LGE2024 Hii ya Samia kupanga foleni kujiandikisha inafikirisha kidogo

LGE2024 Hii ya Samia kupanga foleni kujiandikisha inafikirisha kidogo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Elsa Marie

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2017
Posts
2,284
Reaction score
5,596
HIi imenishangaza yaani akili yangu imegoma kuelewa.

Yaani, mtu alikuwa anaelekea kujiandiandikisha kupiga kura, huko barabarani msafara wake umesababisha watu na magari kusimamishwa ili kuruhusu “mheshimiwa awahi” aendako (hili ni la ajabu pia lakini tumeshalizoea hakuna namna ya kulibadilisha kwa sasa)

Kilichonistaajabisha hadi kufikia kuandika huu uzi ni yeye baada ya kufika huko kwenye kujiandikisha eti akapanga foleni, yaani eti aliowakuta hawakumpisha.

Naona kama vile wananchi wamekosa adabu, iweje ushindwe kumpisha mheshimiwa apite mbele wakati huko barabarani watu wamempisha na kusababisha kuchelewa kwenye shughuli zao na wengine wagonjwa wamechelewa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu.

IMG_6522.jpeg
 
mamlaka zote za dunia zimetoka kwa Mungu. Na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Tii mamlaka bila shuruti, usijilazimishe kupata laana 🐒
Mimi sina tatizo na kutii mamlaka, nimeshangazwa na hao wapanga foleni kwanini wasimpishe mheshimiwa ahudumiwe haraka kama ambavyo wananchi wengine barabarani walimpisha bila tatizo?
 
mamlaka zote za dunia zimetoka kwa Mungu. Na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Tii mamlaka bila shuruti, usijilazimishe kupata laana 🐒
Kama kweli mamlaka za dunia zimetoka kwa Mungu. Iweje mamlaka hizo hizo zipingane baina ya nchi na nchi? Mungu anafitinisha mamlaka alizoziweka?
Au ni Mungiu yupi unamzungumzia?
 
Mimi sina tatizo na kutii mamlaka, nimeshangazwa na hao wapanga foleni kwanini wasimpishe mheshimiwa ahudumiwe haraka kama ambavyo wananchi wengine barabarani walimpisha bila tatizo?
jitahidi uwe unashiriki mambo haya ya kawaida mara kwa mara ili usishangae tena siku zingine...

halafu huwa unatumia nini kuwepo kwenye msafara wa viongozi, halafu tena wewe huyo huyo upo kwenye foleni ya kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wakati moja?

wewe ni mercenary sio ndani ya msafara?🐒
 
Sikuwepo kwenye msafara wa viongozi bali nilikuwepo barabarani ndani ya gari nikasimamishwa ili kumpisha., baada ya muda namuona kwenye vyombo vya habari kapanga foleni, what a joke!
 
Kama kweli mamlaka za dunia zimetoka kwa Mungu. Iweje mamlaka hizo hizo zipingane baina ya nchi na nchi? Mungu anafitinisha mamlaka alizoziweka?
Au ni Mungiu yupi unamzungumzia?
nchi na nchi ni falme ambazo ni familia ya Mungu, haziwezi kulingana kwa chochote. Chuki ni pepo linalowaingia viongozi wa nchi hizo na huwa ni ishara ulevi wa madaraka, kiburi na kutokumuheshimi wala kumkufuru Mungu 🐒
 
Back
Top Bottom