Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Siku za mwisho yametabiriwa haya,maandiko yapo wazi,acha watimize unabii ila kibaya wazazi ndio hawasomi maandiko na kuruhusu watoto wao kuchezewa bongo na kuachiwa mapepo wakue nayo,fuatilia hao watoto 10 yrs to come,utawaonea huruma
 
Kwanza usinibwatukie. Nikuulize kitu labda utajielewa na kuacha kubwatuka. Wakati wa ukuaji wako (utoto wako) uliwahi kushuhudia uotaji wa haya makanisa mitaani kama ilivyo sasa? Kulikuwa na makanisa rasmi na yanajulikana. Nadhani jibu umelipata.
Huyu uliemjibu hapo juu nae ana kanisa lake huko alipo ss unategemea atakuja hapa kusapoti hili suala?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo jamaa alikutana na kih fih rho hevi?
 
Mkuu serikali haina dini ila inatambua uwepo wa dini na imani za watu, na ndo mana ata mashuleni kuna muda umetengwa maalumu na kuingizwa kwenye time table kwa ajili ya vipindi vya dini.

Apo sidhan kama kuna tatizo
Acha kuchanganya mambo ndugu.
 
Tulishawapiga marufuku kuhubiri kwenye mabasi,bado hizo nyimbo.....
 
Hayo mambo huwa yanafanyika sana,au wewe ni mgeni wa hizi ishu? Au tatizo ni kuwekwa mtandaon.... Ungekuwa wazi kama unatetea faragha za watu au unapinga maombi yasiwepo school
 
Hata hao uliowasemea tunawapinga sana ila Masanja ameenda mbali zaid,kwanin aende shuleni hao ni watt isitoshe kuna wtt hawajalelewa kwenye hio imani anayoiamini yeye,serikali iangalie hilo jambo kwa jicho la tatu

Nb:hao wanaoenda huko kwa sijui mwamposa,kawa na sehemu waache wapigwe mpaka akili zitakapowakaa sawa
 
Siku za mwisho yametabiriwa haya,maandiko yapo wazi,acha watimize unabii ila kibaya wazazi ndio hawasomi maandiko na kuruhusu watoto wao kuchezewa bongo na kuachiwa mapepo wakue nayo,fuatilia hao watoto 10 yrs to come,utawaonea huruma
Inawezekana aiseee
 
Naipenda sana dini ya Kiislam huu uzuzu na uzwazwa haupo. Kila mtu anajifungulia kanisa lake kama nini sijui.
Unahaki ya kuipenda hiyo ndiyo dini yako,kuhusu Kila mtu kufungua kanisa,ni agizo la BWANA YESU mwenye,ukisoma Biblia kitabu cha Mathayo mlango wa 28,Mistari kuanzia wa 18,anasema enendeni ulimwenguni mkawafanye watu kuwa wanafunzi wangu......
Kwa mujibu wa hilo andiko huwezi ukawafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU kwa kufungua mabaa,inambidi mtu afungue kanisa ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU.
 
Amehamishia comedy kwenye dini?!
 
Ukiruhusu kila mtu akafanyie mambo ya dini yake shuleni kwa watoto wadogo itakuwa ni upuuzi.
Hayo hayakua maombi? Labda unataka serikali ipinge marufuku Dini za wenzetu, ndo jinsi wanavo omba brother
 
Shule za msingi na sekondari ni sehemu za watoto kusoma na kucheza tu sio kuendesha mambo ya kidini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…