarab waliokuwa wanawabagua ni kulazimisha muungano?
 
Kuonewa huruma kutoka utumwani kwenye mikono ya Waarab waliokuwa wanawabagua ni kulazimisha muungano?
Zanzibar walipata uhuru kabla ya huo muungano....... ukweli upo wazi Nyerere alilazimisha.....ndio maana wazanzibar waliabaki na serikali Yao....just imagine mtu wa bara hawezi kumiliki ardhi Zanzibar lakini wazanzibar wanaruhusiwa kununua na kumiliki ardhi bara....
 
Nimeiona hii video ya kijana Ali mwenye ulemavu na tatizo la kifafa. Nimesikitika sana alichofanyiwa na wananchi wenzetu wa Zanzibar.

Huyu kijana kwa wanaomjua wanasema amekulia Sinza na ni mlemavu kweli na amekua akiishi kwa kupata vibarua na kuomba msaada wa chakula na hela.

Udhalilishaji aliofanyiwa umeniacha na maumivu makubwa moyoni. Mtu hata kwa kumtazama usoni unaona dhahiri hayuko sawa na asiye na siha njema. Nimesawijika sana.

Wanasema amewaibia lakini hakuna uthibitisho wa hilo. Zaidi unaona ni chuki ya kwa kua ni mtu wa bara na zaidi ukisikiliza clip kwa uzuri kuna mtu anaropoka hawezi kua na msalaba huyo? Hiyo baada ya mmoja kumuuliza bwana Ali kuhusu mtu anaitwa Eric Masawe.

Nimekerekwa sana kwa udhalilishaji huu. Hii chuki ya dini ya mtu inatoka wapi? Asilani siwezi kumchukia mtu kwa dini yake hata kama si wa imani yangu na siafiki mambo juu ya imani yake. Kulikua na haja gani kutaja suala la msalaba?

Mimi kwetu Arumeru baba yangu alikua anakodisha ardhi kwa wazanzibari kiroho safi bila kujali dini zao wala utofauti wa makabila. Lakini, wenzetu hii chuki inatoka wapi?

Bwana Ali ametwezwa sana utu wake. Na huyu ni ndugu muislam vipi kwa asiye muislam? Hivi ndio dini inaelekeza? Kama mnaona kuomba anapata sana basi nanyi muombe muone kama ni jambo la kujivunia.

Wazanzibari mkae mkijua kama ni hasira zenu basi muipelekee CCM na sio wananchi wa kawaida. Huyo ndie adui yenu na adui wa kila mmoja wetu.

Ifike wakati mstaarabike. Dini badala ya kutujenga zinatufanya kuwa mafala na majinga.

View attachment 2977699
Tatizo hampendi kukubali ukweli, kila kitachofanywa na Mzanzibari mtakitafutia angle ya kukikosoa. Umejiuliza kwanini huyu mlemavu kama kweli kwao ni Sinza akaamua kuhama na mji akaenda Zanzibar kuomba? It's simple, wazanzibari ni watu wenye imani na utu na hiyo dini yao unayoiponda ndo inayowafunza hilo.

Upande mwegine nikuulize, ushawahi kumuona Mzanzibari ombaomba bara? pia ni dini hiyo hiyo inayomfundisha mwenye matatizo kuwa na kinaa na anachokipata lakini pia kutokana na misingi imara ya familia na udugu mara nyingi watu wa karibu wa watu kama hawa huchukua majukumu ya malezi juu ya watu wao. Au unadhani Zanzibar hakuna walemavu na wenye mahitaji?

Kuna swali alikuwa anaulizwa hapo ya kuwa huyo Erick massawe unaemtumia pesa kila siku ni nani yako? hili swali halina lengo la kidini bali linazua hoja ya kwamba huyu ombaomba anatuma pesa kila siku kwa mtu huyo Erick Massawe kitu ambacho kinaleta mashaka juu ya uhitaji wake huyu kijana! Ikiwa anacho cha kumtumia mtu kila siku then vipi anaendelea kuishi kwa kuomba? Pia hili swali linalenga kutaka kufahamu je huyu Erick Massawe ana uhusiano nae wa kindugu ama kuna miamala ya kibiashara kati yao? Kwahayo maswali mawili yanaleta mashaka juu ya uhitaji wa kweli wa huyu mtu na kumbuka ikiwa wanaompa wanampa wakiamini kuwa yeye ni muhitaji na hana msaada baada yao wao then inakuwa amewatapeli kwa kuwaaminisha uongo!

Sasa unaweza kusema kama wana mashaka si wasimpe tu! ... na hapa ndo unapokuja mzozo mkuu wa hili swala, huwezi kutoka kwenu na kuja Zanzibar kuchukulia advantage utu wa watu wake kwa tamaa zako, tena mpaka ifikie pahala ukaharibu utaratibu wa utu wa wazanzibari wenyewe! watu waache kuaminiana kwa tamaa zenu nyie? kwahiyo ndani ya ardhi yetu mnataka kutupa option ya either tukubali kutapeliwa au tukubali kubadilisha desturi zetu, hatutaki vyote! ikiwa mtu ni muhitaji atasaidiwa kwa kiwango kinachostahili na ndo maana huyo mtu hayajmtokea hayo siku ya kwanza tu! lakini ikithibitika kuwa anafanya biashara ya kuombaomba kama mradi basi hatutokubali!

Yote kwa yote, yoote yanawezekana. Ikiwa kweli huyo kijana ni muhitaji na hana budi isipokuwa kuomba then hawajamtendea haki lakini ikiwa huyo kijana amewafanya wazanzibari kuwa ni mtaji basi na yeye hajawatendea haki lakini pia hajajitendea haki na yeye mwenyewe pia kwa kuwa Uislamu umediscourage kuombaomba!

Busara itumike
 
Sitamani kwenda tena huko yaani mbara wanakuona kama kinyesi ukiwa Mkristo ndio balaa kabisa ukiwa hujashika dini inabidi udanganye jina Tu
 
Hatutaki muungano bila Tanganyika huru
Maneno haya hata Waccm waliopo humu wanakubaliana nayo 💯 % lakini kwa vile unasema wewe au mwenzao shati la kijani.
Sasa ayatamke Mbowe au Lissu utaona wanavyo ng'aka kama wameumwa na nyoka kalioni! Huyu ni mbaguzi, wanaleta vita nchini, nywe nywe nywe nk.
Lakini rohoni wanaumizwa na huo muungano na hawautaki.
Nakumbuka Lema aliwahi kusema bungeni jinsi wabunge wa ccm wanavyo msema Rais wao wakiwa canteen na kuwatuma wapige nyundo Samia lakini wakiwa ndani wanawapiga vijembe kama sio wao. Akawauliza sasa tutoe video tulizo warikodi mkimsema Magu(alipokuwa hai)?
Zaidi ya nusu ya wabunge na mawaziri kidogo wakate moto na kuzimia kama sio kufa kabisa, maana hakuna ajuaye nani karekodiwa.
CCM waache unafiki, wasemacho wapinzani kuhusu Muungano ndio ukweli.
 
Siongei mengi ila kuna clip zilirushwa wamekamatwa omba omba wengi toka bara ,kumbe wameletwa na mtu wafanye kazi ya kuomba na wanalipwa na nyumba ya kuishi wamekodiwa!
Huyo mgonjwa alifikaje znz? ...

Watu wamekuwa waoga sana .....wazanzibari wanaishi bara hawana fujo ..ila hao wengine mpaka ujambazi wa kuvamia sasa hivi znz upo!

Matatizo yapo ila kuna mengi yanachangia!
 
Back
Top Bottom